Mike Tyson was overrated

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
16,455
30,876
Mike Tyson hakuwa bondia bora. Alikuwa overrated. Management ya Mike Tyson walikuwa wanamkutanisha na mabondia dhaifu . Kabla ya kumkutanisha na bondia yoyote, management ya Mike Tyson ikiongozwa na Promoter wake Don King, chini ya jopo la wataalamu walio bobea katika mchezo wa boxing, walihakikisha kwanza wanajiridhisha pasi na shaka yoyote ile kwamba Mike Tyson atampiga bondia watakae mkutanisha nae. Ndio maana kwa kipindi kirefu sana management ya Mike Tyson ilikuwa inafanya kila namna, kuhakikisha bondia wao, hakutani na mabondia wakali kama Evander Holyfield, Lennox Lewis etc.

Unaweza kuona Mike alianza kupewa vipigo mfululizo tangu atemane na uongozi wake. Ukimuita Mike Tyson bingwa " Joe Frazier" George Foreman utawaita nani ? Jaribu kutafuta cd za mapambano ya watu kama George Foreman, Joe Frazier & Muhammad Ali, uone mabondia wa ukweli.

R.I.P Muhammad Ali
 
Boxing ina peak time kwa kila bondia, baada ya hapo unakuwa mdebwedo, hata Muhammad Ali past his prime alionekana wazi kuwa chini ya kiwango, mabondia wajanja kama kina Lewis na Mayweather walipong'amua kuwa their time was over wakaamua kustaafu.

Kweli mkuu, ila mpaka leo najiuliza. Muhammad Ali aliweza vipi kumpiga George Foreman?
 
Mkuu nahisi unamapenzi binafsi huyu mike 'iron' Tyson awe overrated kweli???

Kumbuka Tyson ndiyo ingawa pekee akiwa mdogo miaka 21 (kama niko sahihi kwa umri)akimpiga Trevor ambayo ndiye mtu wa mwisho kumpiga Muhammad Ali .... Tyson huyu huyu ndiyo mtu pekee ambaye anarekodi ya kushikilia mikanda mitatu ya juu kwa wakati mmoja akiwa mdogo...
 
Hiiivi labda mi cjui ila mleta maada;wale mabondia huwa wanamchalenge bondia au mkanda alionao bondia; maana inafikia wakati ili uwe bingwa wa level flani ni lazima ukamchalenge anaeushika, na huitaji kufikiri ana nguvu kias gAni ila wewe una nguvu kiasi gAni mpaka ukawazia mkanda wa huyo jamaa;
So tyson was the best 7bu tu aliwanyang'anya watu mikanda na sio ujasusi katika ndondi kama anavomaanisha mleta maada
 
Back
Top Bottom