Mikopo mibaya, Benki ya wanawake, Efatha na Ecobank hatarini kufungwa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
pic+benki+kufungwa.jpg

  • Twiga Bancorp, ambayo kwa sehemu kubwa inamilikiwa na Serikali, imewekwa chini ya uangalizi wa BoT baada ya madeni yasiyolipwa (NPL) kuzidi kiwango kinachotakiwa kisheria.

Dar es Salaam. Hali ya mtikisiko wa uchumi uliozikumba taasisi nyingi, hasa za fedha sasa unazinyemelea benki tatu ambazo zinaweza kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama ilivyokuwa kwa Twiga Bancorp.

Twiga Bancorp, ambayo kwa sehemu kubwa inamilikiwa na Serikali, imewekwa chini ya uangalizi wa BoT baada ya madeni yasiyolipwa (NPL) kuzidi kiwango kinachotakiwa kisheria.

Hali hiyo inazinyemelea taasisi nyingine tatu za fedh; Benki ya Wanawake (TWB), ambayo pia inamilikiwa na Serikali, Ecobank Tanzania na Efatha Bank, ambayo inahusishwa na taasisi ya kidini ya Efatha, kwa mujibu wa uchambuzi wa The Citizen ambalo ni gazeti dada la Mwananchi.

Benki hizo tatu zimelimbikiza kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 50 ya jumla ya mikopo iliyotolewa, huku kiwango cha Efatha kikifikia asilimia 63.

Wataalamu wa benki wanaamini kuwa kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 15 ya jumla ya mikopo yote ya beki za biashara, kinaashiria uwezekano wa kuanguka.

Katika toleo la tisa la Hali ya Kiuchumi Tanzania, Benki ya Dunia ilitahadharisha kuhusu kukua kupita kiasi kwa kiwango cha NPL, ambacho kilifikia asilimia 9.5 mwaka 2016 kutoka asilimia 6.4 mwaka 2015.

Ripoti hiyo iliitaja TIB Development Bank ambayo kiwango chake cha NPL kilikuwa asilimia 38 katika robo ya kwanza ya mwaka 2017.

Hata hivyo, taarifa za fedha za benki za biashara za robo ya kwanza mwaka 2017 zinaonyesha hali ni mbaya zaidi kwa Efatha, TWB na Ecobank Tanzania.
 
The Citezen la leo lina habari kuhusu hali mbaya ya mabenki kutokana na bad loans.
 
Magufuli aanze kutumia sheria kuwafunga CEOs wa haya mabenki yenye madeni yasiyolipika kwa wingi. Mengi yanatoa mikopo kwa misukumo ya rushwa kwa maafisa mikopo bila kufanya assessment na analysis za kutosha za wateja. TWB na TIB ni hela za kodi zetu wafungwe hao
 
pic+benki+kufungwa.jpg
...

Wataalamu wa benki wanaamini kuwa kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 15 ya jumla ya mikopo yote ya beki za biashara, kinaashiria uwezekano wa kuanguka.

Katika toleo la tisa la Hali ya Kiuchumi Tanzania, Benki ya Dunia ilitahadharisha kuhusu kukua kupita kiasi kwa kiwango cha NPL, ambacho kilifikia asilimia 9.5 mwaka 2016 kutoka asilimia 6.4 mwaka 2015 ...

Return Of Undertaker: watendaji wa benki husika wanapashwa kujiuliza wenyewe kwa nini kiwango cha 'NPL' kinaongezeka.

Mimi siyo mtaalamu wa uchumi ila hatua za Serikali za kuziba mianya ya fedha chafu na utakatishaji wake ni moja ya sababu kuu.

Ikumbukwe pia kuongezeka kwa 'NPL' ni uzembe wa watendaji wa hizo benki au utaratibu/mfumo wa ukopeshaji. Hii inaweza kuthibitishwa na aina ya wateja waliokopeshwa wakashindwa kulipia hiyo mikopo.

Kuna kina dalili utitiri wa mabenki na bishara, zisizofuata misingi yake, nyingi zitafungwa. Matokeo yake ni uchumi kukua kiendelevu (sustainabale economic growth).
 
Kiongozi tusiwaumu mabenki kabisaaaa kabisaaa shida siasa imeingia katika mabenki kwa kusema wapunguze vigezo na masharti ya mikopo na imepelekea hata wasio stahili kukopeshwa, na kingine sera zinabadilika kila mwaka na ukumbuke unaposikia guarentee hasa za serikali ni kilio kwa mabenki.

Serikali ni mdaiwa mkubwa na halipi
 
The Citezen la leo lina habari kuhusu hali mbaya ya mabenki kutokana na bad loans.
On top of that, taarifa za ndani za NMB zinasema wana zoezi la kupitia na kulinganisha majina ya orodha ya serikali ya wenye vyeti feki against orodha ya wakopaji wao, ambao wengi ni watumishi wa umma, ili kuangalia ni namna gani wata deal na wakopaji ambao wametumbuliwa na serikali kwa vyeti feki. In fact kuna shida mahali.
 
Kiongozi tusiwaumu mabenki kabisaaaa kabisaaa shida siasa imeingia katika mabenki kwa kusema wapunguze vigezo na masharti ya mikopo na imepelekea hata wasio stahili kukopeshwa, na kingine sera zinabadilika kila mwaka na ukumbuke unaposikia guarentee hasa za serikali ni kilio kwa mabenki.

Serikali ni mdaiwa mkubwa na halipi

Nitaomba kutokubaliana na wewe kuwalaumu watendaji wa benki mpaka pale utakapotoa mchanganuo wa hizo 'NPL' km ni nani na umri wa hizo 'NPLs'.

