Kutokana na changamoto ya muda mrefu wanayopitia wananchi wa kata ya Mahuninga halmashauri ya wilaya ya Iringa Mkoani ya kufuata huduma za afya umbali mrefu uenda ikabaki historia mara baada ya kutengwa kiasi cha sh milion 600 kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha afya.
Kituo hicho kinajengwa ili kusaidia upatikanaji wa huduma za afya kwa jamii ya kata hiyo na maeneo jirani ambapo takribani wananchi 6842 watapata huduma katika kituo hicho awali iliwalazimu kutembea umbali mrefu.
Wakiwa katika ziara ya ukaguzi maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Isimani Amos Ndasso akiambatana na Afisa Tarafa, Tarafa ya Idodi Mapessa Makalla pamoja na Katibu wa hamasa na uhamasishaji Wilaya ya Iringa Omary Chulla wameridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo na kuagiza kasi zaidi ili mradi ukamilike kwa wakati.