Miliki Watu Upate Utajiri

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
July 2019

MILIKI WATU UPATE UTAJIRI.

Na. Robert Heriel.
Reposted.

Kama kuna siri watu hawataki kuisema kuhusu utajiri basi ni hii hapa. Siri ya kumiliki watu. Huwezi kuwa tajiri bila kumiliki watu. Na hakuna tajiri yeyote duniani au nchi tajiri yoyote duniani bila kumiliki watu.

MAANA YA KUMILIKI WATU
Kumiliki mtu ni kumtawala yaani ni kumfanya mtu kuwa mali yako na kuitumia katika shughuli zako. Mtu unaweza kummiliki katika nyanja zifuatazo, Kummiliki kiakili, Kiimani, Kimwili, Kihisia, Kisiasa na kiuchumi. Ili uwe tajiri lazima uchague Kategori ya kumiliki watu.

Na katika huu Ulimwengu lazima uwe Mmiliki au mmilikiwa. Yaani lazima kuna watu unawamiliki au wanakumiliki. Ukimiliki watu basi ni wazi utakuwa ni tajiri. Ukimilikiwa ni wazi utakuwa masikini na kama utakuwa na maisha ya kati hii ni matokeo ya kujipendekeza kwa wamiliki watu.

Kumiliki watu ni kumiliki muda. Kwani utakuwa unatumia Mida yao kujizalishia mali. Kama unamilikiwa na mtu basi muda wako utakuwa unatumiwa na mtu anayekumiliki.

Zamani watu walinunua Watumwa na hata baadhi ya nchi zilifanya biashara hii ya utumwa. Zilinunua watumwa kutoka nchi nyingine. Hii ilipelekea nchi hizo kupata Manpower ambao walizalisha na kuzifanya nchi hizo kuwa nchi tajiri. Kupitia kumiliki watu nchi kama Misri ya zamani, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zilinufaika na kuneemeka.

Pia kuna hadithi za jadi kuwa Baadhi ya watu wachawi humiliki misukule ambayo inawasaidia kulima mashamba makubwa na kazi zinginezo. Ikumbukwe kuwa Misukule pia ni Kumiliki watu kwa namna ya kichawi. Zipo hadithi zingine zinaeleza kuwa wapo wafanyabiashara wanaotumia misukule AKA ndondocha kujitajirisha. Kanuni ni ile ile Miliki watu upate pesa.

Hata wasanii wakubwa wanahangaika kutwa kucha kupata Mashabiki wa kuwamiliki Kihisia ili wapate pesa. Bila kuwa na mashabiki ni wazi kuwa msanii hawezifika popote. Kwani siku za kupiga shoo ukumbi hautajaa lakini kama anamiliki watu kihisia ni wazi kuwa siku akisema ninashoo mahali fulani utaona watu wanajaa Na kutoa muda wao na pesa zao.

Tunaona Hata kwenye ishu ya michezo hapa nchini Club ya Simba inamiliki washabiki wengi hivyo huwapelekea kupata pesa ndefu. Hii imekuwa changamoto kwa timu zisizomiliki watu.

Ukija kwenye Siasa Chama Cha Mapinduzi CCM kinamiliki watu wengi ndio maana ni chama chenye nguvu na kina miradi mingi kutokana na pesa za wanachama. Vyama vingine vinapata changamoto nyingi kutokana na kuwa havina Mtaji wa watu. Havimiliki watu hivyo ni kusema havina nguvu.

Kwenye suala la imani. Ili dini iwe tajiri inahitaji waumini wengi. Hapa ndio tunaona Dini ya Kikristo mathalan Dhehebu la Roman Catholic lilivyo na utajiri wa kufa mtu. Tunaona dhehebu hili lina miradi kama shule karibu dunia nzima, Huduma za Afya na Makanisa ya gharama. Hawa walijua siri ni kumiliki watu ndio maana enzi za zamani walitumia mbinu za aina zote kuhakikisha wanapata waumini wengi. Leo wanakula bata. Tunawaona kina Bishop Josephat Gwajima, Anthony Lusekelo, Mch. Kakobe na Mwamposa wakipiga pesa. Hii ni kutokana na wanamiliki watu kiimani. Usishangae wakinunua madege au majumba ya kifahari. Hao wanajua siri ya kumiliki watu.

