CARDLESS
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 7,869
- 16,014
Tanga iko mbali sana na Dar sema mnataka iweka karibu.. Moro inafaa kuwekwa state ya Dar... Factor muhimu ni umbali kutoka mkoa na mkoa..
Sent using Jamii Forums mobile app
Tanga iko mbali sana na Dar sema mnataka iweka karibu.. Moro inafaa kuwekwa state ya Dar... Factor muhimu ni umbali kutoka mkoa na mkoa..
Majimbo yaundwe kulingana na maeneo yake Geographically, ukaribu na mambo mengine kama tamaduni etc... Mfano jimbo la pwani iwe Dar, Tanga, Pwani... Jimbo la kati Dodoma, Singida, Tabora.... Jimbo la kanda ya ziwa Mwanza, Kagera, Mara etc..Wazo ni zuri, ila linahitaji utulivu kiakili na kulitafakari kwa kina bila kuweka ushabiki wa kisiasa. Kimsingi states za namna unayopendekeza zilikuwepo hata kabla ya ukoloni na ndiyo hizo zilizotumika kufanikisha utawala wakati wa ukoloni wa kijeremani na baadaye waingereza. Zilikuja kuzuiwa kutumika katika utawala wa maeneo husika baada ya mwalimu nyerere kuondoa ukabila na kuunda Taifa la Tanganyika.
Kiutawala Tanzania ni kubwa mno kuweza kuitawala kutoka Dodoma, pamoja na kufanikiwa kwa kiasi fulani baadhi ya mikoa imepiga hatua kubwa kimaendeleo wakati mingine hasa magharibi ya Tanzania imebakia kuwa nyuma licha ya rasilimali za asili ambazo kwa mfumo wa sasa, mgawanyo wowote wa rasilimali za nchi hufanyika Dodoma.
Ushauri wako ni mzuri kwani kila Jimbo au state ingekuwa na mamlaka ya kujiendesha yenyewe na baadhi ya mambo makubwa ya kitaifa yakaamuliwa Dodoma kwa kuwatumia wawakilishi. Mimi ningependekeza kuunda majimbo kumi: Jimbo la kati, Jimbo la kaskazini, Jimbo la ziwa, Jimbo la magharibi, Jimbo la nyanda za juu kusini, Jimbo la kusini, Jimbo mashariki, Jimbo la pwani mashariki Jimbo la Zanzibar na majimbo yanayogusa miji mikubwa hasa Dar es salaam Mwanza na Dodoma.
Ukimsikia mtu anapinga hili ni kwa maslahi binafsi tuu hakuna kingine... Halafu kama vipi si ipigwe kura ya maoni watanzania waamue wenyewe??Federal state inafaa lakini wapo watu jambo hili hawalitaki kwa kisingizio cha ku promote ukabila nakupunguza himaya ya ku maintain status quo hawataki mabadiliko ya mfumo wa kiuongozi usije ukavuruga Vanguard Party .Mbona Kenya wamefanikiwa kutawala kupitia majimbo wanaunganishwa na central Govt
Sorry nilisahau Morogoro...Tanga iko mbali sana na Dar sema mnataka iweka karibu.. Moro inafaa kuwekwa state ya Dar... Factor muhimu ni umbali kutoka mkoa na mkoa..
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi huna taarifa kuwa Rwanda na Burundi ni mataifa yenye mamlaka kamili na yana viti kwenye umoja wa mataifa?.. Kwa upande mwingine Kigoma ni mkoa uliokuwa katika mamlaka ya Tanganyika na baadaye Tanzania!!!, Nadhani unapaswa kulijua hili.🙄Kigoma, Rwanda na Burundi iwe moja!!
Hii noma Sana.shinyanga, kagera, geita, mara, simiyu na MWANZA ziwe state moja a.k.a empire.
Watakuja wale wanaojiita wazalendo na kusema unataka kuigawa nchi kwa misingi ya ukabila na ukanda sawasawa na alivyoambiwa Lowasa.Wanajamii,
Nimekaa na kufikiria kuwa, kuna haja ya Tanzania yetu kubadilisha sheria na katiba ili kutoa nafasi na ufanisi zaidi katika ngazi zote za utawala na sheria.
Mikoa yetu yote iwe sovereign states ziwe na sheria zao na serikali zao. Nathani itasaidia sana kufanya mikoa ijitegemee na kuwezesha ufanisi zaidi.
Nchi yetu ni kubwa mno. Tunahitaji kujipanga upya katika utawala bora, sheria na pia kupunguza ukubwa wa serikali.
Nawakilisha hoja.
Juice toka tanga kwa matunda ya msimu mkuu? Upo sahihi lakini nadhani huko tanga tunahitaji kufanya mageuzi makubwa ya kilimo. Badala ya kuachia maji matamu ya mto pangani yaingie baharini, tungefikiria kuyatumia maji yale kwenye kilimo cha umwagiliaji. Maji mengi sana yanapotelea baharini, yak8shaingia kwenye bahari yanakuwa salty.Kwa mfano Tanga. Binafsi hakuna sehemu Tanzania nzuri na yenye nafasi kubwa sana kiuchumi kama Tanga.
Tanga kuna ardhi nzuri,bahari lakni corridor ta kaskazini kupitia Tanga ni shida. Mwenyezi Mungu ametupa miundo mbinu yote lakni hakuna mtu anafikiria.
Mfano Mtwara kule kuna bandari ambayo inaweza kusaidia uchumi wa southern corridor.
Kwa kumalizia, Tanga kuna machungwa matamu sana na matunda mengi, lakni bado tunahangaika kuagiza matunda SA. Hakuna mtu anatengeneza hata juice za machungwa kutoka Tanga.
Je waafric tunalaana au tumeridhika na hali zetu?
Wazo zuri lkn kwangu mm kidogo wasifanye mikoa yote badala yake state ziwe hata 12 tu.. kwa maana mikoa iunganishwe katika state moja.. mfano.. Tanga, Manyara, Arusha na Kilimanjaro iwe state moja.. Morogoro pwani na Dar iwe state moja..
Iringa, Njombe Na mbeya iwe state moja nk nk...
Sent using Jamii Forums mobile app