Milipuko: Polisi yatangaza donge la Milion 10.

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Jeshi la polisi nchini limetoa donge nono la shilingi milioni kumi kwa mwananchi yeyote atakayefichua mtandao wa watu wanaotengeneza na kulipua mabomu katika mikusanyiko ya wananchi vitendo ambavyo vimekuwa vikiuwa na kujeruhi wananchi wasio na hatia.
Hayo yamesema na kamshina wa makosa ya jinai nchini (DCI) Isaya Mngulu alipokuwa akizungumza na waadishi wa habari jijini Arusha
Kuhusu hatua iliyofikiwa kuwatafuta watu waliohusika katika tukio la mlipuko wa bomu kwenye baa ya Night Park kamshna Mngulu amesema hawajapatikana na kwamba hata waliohusika kwenye matukio ya bomu katika kanisa la Olasiti na pia kwenye mkutano wa CHADEMA Soweto pia hawajapatikana japo amesema jitihada za kuwatafuta zinaendelea.
Katika hatua nyingine kamshina Mngulu amekiri kuwa changamoto bado ni kubwa katika kuwatambua watu wanaoendesha vitendo hivyo na ameendelea kuwaomba wananchi kusaidia kwa kutoa taarifa na kwamba hata ndani ya vyombo vya dola pia iko haja ya kujichunguza kwani haiwezekani vitendeo hivyo viendelee kutokea na wahusika wasipatikane.
Wakizungumzia vitendo hivyo baadhi ya wananchi wamelitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa hata kutoa taarifa za matukio ya milipuko ya mabomu kila inapotokea.
Siku ya tarehe 13/04/2014 majira ya saa moja na nusu ulitokea mlipuko katika baa ya Night Park iliyoko jijini Arusha uliojeruhi watu 17 likiwa ni tukio la tatu kutokea katika jiji la Arusha ambapo matukio mengine mawili ya milipuko ya mabomu yalitokea mwaka 2013
 
Askari Polisi kibao wanadai posho zao la likizo na nyongeza ya mishahara.
hizo ela kwanini wasipunguze madeni kwa kuwalipa askari polisi wao wanaowadai?
 
Jeshi la polisi nchini limetoa donge nono la shilingi milioni kumi kwa mwananchi yeyote atakayefichua mtandao wa watu wanaotengeneza na kulipua mabomu katika mikusanyiko ya wananchi vitendo ambavyo vimekuwa vikiuwa na kujeruhi wananchi wasio na hatia.
Hayo yamesema na kamshina wa makosa ya jinai nchini (DCI) Isaya Mngulu alipokuwa akizungumza na waadishi wa habari jijini Arusha
Kuhusu hatua iliyofikiwa kuwatafuta watu waliohusika katika tukio la mlipuko wa bomu kwenye baa ya Night Park kamshna Mngulu amesema hawajapatikana na kwamba hata waliohusika kwenye matukio ya bomu katika kanisa la Olasiti na pia kwenye mkutano wa CHADEMA Soweto pia hawajapatikana japo amesema jitihada za kuwatafuta zinaendelea.
Katika hatua nyingine kamshina Mngulu amekiri kuwa changamoto bado ni kubwa katika kuwatambua watu wanaoendesha vitendo hivyo na ameendelea kuwaomba wananchi kusaidia kwa kutoa taarifa na kwamba hata ndani ya vyombo vya dola pia iko haja ya kujichunguza kwani haiwezekani vitendeo hivyo viendelee kutokea na wahusika wasipatikane.
Wakizungumzia vitendo hivyo baadhi ya wananchi wamelitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa hata kutoa taarifa za matukio ya milipuko ya mabomu kila inapotokea.
Siku ya tarehe 13/04/2014 majira ya saa moja na nusu ulitokea mlipuko katika baa ya Night Park iliyoko jijini Arusha uliojeruhi watu 17 likiwa ni tukio la tatu kutokea katika jiji la Arusha ambapo matukio mengine mawili ya milipuko ya mabomu yalitokea mwaka 2013

Taarabu za serikali hizo,
waeleze kwanza walioitiwa hatiani kwa matukio ya olasiti na Soweto ni wa ngapi, na wananchi tujuzwe status za kesi kama hizo kesi zipo.

