MIKASA YA MAISHA (TRUE STORY)

Foxhound

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
28,057
74,465
Habari waungwana, leo nimeamua kushare nanyi mikasa ya kimaisha ambayo ilinikuta kipindi nipo nyumba ya kupanga.

Ilikuwa hivi:
Mwaka 2006 nilifanya vizuri katika masomo yangu ya Electronics nikawa nafanya kazi kitaa hadi kufikia mwaka 2013 nikataka kujiendeleza (Chuo) ili nifike mbali zaidi, bila kutegemea nikajikuta nimepatwa na ugonjwa ambao ulinifanya nishindwe kuendelea na masomo yangu. Hivyo nikaanza kuhangaika na tiba bila mafanikio hadi kufika hospitali moja (jina nalihifadhi) ambapo nilikutana na daktari mmoja bingwa wa magonjwa hayo. Aliniandikia vipimo na kuvifanya katika hospitali hiyo lakini majibu yalipotoka yule daktari aliniandikia niende Regency kwa vipimo zaidi. Nilifika Regency na kufanya vipimo, nakumbuka Dkt Naveen wa Regency baada ya vipimo aliniambia kuwa hajaona tatizo lolote, hivyo nirudi na vipimo hospitali niliyotoka. Nilipomrudishia majibu daktari hospitali niliyotoka aliniandikia dawa za kutumia mwezi mmoja na kunitaka nirudi tena kwake baada ya kumaliza dawa kwa uchunguzi zaidi. Nilitumia dawa zile na baada ya mwezi nilirudi kwake nikiwa nimepata nafuu, hivyo aliniandikia niendelee kutumia dawa zile kwa mwezi zaidi. Nashukuru baada ya hapo nilipona na kuwa mzima kabisa.

Mwanzoni mwa mwaka 2014 nilitaka kufunga ndoa lakini kabla sijaweka wazi mipango yangu nilikumbwa na balaa jingine (mara hii mguu wa kushoto nilipatwa na uvimbe na mashine ikawa haisimami barabara) Dah! Nilikuwa nashindwa hadi kutembea, nashukuru kuna rafiki yangu mmoja alijitolea ndie akawa ananisaidia kwenye kuhangaika kutafuta tiba, kipindi hicho nilikuwa nimepanga nyumba Temeke (kabla ya hapo nilikuwa nimepanga Mtoni kwa Azizi Ali), nilifahamishwa Zahanati ya Wakorea hivyo nilifika huko na kupata tiba ya mguu (huku nikitumia kongoro, bamia na dagaa kwa wingi) pia nikiendelea kutumia dawa za Kisunna kwa ajili ya mashine. Baada ya kufunga ndoa nakumbuka mguu nilikuwa nachechemea na mashine ikawa imepona hivyo nikataka kuhakikisha kuwa imepona kweli au kwa muda tu!! Nikajikuta haraka haraka nimetembea na wanawake kama 150 ndani ya muda mfupi tu! Hivyo baada ya hapo niliamini kuwa kweli mashine imepona na mwishoni mwa mwaka huo mguu ukawa umepona kabisa.

Mwaka 2016 nilifanikiwa kupata hela nyingi kiasi kutokana kujichanga na vibiashara vya hapa na pale pamoja na mihangaiko yangu hivyo nikaamua nitafute kiwanja nianze ujenzi ili niweze kujikwamua kwenye mikono ya wenye nyumba. Nilifanikiwa kupata kiwanja lakini nikiwa katika mipango ya kuanza ujenzi nakumbuka siku moja jioni wakati narudi nyumbani, nilikutana na mama mwenye nyumba, baada ya salamu aliniuliza kiutani tu "Nasikia umenunua kiwanja? Hongera" Nilimjibu ndio lakini nilijiuliza sana hizo habari amezipata wapi! Kwani mipango yangu yote nilikuwa nafanya kimya kimya na kwa siri sana! Moyoni nilijiuliza sana lakini niliamini labda pengine niliwahi kuongea na simu akanisikia au pengine wapangaji wenzangu walinisikia na wakamsimulia (maana umbea ni jambo la kawaida kwenye nyumba za kupanga). Hivyo sikutilia maanani juu ya hilo nikaendelea na mipango yangu kama kawaida.

