Milion mbili yatosha kuwa mtaji wa kuku wa mayai?

prince dudu

Senior Member
May 24, 2015
109
76
Habari zenu Wakuu,

Nahitaji kufuga kuku wa Mayai, ila sijui pa kuanzia. Naomba msaada wenu mnielekeze ili niweze fanikiwa lengo langu.

Je Nikiwa na milion mbili yatosha kuwa mtaji wa kuku wamayai?
 
Last edited by a moderator:
Je, Una Eneo La Kufugia ... Je, Umeshajenga Banda ... Je, Idadi Gani Ya Kuku Unaotaka Kufuga ... Je, Umeshawahi Kufuga Au Ndo Unaanza ... Je, Uko Tiyari Kukabiliana Na Changamoto Za Ufugaji ... Ukinijibu Maswali Haya Ndo Tutajua Pakuanzia ...
 
Mkuu masuali mazuri

Miezi 3 ilopita, nimechinja kuku karibia 200 wa mayai, walipata maradhi ya kiharisha, nimetumia dawa zote haikusaidia, kila siku kuku 2au 3 walikuwa wanakufa, nikaona watamalizika, nikachinja na kuwauza.

Miaka 25 au zaidi tunafuga kuku nyumbani, lakini tatizo kama hili sijawahi kuona, it's too much.
 
Habari zenu Wakuu,

Nahitaji kufuga kuku wa Mayai, ila sijui pa kuanzia. Naomba msaada wenu mnielekeze ili niweze fanikiwa lengo langu.

Je Nikiwa na milion mbili yatosha kuwa mtaji wa kuku wamayai?
inafaa kwa kuku 200 kama banda unalo.
 
Mkuu masuali mazuri

Miezi 3 ilopita, nimechinja kuku karibia 200 wa mayai, walipata maradhi ya kiharisha, nimetumia dawa zote haikusaidia, kila siku kuku 2au 3 walikuwa wanakufa, nikaona watamalizika, nikachinja na kuwauza.

Miaka 25 au zaidi tunafuga kuku nyumbani, lakini tatizo kama hili sijawahi kuona, it's too much.
Pole Sana Mkuu Hao Kuku Wako Walikuwa Wanaharisha Uharo Wa Rangi Gani
 
Last edited:
Habari zenu Wakuu,

Nahitaji kufuga kuku wa Mayai, ila sijui pa kuanzia. Naomba msaada wenu mnielekeze ili niweze fanikiwa lengo langu.

Je Nikiwa na milion mbili yatosha kuwa mtaji wa kuku wamayai?
kwa ninavyosikia mkuu hao kuku changamoto zake anza na kuku kama 20 hivi ili usije juta
 
Ukiamua kufuga kibiashara anza na hao 200 huku ukiendelea kujifunza kwa Tuliokutangulia kiuzoefu,chini ya Idadi hiyo ni hasara kwa faida yako Kuku awe wa mayai au wa Kawaida huanza kutaga kuanzia miezi mitano au sita kama atalishwa na kutunzwa vizuri. Sasa kufuga 100 au chini ya hapo kwa miezi hiyo utakuwa umepoteza muda mrefu.
 
Inaonekana una uzoefu kidogo. Humu watu wengi naona wanazungumzia sana kuku wa mayai kuliko wa nyama. Mimi napenda nianze na kuku wa nyama coz wanatumia muda mfupi mpk kuuza. Unashauri idadi ipi inafaa kwa kuanzia?
 
Mi nafatilia mjadala huu nijifunze kitu
 
Kwa huo mtaji wako kuku 200 haitafaa kwa sababu, hapa kwa huo mtaji ni kama una kila kitu on handa yaani hiyo pesa ni ya. watunza tu.
ila kama hiyom pesa ni:
- Kununua vifaranga
-Kununulia chakula
-Madawa
- Na kazalika basi haitatosha

Kuku wa mayai wana kula sana

kifaranga anakula grama 60 kwa siku
Kuku wanao kuwa wanakula hadi gram 90 kwa siku
Kuku wanao taga wanakula gram 140 kwa siku

sasa piga hizo gram

200 x 60 = 12 kg piga na bei yake mara siku zake

200 x 90 gram= 18 kg per day

200 x 140 gram= 28 kg per day
 
Umenitisha. Nilidhani kuku 200 ni wachache. Je unashauri mtu kama hana experience aanze na wangapi?
aisee sikutishi, kuku wana complications nyingi sana, usije ukasoma tu hapa j.f, watu wanakuambia inalipa inalipa, wewe ukaenda kujitumbukiza full ukitaka faida ya haraka haraka, utakuja kulaani ufugaji hadi uape kutofanya tena
anza na kuku wachache kwa 2 mil nakushauri wasizidi 50
huyo anaekwambia wachache watakupotezea muda sijui kama anajua changamoto kwa wajasiriamali wageni kwenye kilimo/ufugaji
tumia muda mwingi ufanye kitu ambacho utakua na uelewa nacho wa kutosha kinadharia na kivitendo pia
halafu kumbuka kwa ujasiriamali hasa wa kilimo au ufugaji usitake kupata faida kubwaaa pale mwanzoni, anza na kidogo hata ukipata faida kidoga au usipopata faida kabisa lakini utakua umepata knowledge na kujiepusha na hasara nyingine kubwa zaidi
 
Mkuu hao 50 unaomwambia aanze nao ni wepi!. Labda wa kienyeji, lakini si wa nyama au mayai andika Hasara. Kingine kwa Mjasiriamali mfugaji, hakuna mfugo usio na hasara. Wajasiamali msisahau hii pia na biashara ambayo lazima kuna kipindi lazima changamoto ziwepo.Na kama ufugaji upo kwenye Damu hutaacha
 
wa kisasa/wa kienyeji bruh, lengo lake sio faida, bali aone jinsi ufugaji ulivyo ki ukweli ukweli, faida ataanza kuitafuta round ya pili baada ya kujua changamoto zake nje na ndani kwenye round ya kwanza, nimempa hiyo idadi ndogo kwa kua mtaji wake ni milioni 2, ili zisije zikaishia hapo
 
Mkuu nukubaliane na mawazo yako, maana hapa nia ni katika kujenga mnara wa wajasiriamali. Ahsante
 
Back
Top Bottom