kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,010
Napenda kama kuna yeyote ataweza kunikumbusha hiki kitu kinachoitwa mkataba wa EPA ni nini,na madhara ya kutojiunga nao ni yapi?Maana naona nchi hii tumeumia sana na bidhaa feki za mchina.Binafsi hasara niliyopata kutokana na kununua vitu feki vya China tena kwa bei kubwa sana,ni mamilioni ya pesa.Natamani sana ni bora tungeuziwa bidhaa hata kama ni used kutoka Ulaya.Naamini hawa wazungu ni wezi lakini si kwa kiwango cha wachina.Wachina hawana hata utu