Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Nilikuwa nazungumza na jamaa yangu mmoja mjini Mwanza ambaye pia ni Afisa wa benki ya NMB.
Pamoja na mambo mengine tulijadiliana kuhusiana na sakata la vyeti feki.
Jamaa anadai katika taasisi yake kuna watumishi wengi waliokumbwa na sakata LA vyeti feki ambapo sintofahamu kubwa imeibuka miongoni Mwa taasisi nyingi za kifedha. Katika kuthibitisha hilo karibia benki zote zime share internal memo kuhusiana na majina ya watumishi wenye vyeti feki kusudi maafisa wachukue tahadhari wasijeingizwa mjini.
Pamoja na hilo bado hasara IPO mlangoni mwa taasisi nyingi za kifedha.
Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za ukopeshaji kwa watumishi wa umma, mwajiri (serikali) ndiye Mdhamini mkuu wa mwajiriwa hivyo mtumishi anakopa na kudhaminiwa na mwajiri kupitia mshahara wake.
Ukiacha hilo katika mikataba mingi utakuta mkopaji anatoa tamko kwamba ikitoa akashindwa kulipa basi pensheni yake italipa na mwajiri huthibitisha hilo.
Sasa kwa hawa ndugu zetu itakuwaje maana hata pension hazitabiriki.
Pia, halikuwa kosa LA taasisi za kifedha kuwakopesha watumishi wenye vyeti feki ambao mamlaka ilithibitisha kuwa ni halali na wanakidhi vigezo vya kukopeshwa.
Tujadili...nani atalipa MIKOPO hiyo?