Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 39,940
- 51,015
Ndugu zangu, nilishawahi kuandika humu namna mienendo ya ndugu yetu huyu Bwn. Lisu kuwa ni kuanza safari yake ya Urais 2020.
Narudia tena kuwakumbusha kuwa safari hiyo bado ipo na inaonekana wazi wazi kwa kauli zake na matendo yake kwa Rais wetu.
Kwa kuwa Lisu hana haiba wala mvuto wala ushawishi wa kuipata nafasi hiyo, ameamua kutumia staili ya kutoa kauli za kichochezi ambazo nimeipa jina la kauli za mlipuko.
Siasa za kauli mlipuko za Lisu zinalenga kuleta taharuki na kuchochea uma ili ijenge picha hasi kwa Rais na serikali anayoiongoza.
Kwakua aina hii ya siasa mlipuko ni ngeni kwetu, watu wengi wamekuwa wakishtushwa na kauli hizo na kusahau kufuatilia kauli hizo kama zina ukweli ama la?
Kwakua kauli anazotoa zinashtua muda wa kufuatilia kujua ukweli wa hizo kauli unakuwa mdogo na kauli zake zinasambaa na kubaki vichwani mwa watu kwa muda mrefu.
Kwakuwa wahenga wanasema Uongo huja kwa lifti na ukweli huja kwa kutumia ngazi, ni muda pekee ndio utakao mwacha Lisu katika Lindi la aibu ambalo tayari baadhi ya kauli zake zimeshaonekana kuwa zilikuwa ni za kichochezi na zimejaa uongo.
Hivi karibuni, Ndugu Lowasa aliamua kutangaza kuwa atagombea tena Urais ,2020.
Tangazo hilo bila shaka kabisa limemuacha ndugu huyu njia panda, na suluhu pekee ya kutetea haki yake ni kuja na kauli mlipuko ili kujibu mapigo kwa Lowasa. Lisu ameamua kabisa kuja na kauli mlipuko akijua kuwa kwa kufanya hivyo kwa kiasi flani atamtishia Lowasa ili kama akigombea tena amweke katika nafasi ambayo naye atapata chochote.
Tuendelee kushuhudia mfululizo wa kauli mlipuko toka kwa lisu ikiwa ni sehemu ya vita yake na lowasa kuelekea 2020.