Mikataba ya madini: Ni bora iletwe hapa JamiiForums tuijadili tutaisadia serikali kuliko bungeni

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Baada ya kazi nzuri iliyofanywa na time ya Prof Mruma, limeonekana hitaji la mikataba ya madini kuwekwa wazi ili wananchi waione na kuijadili.

Njia iliyopendekezwa na wengi ni mikataba hiyo kupelekwa bungeni ili wawakilishi wetu wakatusaidie kuipitia na kuishauri serikali accordingly.

Binafsi napendekeza kama itaipendeza mamlaka ya juu basi mikataba hiyo ingeletwa hapa If ili wananchi wenyewe Vila kujali itikadi zetu tuweze kuijadili na kuishauri serikali ambayo sisi wenyewe ndio tumeiweka madarakani.

Siyo kwamba siliamini binge, lahasha Bali kwa swala hiki binge linaweza kuwa bias kwani uwakilishi wake ni wa vyama vitano tu lakini madini ni ya wananchi wore kama alivyo Raid na serikali take.

Pili, If ni jukwaa linaloaminika na linaloweza kuikutanisha mihimili yote ya dola na kwahiyo tutapata mjadala mpana na wenyewe tija kwa taiga. Mdau mwenzangu wa If una maoni gani juu ya hoja yangu? Karibu tuzungumze!
 
naunga mkono hoja. wabunge wengi wako bungeni kwa vile walikuwa na hela za kuhonga wajati wa uchaguzi na sio uwezo wakujenga hoja. wengine wako mule kwa sababu ya kubebwa na wakubwa hasa wa vitu maalumu.
 
Yaani uliyekuja na wazo hili ni great thinker. Kule bungeni wako biased mno kivyama kuanzia na spika mwenyewe ndo kabisaaa! Hapa hoja inachambuliwa kwa kina na jf iko mbali Mara mia kuliko hilo bunge la akina mkuchika
 
Mleta mada ana nia njema kabisa lakini umekosea sana tena sana kuleta wazo lako hapa... Nani kakwambia CCM wana akili hizo? Hawawezi kubali hata kama kwa greda. Kwanza Magufuli akiona hii post yako atatamani kuifutilia mbali kabisaJF...
 
Naunga mkono,kama kuna chombo kinachitia hii nchi hasara ni kitu kinaitwa bunge umaskini wa watanzania umesababishwa na bunge mikataba yote mibovu imepitishwa na bunge, inaonekana wazi kabisa serkali ndo inasimamia bunge na sio bunge kuisimamia serkal, sasa serkali istarajie mawazo yenye maslhahi kwa wananch kutoka bungeni,ni bora mijadara ikaja humu jf humu kuna watu wenye nia njema.ambao hawana maslahi na vyama na matumbo yao.
 
Hapa pana madini, kule kuna watu ambao wanapenda waonekane kwenye TVs tu...yaani wazungumzwe wao....
 
Kama DOM wanakwenda kupiga porojo mara zote jf. ila kwa matusi na kununuliwa kwa wana jf. itakuwa kama wakati wa uchaguzi au wakati wa "uvamizi wa cl.." Kwa mitazamo hiyo ni bora isije humu kabisa ila iundwe tume kama ya mruma ilindwe kama wasahihishaji wa mitihani ya necta. kisha walete majibu. Sina imani na bunge asijerokea Karamage wa TICTS akaenda kusahinia mikataba London. aibu dume zima unawaangukia wanaume wenzio ili wakuibie.
 
Kule vigezo vyenyewe KKK unafikiri mkataba utajadiliwa ipasavyo? Wakati mwingine tunawalaumu bure tu kwamba wanapiga meza na kushangilia, sasa watajadili vipi wakati uwezo na upeo wao hauwezi kuchambua yaliyopo kwenye mkataba?

Ila wanaweza kuwa kikundi maridadi sana cha kuburudisha taarabu na vichekesho.
 
Yule mzee anayetamani mitandao ya kijamii ifutwe na malaika atakubali, labda aache kuangalia mitandao ya kijamii maana humu JF tutafukunyua kila kitu
 
Back
Top Bottom