Ukitaka kupata utajiri wala usihangaike. wewe Miliki watu hapo ndipo utajiri ulipo. Ukimiliki watu umemiliki akili mbalimbali, Umemiliki maelfu ya muda. Kumbuka maisha ni mafupi hivyo kumiliki mida ya watu wengine unaongeza chance ya wewe kuyafanya maisha yawe marefu hasa kwenye utajiri. Utakuwa umemiliki mawazo mengi. Utakuwa umemiliki nguvu nyingi. Bila kumiliki watu ni kujihangaisha tuu hutaambulia lolote katika ulimwengu huu.

Hata ugundue nini. Kama hakuna watumiaji wa kitu hicho utaendelea kuwa masikini. Hata tajiri wa dunia Billgate baada ya kugundua program ya Microsoft kama wasingekuwepo watumiaji yaani watu basi ni wazi angeendelea kuwa masikini tuu.

MBINU ZA KUMILIKI WATU
Utawezaje kumiliki watu ili uwe tajiri. Zipo njia mbalimbali zitakazokufanya umiliki watu na uwatawale ile baadae wawe watumwa wako ujipigie pesa. Mbinu hizo ni;

1. TENGENEZA MBINU BANDIA YA KUTATUA MATATIZO YAO
Hii mbinu inahusiana zaidi na mambo ya hospitalini na Masuala ya vita. Ishu ya magonjwa kama UKIMWI si kwamba dawa haiwezi kupatikana au haipo. Dawa ipo na inaweza kupatikana sema ili watu fulani waendelee kupiga pesa sharti Dawa za kuzuia makali ziwepo ilhali uwezekano wa kupatikana dawa kamili Upo. Ishu ya vita. Si kwamba vita haviwezi kuisha bali katika vita kuna fursa kibao za kupata utajiri.
Mbinu inayotumika ni kuuza silaha wakati mbinu halisi ni kuacha kutengeneza silaha kisha kusuluhisha kwa amani.

2. AJIRI WATU
Njia hii itakusaidia kupata watumishi watakao kuzalishia mali. Hapa utawapa ujira kulingana na watakavyo zalisha. Mbinu hii naiita Utumwa wa hiari. Ukiajiri watu kuanzia watano kuendelea ni lazima upate pesa. Hakikisha unaowaajiri watumike kuzalisha mali na si kukuhudumia kwa mambo ya anasa kama vile ngono.

3. KUWA BINGWA WA UTAPELI
Hapa lazima umiliki watu wengi zaidi. Njia hii inatumiwa zaidi na Waganga wa Kienyeji AKA Sangoma, Manabii wa kileo na MaBishop, Wanasiasa miongoni mwa watu wengine. Njia hii hutumia ulaghai hasa kwa mambo yasiyowezekana kuyafanya yawezekane mdomoni ilhali kihalisia huwa magumu kufanyika. Hii hutumiwa na wanasiasa kipindi cha Kampeni ambapo huwatapeli wananchi kwa ahadi za uongo. Na hapo hupata wafuasi na kujipatia utawala kisha pesa nje nje. Huko kwa Manabii ndio kabisa ulaghai nje nje.

4. TOA HUDUMA BORA
Hii huwahusu Wafanyabiashara na watoa huduma. Pia Wanamuziki na Wasanii huangukia kundi hili. Toa huduma makini na bora ambayo watu wakiipata wawe wateja yaani watumwa wako. Bila kutumia bidhaa au huduma yako hawajisikia raha. Kama ni Dereva bodaboda, au daladala au mabasi. Toa huduma nzuri. Kuwa na kauli njema na uso wenye bashasha. Vaa upendeza na kuwa msafi. Utashangaa unamiliki watu. Yaani bila wewe wanahisi watapata ajali njiani. Halikadhalika na Mama Ntilie, Vinyozi, Fundi nguo, N.k. Wasanii kama kina Diamond na Kiba. Ukimiliki watu umemiliki dunia.