Pia ungechunguza hizo benki zimeanzishwa kwa mitaji gani na vyanzo vyake kuona kama zimekuwa zikifanya biashara endelevu.

Hoja kwamba Serikali ni mdaiwa mkubwa na halipi haina uzito sana, ila unazua maswali kadhaa, moja ni mazingira gani na kwa jinsi ipi mabenki yameikopesha Serikali wakati, kwa muda mrefu, ndiyo imekuwa ikiyapa uhai mabenki kwa kutunza fedha zake huko. Baada ya Serikali iliyopo madarakani kuamuru fedha zake zitunzwe BOT, hicho unachosema kinaanza kutokea.
 
Non performing loans nyingi ni matokeo ya rushwa...

unatoa mikopo kwenye projects ambazo hazilipi kabisa... mradi tu unapewa rushwa
 
Non performing loans (NPL) ni makosa ya mabenki yenyewe, Bank nyingi zilikuwa zinajilipua kwa kukopesha ovyo, Kulikuwa na poor analysis ya kutoa mikopo, Mtu akijiita mapedeshee kwenye kumbi za starehe na kugawa buku buku Ujue kesho atapewa mkopo ,Haya makosa ya ushindani Ndio yamezaa Haya yote, Ushindani wa kutaka kuwa na wateja na mikopo mingi,
 
Pale unapodhani unawakomoa wananchi kumbe madhara yake ni mapana,pia tuambiwe TRA watapoteza kodi kiasi gani,hii nadhani waandishi wachimbe wajue mwaka jana mabenki haya yalilipa kodi kiasi gani na taifa litapata hasara kiasi gani kwa kukosa kodi
 
Kila upande unahusika na hali hili. Hakuna aliye salama. Management na serikali kisha wakipeshwaji.

Hali ya uchumi imebadilika. Sera za uchumi kwa sasa hivi hazieleweki. Benki zilihitaji kuwakopesha wafanyabiashara ili wafanye biashara. Bahati mbaya serikali inafanya biashara na taasisi zake. Wale waliokopeshwa, wengine ni wafanyabiashara, wanaidai serikali. Hizo taasisi za serikali, ukiangalia mtaji wake hasa, inawezekana ni namba tu na serikali haikupeleka pesa na imekopa pia.

Kwenye management, hawaangalii wanakopesha kiasi gani. Watu wanadanganya mno kwenye mikopo yao. Leo hii loan recovery ni kama haiwezekana. Pia thamani ya assets imeporoka na soko hakuna.
 
Magufuli aanze kutumia sheria kuwafunga CEOs wa haya mabenki yenye madeni yasiyolipika kwa wingi. Mengi yanatoa mikopo kwa misukumo ya rushwa kwa maafisa mikopo bila kufanya assessment na analysis za kutosha za wateja. TWB na TIB ni hela za kodi zetu wafungwe hao
Umenena vema, afisa mikopo akifanya assesment vizuri na akafuata taratibu zote za utoaji mkopo hii mikopo isiyolipika itakuwa michache sana.
Rushwa na 10% ndizo zinazowaharibu maafisa mikopo
 
On top of that, taarifa za ndani za NMB zinasema wana zoezi la kupitia na kulinganisha majina ya orodha ya serikali ya wenye vyeti feki against orodha ya wakopaji wao, ambao wengi ni watumishi wa umma, ili kuangalia ni namna gani wata deal na wakopaji ambao wametumbuliwa na serikali kwa vyeti feki. In fact kuna shida mahali.
On top of that, taarifa za ndani za NMB zinasema wana zoezi la kupitia na kulinganisha majina ya orodha ya serikali ya wenye vyeti feki against orodha ya wakopaji wao, ambao wengi ni watumishi wa umma, ili kuangalia ni namna gani wata deal na wakopaji ambao wametumbuliwa na serikali kwa vyeti feki. In fact kuna shida mahali.
On top of that, taarifa za ndani za NMB zinasema wana zoezi la kupitia na kulinganisha majina ya orodha ya serikali ya wenye vyeti feki against orodha ya wakopaji wao, ambao wengi ni watumishi wa umma, ili kuangalia ni namna gani wata deal na wakopaji ambao wametumbuliwa na serikali kwa vyeti feki. In fact kuna shida mahali.
Hakuna namna,wakakamate chochote walicho nacho,ili angalau warudishe kiasi,hata kama sio chote.
 
Ila kwa Efatha huenda vigezo vya kukopesheka vilikuwa vya ki-uumini zaidi badala ya viability ya project zenyewe!
 
Possible. Ila kimsingi masharti ya ukopaji nadhani yako regulated na benki kuu
 
Umenena vema, afisa mikopo akifanya assesment vizuri na akafuata taratibu zote za utoaji mkopo hii mikopo isiyolipika itakuwa michache sana.
Rushwa na 10% ndizo zinazowaharibu maafisa mikopo
Tujiulize linawezekana? Kwasababu wengi tunapenda kufanikiwa kwa njia ya mkato,kuwa na maisha mazuri ya haraka,kumiliki mabinti mazuri,kukaa vitu virefu etc
 
Magufuli aanze kutumia sheria kuwafunga CEOs wa haya mabenki yenye madeni yasiyolipika kwa wingi. Mengi yanatoa mikopo kwa misukumo ya rushwa kwa maafisa mikopo bila kufanya assessment na analysis za kutosha za wateja. TWB na TIB ni hela za kodi zetu wafungwe hao
very true..kuna maafisa wanapiga hela balaaa
 
Back
Top Bottom