Mikakati ya CHADEMA, Iringa kuwa jiji

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,782
239,461
Huu ni mkakati uliowekwa na viongozi wa CHADEMA ambacho ni chama tawala Iringa mjini baada ya kunyakuwa viti 14 vya udiwani kati ya 18 , Alex Kimbe Meya wa Manispaa hiyo ametangaza kupandisha pato la ndani kutoka bilioni 2 hadi bilion 7 ili kupata fedha za kuboresha huduma muhimu za jamii .

My take - hakika penye nia pana njia , wakati wengine wameshindwa kwa zaidi ya nusu karne, CHADEMA wanafanya maajabu ndani ya miezi mitatu !
 
It's easier to talk about doing something than actually doing it!

Kama gari ya meya wameshindwa kuiuza wakati walisema wataiuza wakishinda viti vingi vya udiwani, kwa sasa wataweza kukusanya mapato na kuyatumia kama wanavyotaka tuamini tena!
Una haraka sana .
 
Mkuu ahsante kwa taarifa.
Naomba nikunong'oneze kidogo , ila usimwambie mtu , ni hivi mimi mwenyewe binafsi japo si mkazi wa Iringa nimeamua kutafuta soko la viazi ( vile vya chips ) na njegere za kihesa nje ya nchi ili kusaidia wakulima wa iringa , kwenye suala la maendeleo hasa kwenye maeneo tuliyoshinda hatutaki masihara , baada ya muda mfupi sana utaona tofauti kubwa kati ya magamba na chadema , tuombe uzima .
 
Hivi huyu meya kapata lini hicho cheo ? Kwanini usivute subira uone itakuwaje ?
Kikao cha kwanza kilishafanyika na baadhi ya madiwani wa chadema walitaka iyo ahadi itekelezwe lakini baadhi ya madiwani wakiongozwa na mbunge wa Iringa mch msigwa walipinga wakitaka meya wa sasa nae apigwe kiyoyozi kwenye hiyo V8 na mkulugenzi nae amesapoti kuwa watatafuta njia mbadala kwa mantiki hiyo ile ahadi ya kuliuza hilo gari lenye thamani kubwa milioni130 pindi wapatapo uongozi taratibu sisi wananchi tunaona inaota mbawa sasa sijui hizo ahadi ulizotueleza kama zitatimizwa tusubiri na tuone
 
It's easier to talk about doing something than actually doing it!

Kama gari ya meya wameshindwa kuiuza wakati walisema wataiuza wakishinda viti vingi vya udiwani, kwa sasa wataweza kukusanya mapato na kuyatumia kama wanavyotaka tuamini tena!
Mkuu UNAONGOZWA NA ROHO YA CHUKI
HUSDA.
UZANDIKI
 
5.6 Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Jiji

i. Kuwe idadi ya watu wasiopungua laki tano (500,000);

ii. Kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa asilimia tisini na tano (95%) kwamapato yake ya ndani; na

iii. Kuwepo sifa nyingine zaidi ya sifa za kawaida za Manispaa kama vilemaeneo ya kihistoria, maeneo ya utalii; Makao Makuu ya Mkoa; kituo chashughuli za Kimataifa na nyinginezo.
 
Lengo zuri lakini nina mashaka kama itakidhi vigezo hasa cha idadi ya watu.
Usitie shaka mkuu , mji ukishakuwa na mipango mizuri na fursa kedekede wahamiaji wanaongezeka kwa kasi sana .
 
5.6 Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Jiji

i. Kuwe idadi ya watu wasiopungua laki tano (500,000);

ii. Kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa asilimia tisini na tano (95%) kwamapato yake ya ndani; na

iii. Kuwepo sifa nyingine zaidi ya sifa za kawaida za Manispaa kama vilemaeneo ya kihistoria, maeneo ya utalii; Makao Makuu ya Mkoa; kituo chashughuli za Kimataifa na nyinginezo.
Kwa niaba ya familia yangu nakushukuru kwa mchango wako .
 
  • Thanks
Reactions: KXY
Tatizo kamji kadogo sana, inabidi wafanye jitihada za kupima maeneo kuongeza eneo la manispaa.
Mkuu mji wa Iringa sio mdogo swala ni kutimiza hivyo vigezo lakini kwa upande wa eneo manispaa wana eneo la kutosha umeona mkoa wa Mbeya? Kutoka katikati ya mji mpaka mwisho wa jiji si zaidi ya km10
 
chadema iringa timizeni ahadi zenu kwa wana iringa mjini. kumbukeni miaka mitano si mingi mtakuja kuulizwa...
 
Mkuu mji wa Iringa sio mdogo swala ni kutimiza hivyo vigezo lakini kwa upande wa eneo manispaa wana eneo la kutosha umeona mkoa wa Mbeya? Kutoka katikati ya mji mpaka mwisho wa jiji si zaidi ya km10
Inawezekana eneo kubwa halina makazi ya watu kwasababu idadi ya watu haifiki 200,000 kama sijakosea.
Pia sio vijiji vyote vimekuwa urbanised, manispaa bado ina vijiji badala ya kuwa na mitaa tupu
 
Back
Top Bottom