Mazoea huzaa tabia, njia pekee ya kukomesha mazoea ni kuwatia nguvuni wahusika, ila serikali ikiwa inaambia Taarabu namna ilivyozoeleka matukio haya hayatakoma na zaidi yataongezeka maradufu!

Itafika wakati watu wakifumaniana ni Mabomu tu kurushiana......serikali iache ngonjera ifanye kazi kwenye haya!
 
Hili Jeshi la polisi limejaa wapumbavu, toka milipuko imeanza kunayeyote aliekamatwa na kuthibitishwa. Wasipende kutoa kauli kimatukio ilikuonekana wanafanyakazi.
 
Si umeona walivyo jifanya kusawazisha mambo? Eti osama alijulikana lakini ilichukua miaka kumkamata.
 
Taarabu za serikali hizo,
waeleze kwanza walioitiwa hatiani kwa matukio ya olasiti na Soweto ni wa ngapi, na wananchi tujuzwe status za kesi kama hizo kesi zipo.

Mazoea huzaa tabia, njia pekee ya kukomesha mazoea ni kuwatia nguvuni wahusika, ila serikali ikiwa inaambia Taarabu namna ilivyozoeleka matukio haya hayatakoma na zaidi yataongezeka maradufu!

Itafika wakati watu wakifumaniana ni Mabomu tu kurushiana......serikali iache ngonjera ifanye kazi kwenye haya!

Naunga mkono mkuu tunataka matokeo ya matukio haya
 
mbona mwigulu mchemba hajakamatwa pamoja na kutajwa na kulalamikiwa.
 
DVR ya Chadema ina mkanda mzima wa walipuaji,mbona Mr.President haundi tume?au hana maslahi nayo?Maisha ya Watanzania yanaangamizwa huku wahusika waki endelea na maisha kanakwamba hakuna kilichotokea.Mungu wa Mbinguni anawaona.
 
Swala siyo kulaumu jeshi la polisi ila kuibuka kwa matukio ya namna kunaitaji ushirikishwaji wa umma wote katika kuwabaini na kuwakamata wote waliopo kwenye mtandao wa uhalifu huu
 
hapo ndo huwa napata homa nikisikia chadema wakitoa hiyo kauli,kwa nini wasitoe ushahidi kama wanao ili kuepusha matumizi ya kodi za wananchi na kuokoa muda pia, itakuwaje kama wananchi nao wakiwa wanagoma kutoa ushirikiano katika matukio kwa kisingizo kama hicho cha chadema, ni vizuri chadema wakajua kwamba mchango wao nao unahitajika na serikali na sio kubaki tu kuikomoa serikali
 
kwa hili mlaumu Rais kwani CHADEMA waliomba iundwe tume huru lakini mpaka leo kimya kana kwamba hilo jambo halimuhusu Rais. Huwezi kupeleka kesi ya mbuzi kwa fisi tena ya kumtuhumu fisi kula mbuzi.
 
Swala siyo kulaumu jeshi la polisi ila kuibuka kwa matukio ya namna kunaitaji ushirikishwaji wa umma wote katika kuwabaini na kuwakamata wote waliopo kwenye mtandao wa uhalifu huu

Mkuu ellypk Kwanza hongera kwa kujiunga JF na karibu sana!
Kwa sababu polisi wetu wanaishi kwa rushwa hivyo rafiki wa polisi wa Tanzania ni mwaarifu pekee maana ana sababu ya kumpa rushwa, raia wa kawaida ni Audi maana hana sababu ya kumpa rushwa polisi!
 
Last edited by a moderator:
katika hiyo milion 10 kwanza polisi wangenipaa advance au wangetoaaa advance kwanza....angalau 2mln tuwatafute hao walipuaji....si mnajuaa kuwa hunt hao ni garama..kna mafuta ya gari, vocha, kula, ssehemu ya kulalaa....haya nyie polisi toeni advnce
 
Back
Top Bottom