Mikorosho ya kisasa

Mikorosho ya kisasa

Natafuta mikorosho ya kisasa nitapataje mwenye kujua pakuipata ani pm

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu kama bado hujafanikisha ni-PM nikuunganishe na jamaa mmoja hivi yupo NEWALA anatumiwa na watu BODI YA KOROSHO kuzalisha miche ya wakulima.
kwa mwaka yeye tu anaweza kuzalisha zaidi ya miche laki 8.
 
nanjinji -nimeku pm naona msg haijakubali nilihitaji connection na Huyo jamaa yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Nlikujibu mkuu na nimekuuliza maswali kadhaa lakini umeshindwa kujibu.
Twende PM au jibu hapa suala shamba lako lilipo ili nimueleze jamaa kama anaweza kufika huko kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu pia.
 
Kakak
Nami ningependa kupata msaada huo nahitaji miche



Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna mkuu,
shamba lako liko wilaya gani na lina ukubwa gani..?
nakuuliza hivi kwa sababu za kitaalamu na jamaa anapokea order nyingi pia hivyo inakuwa rahisi kwake kupanga route za upande mmoja.
Kesho BODI YA KOROSHO inapanga bei elekezi huko makao makuu ya Mtwara
 
Kwani hii miche ambaya serikali inagawa bure sio bora?
Sisi tumesha pewa na tumesha ipanda mwaka jana..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni bora na nakumbuka mwaka jana walianza wilaya ya Ruangwa kwa kugawa miche bure,
kuwa na amani tu mkuu, ila kinachofanyika Bodi ya korosho wanawatumia watu waliopewa mafunzo ili kutengeneza vitalu kwa ajili ya kuotesha miche ambayo baadae inaenda kwa wananchi bure lakin hawapati wote si unajua tena kitu cha bure..
Bei dira mwaka ni Tzs 1450 kutoka ile ya mwaka jana Tzs 1300.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom