Nashukuru kwa huu uzi kuanzishwa juu ya hii Taasisi:
Nilijiunga nao mwei wa 10,2014. Na nikatakiwa kuweka akiba na nikafanya hivyo.
Baada ya kuijua vizuri hii taasisi nikaomba kujitoa, na utaratibu wa kujitoa ni kutoa taarifa ndani ya siku 90.Hii itafanywa ulipwe kiasi cha fedha ulizoweka kama akiba.
Nilitoa taarifa mwezi wa tatu,2015. Mpaka sasa ninavyo andika ile akiba sijarudishiwa ikiwa ni zaidi ya miezi nane!!!(swali ni wangapi wamefanyiwa hivyo?)
Sababu za kujitoa:
Sio rahisi kupata hiyo mikopo kama inavyotangazwa.
Hatua nilizochukua:
Mbali ya kufika ofisini kwao mara kwa mara, kinacho fanyika ni kupewa ahadi tu.Walitoa tangazo kwamba "tulioomba kujiondoa malipo yetu yatafanyika mwezi wa tisa baada ya madeni kukusanywa na Linyama Auction Mart.
Tulisubiri mpaka huo mwezi wa tisa,laiki hakuna malipo yaliyofanyika, ukirudi tena pale ofisini wafanyakazi wanakuambia watu wa kukusaidi ni hawa"majina yamebadikwa ktk ubao wa matangazo". ukiwasiliana na wahusika, kwanza nao hawana taarifa na wanasema wao sio watu wa msaada.
Lengo:
Sina lengo la kuishafua hiyo Taasisi, lengo langu ni kutoa onyo kwa wajasiliamali na wafanyabiashara kuwa makini na hizi taasisi.Ni kweli ziko kwa kusajiriwa na sheria za nchi lakini huduma zake ni za kitapeli.Ni kweli tuna uhaba wa mitaji, lakini uhaba huu usitufanye kuangukia mikononi mwa watu kama hawa.
Je wewe AFISA MIKOPO unasemaje ktk hili? au nawe uliisha ikimbia ajira PALE?