Nakumbuka 2016 hiyo hiyo kufika mwezi Julai mke wangu aliondoka na kwenda nyumbani, kipindi mke wangu hayupo nikajikuta kila siku usiku nikilala naota ndoto za ajabu ajabu na nikiamka asubuhi nikawa nakuta ushahidi wa nilichokifanya ndotoni, (Nilikuwa naota mama mwenye nyumba anakuja chumbani kwangu na nashiriki naye tendo la ndoa) nilikuwa najiuliza sana inakuwaje niote kitu halafu niwe nimekifanya kweli, niliamini labda ni ndoto zinazosababishwa na uchovu au kwa vile mke wangu hayupo. Hali hiyo ilijirudia mara kwa mara hadi ikafika kipindi asubuhi nikawa namtazama sana usoni mama mwenye nyumba lakini yeye anashindwa kunitazama usoni! Hali hiyo ilinifanya nihisi kitu lakini nikajipa moyo nisiwe na dhana mbaya juu yake.

Nakumbuka siku moja wakati nimerudi kwenye mishe zangu kuingia ndani tu nikahisi maumivu ya mguu, tena mara hii ukiwa ni mguu wa kulia, mwanzoni nilidhani labda maumivu tu ya kawaida lakini siku ya pili nilishindwa kutoka nje kwenda na mihangaiko yangu. Hivyo nilihangaika kutafuta tiba kuna hospitali nilifika lakini daktari kumuelezea tatizo langu akaniambia nipige X ray, majibu kutoka yule daktari akaniambia hakuna tatizo lolote hivyo nitafute tiba kwa njia nyingine. Nilishindwa kumwelewa yule daktari, baada ya kuongea naye kwa muda mrefu hatimaye mwishoni alinambia kuna kitu ameona kwenye mguu wangu ambacho sio kawaida (Kiukweli alinitisha sana) na nilimwomba sana afunguke, ndipo akaniambia mguuni kwangu kuna Sihri (Wataalam wa mambo ya kiswahili hapa wameelewa) hivyo inahitaji kutolewa. Duh! Mwanzoni nilishindwa kumwelewa na nilimhisi vibaya lakini baada ya kuongea naye kwa kina (Aliniambia kuwa case kama hizo ameshakutana nazo nyingi ambazo sio za hospitali) mwishowe nilimkubalia na kuanza kuhangaikia tiba. Nilipata tiba lakini niliyokutana nayo yanatisha. Niligundua yafuatayo kumhusu mwenye nyumba:-
1. Ndoto nilizokuwa naota sio ndoto bali ni kweli, alikuwa na mambo ya kishirikina.

2. Usiku alikuwa anakuja chumbani kwangu na nilikuwa nashiriki naye tendo la ndoa na mbegu alikuwa anaondoka nazo.

2. Hakupendezwa na mimi kununua kiwanja na kuanza ujenzi.

Nilijaribu kuulizia ulizia lakini nilifanikiwa kupata habari pia kuwa nyumba yake ukiingia ni ngumu sana kuhama na hata hivyo pia kuna wapangaji ambao waliwahi kupanga nyumba hiyo na kuhama ndani ya muda mfupi.
Hivyo baada ya kupata tiba na kupona, nilimsubiri mke wangu aliporejea niliamua kuhama, tangu nilipohama hadi sasa sijakumbwa na tatizo lolote kati ya hayo, maisha yanaendelea vizuri tu namshukuru Mungu.

Huu mkasa ni kweli tupu kuhusu maisha yangu, na baadhi ya vitu nimeamua kutokuweka hapa ili kupunguza urefu wa stori kwani naelewa kuna baadhi wasiopenda kusoma mada ndefu.

By: Emiir (Ali Bakari, Beberu mwitu, Careem, Don juan)

Kama umeshawahi kukumbana na mkasa/mikasa kama hii unaweza kushare nasi na jinsi ulivyoweza kujikwamua.

Ahsante
 
Ulizembea sana mkuu ......mtu kama huyo una piga .....06...
Yataka moyo, maana nilipoambiwa kuwa ananifanyia hivyo, mwanzo nilitaka nimfate nimwambie kama vipi si aje live...kuliko kunifata usiku. Nikaambiwa wala nisijaribu kumwambia hivyo bali niachane nae.
 
Mkuu Mshana Jr tafadhali naomba pitia hapa utie neno... maana hii habari ilinipa ukakasi sana.
 
Back
Top Bottom