Taarifa kutoka Nigeria zinaeleza kuwa kituo cha polisi kimeshambuliwa pamoja na shule ya msingi na milingoti minne ya simu, katika mji wa Fika, kaskazini-mashariki mwa nchi.
Wakaazi wa mji wanasema mabomu yalirushwa kwenye sehemu hizo leo asubuhi.
Taarifa zinasema askari polisi wanne wamekufa.
Majimbo ya kaskazini mwa Nigeria yameathirika vibaya katika miaka ya karibuni kutokana na ghasia zinazofanywa na kundi la la Boko Haram.
Mwezi Septemba kundi hilo lilishambulia zaidi ya milingoti 40 ya simu za mkononi na kuchimbua makaburi ya wakristu.