Mikopo ya NSSF kwa wanachama ni ubabaishaji!

kande kavu

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
234
86
Habari wana jamii/ NSSF Staff.


Mimi ni mwanachama wa NSSF kwa kipindi cha miaka 15 sasa. Hivi karibuni mfuko wetu huu ulitangaza kuwa utaanza kutoa mikopo kwa wanachama wake kupitia SACCOS tena kwa riba ndogo! Tangazo hilo kama sikosei lilianza kutolewa mwezi wa Mei mwaka huu, ikiwapo utaratatibu wote wa kupata mikopo hiyo (MWANACHAMA-SACCOS).


La kusikitisha, mimi na SACCOS yangu tumekamilisha utaratibu wote tangu mwezi Agosti lakini mkopo hautoki wala hakuna taarifa ya nini kinaendelea mpaka tumeingia mwezi Disemba. Ifahamike kuwa wengine hatukopi ili tucheze ngoma, bali kuimarisha biashara zetu. Hiyo pesa niliyoomba sipewi bure,na kwa kutangaza riba ndogo kuliko ya SACCOSS yangu au mabenki, mlinifanya niweke mipango yangu ya biashara kwa kukopa kwenu! Lakini ona mlivyonipotezea muda na biashara, si bora ningekopa kwenye riba kubwa lakini nikapata mkopo ndani ya siku kumi! Ya nini kuamsha tamaa na matumaini hewa kwa wanachama kama hamko tayari?

MMENIVURUGA!
 
Mfuko wa NSSF hauko kuwanufaisha wafanyakazi bali uko kwa ajili ya kuwanufaisha watu wengine ambao hawachangii huu mfuko kama wafanyabiashara na viongozi wa serikali wanaokopa pesa kutoka kwenye huo mfuko.
 
Mfuko wa NSSF hauko
kuwanufaisha wafanyakazi bali uko kwa ajili ya kuwanufaisha watu wengine
ambao hawachangii huu mfuko kama wafanyabiashara na viongozi wa
serikali wanaokopa pesa kutoka kwenye huo mfuko.

Thumb up ! NSSF ipo kwa maslahi ya mafisadi lakini wachangiaji hatuna chet...na sasa nasikia bunge lijalo wanandoa fao la kujitoa wenye aina fupi tumemaliza.
 
Back
Top Bottom