Mikataba Inayohusu Mali Kabla ya Ndoa aka Prenups

Mikataba Inayohusu Mali Kabla ya Ndoa aka Prenups

mjasiria

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Posts
4,155
Reaction score
1,870
Hapa nadhani sijawahi kuposti mada yeyote, hii itakuwa ya kwanza. Leo katika stori mbili tatu na jamaa zangu wa karibu, mara paap tukagusia pesa, hatujakaa sawa Jeff Bezos huyu hapa. Kama huna hela kama mimi ila ni mfuatiliaji mzuri wa habari za watu wenye pesa za maana utakuwa unajua kwamba huyu jamaa ni tajiri namba moja kwa sasa duniani kwa mujibu wa Forbes, nina imani kuna wasukuma kule Chato wamechimbia chini pesa ila hawajulikani tu 😛. Tuyaache hayo, huyu jamaa yuko kwenye mchakato kwa kuachana na mkewe - mjadala ulikuwa ni kiasi gani mwanamke atapewa?

Njaa mbaya sana, yaani badala ya kujadili namna ya kutafuta pesa tukajikuta tumeifanya hiyo ni mada kuu. Kila mtu kasema lake hapo, ikafika mahali tukafika kwenye "prenup" (kiswahili chake sijui, kwa asiyejua maana yake ni mkataba wanasaini wanandoa kuhusu hatima ya mali zao pale watakapoachana kabla ya kufunga ndoa. Kwa mfano kama mtu ana pesa ndefu kama Bezos kabla ya ndoa wanaweza kuwa na mkataba unaosema ikitokea akaachana na mkewe atawajibika kumlipa kiasi kadhaa.

Mjadala ukawa mkali kwenye "prenup". Kuna wanaosema suala la kusaini hiyo kitu inamaanisha hakuna mapenzi ya kweli hapo na kuna wengine wanasema haina uhusiano na mapenzi. Nimeona niulete huu mjadala hapa kwa magwiji wa mapenzi.

Wakuu ninyi mnaonaje kuhusu "prenup". Je kuwepo kwake ni ishara ya kutokuwa na mapenzi ya kweli kati ya wawili wapendanao, tena wanandoa? Au ni kitu kisicho na uzito wowote katika mizani ya mapenzi? Kwa mfano wewe unayesoma hapa kama unafunga ndoa na mtu anayekuzidi pesa akisisitiza kuwe na huo mkataba, je itakufanya ujisikie hupendwi ipasavyo? Utakubali?

Itapendeza zaidi majibu yawe na sababu.
 
Nani sasa atakubali kusaini huo mkataba na ndoa hiyo? kwa sisi wanawake wa kibongo?

Kuna theory 2 tu kwa wanawake wa kibongo "Chako ni changu, changu ni changu" au "chako ni changu, changu ni chako"

Kuna theory nyingi za ndoa kuna ile ya mut'aa kibongo bongo ushawahi kuona inakuwa practised?

Hayo mengine tuwaachie wazungu na waarabu.
 
Hahaha kwa hiyo wewe hukubali kabisa? Sasa kwa mfano bakhresa anakuoa halafu anakupa mkataba wa kukulipa M100 akikututema utagoma?
 
Iyoo nilisikia pia kwa jamaa mmoja wa jarida la utupu marekani alifariki mwaka jana waliekeana mkataba uwo na mwanamke wake aliyekuwa na miaka28 yeye akiwa na miaka90+.

Binafsi mm naona ni mkataba mzuri maana unakuta mwanaume au mwanamke ni mtu mzima wanaachana au mwenza wake kafariki na tayari ana watoto ili kulinda Mali zake kwa watoto na yeye mwenyewe ni lazma azilinde zile alizonazo kwa manufaa ya wanae na yeye mwenyewe maana talaka kiukweli zinarudisha watu nyuma sana na nichanzo cha wengi kufilisika.

