Mikopo ya BAYPORT

okonkwo jr

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
2,419
1,737
Natumai hamjambo waungwana,mimi ni mwajiriwa serikalini,sijathibitishwa kazini bado,hoja yangu ni kutaka kuchukua mkopo kupitia bayport kiasi cha sh miliion tano na nusu,na nataka kuurejesha ndani ya miaka mitatu,take home yangu ni sh laki tano.je itanigharimu kiasi gani mpaka kuukamilisha kwa muda huo wa miaka mitatu? Naomba msaada na changamoto za hawa jamaa wa bayport,lengo la mkopo ni kununua nyumba.
 
Hapo ndugu jiandae kurejesha milioni 15. Riba za hao jamaa ni kubwa sana.
Ila nenda ofisini kwao ukajiridhishe zaidi
 
Ukikopo 5.5ml utalipa 11ml. Kwa ujumla hawafai hawa, kimbia
 
hivi kwa mfano ukakopa hiyo m 5 halafu ukafanikiwa kuwekeza kitu ambacho baada ya hiyo miaka mitatu kitakupa faida ya zaidi ya Hayo m 15 watakayokata,hasara iko wapi?
Ishu ni kuchukua mkopo kwa malengo na siyo kukurupuka
 
Lengo la mkopo sio biashara bali ni kununua nyumba
 
Kjana kimbia haraka sana! Hao siyo watu ni hatari, nenda NMB wanakopesha kwa barua ya ajira tu, kuna jamaa alikopa Mil 1.6 akarejesha mil 6, hawa jamaa hawafai hata kidogo

Bado hatujapewa barua ya uthibitisho kazin mpaka one year!
 
Back
Top Bottom