5. TAFUTA ADUI BANDIA NA UNDA UHASAMA
Ili uweze kumiliki watu basi tafuta adui bandia hapo unapoishi na uunde uhasama bandia. Hapa utapata makundi mawili. Moja linakusapoti wewe jingine halikusapoti. Hapa utapata wafuasi na utapata unayoyataka. Hapa ndio tunaona uhasama bandia baina ya UBEPARI na UJAMAA, Ukristo Via Uislam, Shetani Via Mungu, CCM Via Upinzani, ALI KIBA Via Diamond n.k

Miliki watu upate pesa

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi
0693322300
 
Pesa zipo kwa watu. Unakuta mtu ni customer care, au yupo kitengo cha upokeaji simu za idara au shirika, taasisi halafu nyodo kibao kupokea simu, au yupo reception nyodo kidogo huyu mtu anapishana na utajiri. Miliki watu umiliki pesa, watu wanahitaji msaada wako na sio sura yako, wateja wanapiga simu upokei, then unalia umasikini, Mungu akupe nini sasa, Tumia watu fanya connection na watu upate pesa. Kitengo chochote kinachokukutanisha na watu ni utajiri.
 
Ni kweli kabisa..

Kwenye swala zima la mafanikio "corporation" ya watu ni kitu muhimu sanaa sanaa.

Utakuwa unajidanganya kuamini kwamba utaweza kufanikiwa wewe kama wew bila umoja wa watu wengine...
 
Pesa zipo kwa watu.
Unakuta mtu ni customer care, au yupo kitengo cha upokeaji simu za idara au shirika, taasisi halafu nyodo kibao kupokea simu , au yupo reception nyodo kidogo huyu mtu anapishana na utajiri. Miliki watu umiliki pesa, watu wanahitaji msaada wako na sio sura yako, wateja wanapiga simu upokei, then unalia umasikini, Mungu akupe nini sasa
Tumia watu fanya connection na watu upate pesa. Kitengo chochote kinachokukutanisha na watu ni utajiri.
For sure
 
Ni kweli kabisa..

Kwenye swala zima la mafanikio "corporation" ya watu ni kitu muhimu sanaa sanaa.

Utakuwa unajidanganya kuamini kwamba utaweza kufanikiwa wewe kama wew bila umoja wa watu wengine...
Mkuu siyo rahis kihivyo. Tatizo mmatumbi mbishi. Njia rahis kwa mmatumbi kummiliki ni kumshushia mkong'oto tu wa haja. Ukimbembemveleza bembeleza sijui customer care sijui ukarimu mmatumbi atakuzoea na kufikia hatua ya kukupanda mabegani.

Uzuri wa mmatumbi ana nguvu mdomoni tu lakini mwoga kichiz ukimchimbia mkwara jinsi Jiwe alivyokuwa anafanya hadi akatudhibiti na kutumiliki watu zaidi ya million 60 kwa mikwara tu na vitisho.

Mjerumani alishatusoma akatuona Hawa ukicheka nao watakuzoea sana hata kuwashikashika madem zetu akawa anatembeza mboko na mkong'oto na mambo yakaenda.

Yani inachotakiwa unatafuta manigger wachache makatili na kiherehere kama makonda na Sabaya wewe unawatuma tu to create fear and havoc huku wewe unadelegate tu. Mbona utamiliki tu maboya wengi tu kama kina nyboma Mr Dudumizi na Stuxnet
 
Ni kweli kabisa..

Kwenye swala zima la mafanikio "corporation" ya watu ni kitu muhimu sanaa sanaa.

Utakuwa unajidanganya kuamini kwamba utaweza kufanikiwa wewe kama wew bila umoja wa watu wengine...
Jiulize kwanini wahindi hawana iyo micustomer care sijui cooperation na wamatumbi. Mmatumbi ukifanyia hayo yote huwezi kummiliki. Mmatumbi ana tabia ya pekee ya kuzaliwa ( strange peculiar behavioral character ) Dawa pekee ya mmatumbi kummiliki ni kucreate na kuimpose fear. Wahindi kwenye viwanda vyao hawana time na micustom care wanatafuta manigger flani mikatili na viherehere na kuwapa usupervisor hayo manigger ni makatili kuliko hata Wahindi wenyewe waonevu kichiz hao sasa ukiwapata wewe unadelegate. Hakuna kuchecheka na mmatumbi.
 
Mada nzuri lakin mwandishi hauja ichambua vizuri. Umeandika haraka kama unakimbizwaa na hii pia ni changamoto. Mada nzuri sana kama angeweza kuichambua.
 
Back
Top Bottom