Bora uonekane huna mapenzi kuliko kuja kuumia sababu ya talaka sababu kiukweli na usiopingika wanawake au wanaume wadogo wengi wanaingia mapenzini na wazee au watu waliowazidi miaka mingi sababu ya tamaa ya fedha sasa usipokuwa makini ndugu utakwisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
swala la jeff bezzo ni tofauti mkuu...10 Things I Learned Reading Brad Stone's The Everything Store ukisoma hiki kitabu ambocho mtu akihitaji softcopy ninacho kuhusu historia ya amazon..Jeff bezo na mke wake walianza wakiwa hawana kitu hadi kufikia hapo walipo...so ni tofauti na ile ya kuoa kimada wakati ushazeeka ndo maana unaona hata yeye mwenyewe bezzo hajamind halafu ukifuatilia kwa ukaribu zaidi yeye ndo aliyeanzisha mahusiano na msichana wa pembeni
 
Hoja ni prenup, hiyo habari ya Bezos ni backstory tu. Jadili prenup.
 
Mada nzuri ila sio realistic kwa wengi wetu mana wengi wetu ni masikini hatuna vipato vya kuweka uwe mkataba wa prenup

Ila tahadhari ni bora kuliko kinga nadhani kusaini uwo mkataba itategemea na mtazamo wako juu ya mkataba husika
 
Mikataba ya namna hii wanafanya wahuni tu,bila kujali utajiri walionao.Ukiona watu wanaachana ni sawa na ajali kutokea,ndio maana mahakama zipo.
 
Mada ingependa kusikia mtazamo wako
 
Mikataba ya namna hii wanafanya wahuni tu,bila kujali utajiri walionao.Ukiona watu wanaachana ni sawa na ajali kutokea,ndio maana mahakama zipo.
Hahaha mkuu mbona maneno makali sana. Kwa hiyo wewe unaona sawa mtu anaoa na mamilioni halafu mkewe aje achukue nusu ya mali baada ya miaka tuseme mitano?
 
Hahaha mkuu mbona maneno makali sana. Kwa hiyo wewe unaona sawa mtu anaoa na mamilioni halafu mkewe aje achukue nusu ya mali baada ya miaka tuseme mitano?
Kutafuta mke/mume ni mchakato mrefu,si kama wa kwenye mitandao wanavyotafutana,wengi wanasukumwa na tamaa ya mwili tu,kwa staili hiyo lazima mtu aangukie pua tu,na kufikiri suluhisho ni kuvunja mkataba bila kuangalia muda waliopotezeana.
 
Kwahiyo unakubaliana na suala la mikataba ikiwa mke atatafutwa kidigitali zaidi?
 
Mikataba ya namna hii wanafanya wahuni tu,bila kujali utajiri walionao.Ukiona watu wanaachana ni sawa na ajali kutokea,ndio maana mahakama zipo.
Kwani unadhani chanzo cha kufunga ndoa kanisani au msikitini au bomani ni nin ? kama si uhuni uliokuwa unatenda kabla ya aliyebuni hiyo njia.
 
Kibongo bongo mwanamke/ mwanaume akitaka kuwa tapeli kwa kutumia mapenzi anaweza akatajirika haraka sana kupitia ndoa, baadae talaka kama hakukuwa na pre nuptial agreement.

Pre nuptial ni muhimu kwa mtu yeyote sema kwa sisi watafutaji ni muhimu zaidi.

Watu wengi wanaipuuzia kwa sababu hawaielewi vizuri.
 
Ngumu sana hii.
Kwanini mkuu? Kuna ugumu gani kukubaliana kuhusu mgawanyo wa mali kabla ya ndoa ili likitokea la kutokea kunakuwa hakuna sintofahamu yeyote? Huoni kwamba huu utaratibu unasaidiaje kuondoa migogoro isiyo ya lazima kwenye suala la mali?
 
Back
Top Bottom