Milio ya risasi yasikika nje ya Bunge Uingereza

Ava Sancez

Member
Jan 27, 2017
33
50
Taarifa zinasema kumetokea milio kadha ya risasi nje ya majengo ya Bunge la Uingereza.

Eneo hilo kwa sasa limefungwa na watu hawaruhusiwi kutoka wala kuingia.

Wanasiasa na wanahabari wamekuwa wakiandika kwenye Twitter kwamba wamesikia milio mikubwa nje ya majengo hayo.

Walioshuhudia wanasema wamewaona watu kadha wakipokea matibabu.

Baadhi ya walioshuhudia wanasema wamemuona mtu akiwa na kisu katika bustani ya majengo ya bunge.

Afisa wa polisi ameambia mhariri wa BBC wa masuala ya siasa Laura Kuenssberg kwamba kuna mtu aliyepigwa risasi nje ya Jumba la Portcullis.

Chanzo: BBC
 
Kumekucha....wale watu wa mashariki ya kati wenye Majini ya kunywa damu za watu wameanza
 
Back
Top Bottom