Mikopo ya Bajaji na Pikipiki ni komesha!

Mikopo ya Bajaji na Pikipiki ni komesha!

Leo nimepita Sabasaba nikaona kuna Kampuni fulani (Jina Kapuni) inatoa mikopo ya Pikipiki na Tukutuku.

Mjanja M1 nikajisogeza taratibu kuokota Dodo la mkopo wa Bajaji.

Lahaullah Walakuwata! nilishtuka sana kuambiwa marejesho ni zaidi ya ulichokopa, yani kama umekopa 10 Million wanakutaka urejeshe 21 Million.

Nikawaambia Asanteni sana na nikatoka Nduki mithili ya Hussein Bolt wa Jamaica.

WATOA MIKOPO WANAWAKOSEA SANA WATANZANIA.
Uliagizwa ama ulienda mwenyewe kwa Hali yako chief
 
Ungetaka kucheka ungechekea tumboni ili kuwaonesha kwamba hesabu unazijua.

Nilifikaga ofisi fulani wanakopesha pikipiki, aise ni bora ukakope pesa benki ndio ukanunue ulipe benki mdogo mdogo kwa miaka miwili.
Sema tu watu wengi hawakidhi vigezo vya kukopa benki ndio maana makampuni ya kijanja yana-take advantage.
Vigezo ni vipi?
 
Simu cash inauzwa 200000 ukikopa utalipa 260000 kwa mwaka
 
Back
Top Bottom