Mijadala gani hufungwa au kufutwa kabisa katika JamiiForums?

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kuupindisha ukweli ndani ya JF na kuanza kuwafanya watumiaji wa JF kudhani kuwa aidha wanaonewa au kuna jambo nyuma ya pazia. Ni wakati muafaka wa kuwafahamisha watumiaji wa JF (wanachama na wasio wanachama) nini hufanywa na moderators na kwa misingi ipi.

Kwanza tuziangalie kanuni/sheria za JF ambazo ndizo hutumika kuwahukumu watumiaji wote (si nje ya hapo!). Mara nyingi tumekuwa tukiwasisitiza wanachama (members) kuwa ni vema wakazisoma sheria hizi kabla ya kuanza kuitumia JF ili hatua flani zinapochukuliwa zisionekane kuwa zimewakandamiza, ni wajibu wetu kama watumiaji wa JF kuanza kuangalia sheria hizi na kupendekeza wapi pafanyike marekebisho na kivipi.

=============

Tafadhali zingatia mambo yafuatayo:

Participants will keep a polite tone and ensure that a sense of respect and tolerance permeates the discussion.
Wadau wengi wamekuwa wakiivunja kanuni hii; haturuhusu kwa namna yoyote iwayo kuvunjiana heshima kwa makusudi wala matusi kwa namna yoyote iwayo.

Mfano: Kuandika neno fvck kwa nia ya kukwepa censorship ni kutukana kwa kudhamiria kabisa, tumelishtukia hili na mara inapobainika hoja husika huondolewa na mhusika kufahamishwa juu ya kosa lake, anapothibitika kuendelea kukaidi basi hufungiwa kwa muda au kufutiwa uanachama kabisa!

Hili nalo pia husababisha hoja za watu kufungwa, kufutwa au mhusika kupewa onyo.

Avoid provocative jokes
Because you are not in a face-to-face environment, it’s easier for someone to take something you say the wrong way.
Nadhani maelezo yaliyo juu yanajieleza wazi, natamani wengi wangeelewa maana ya maneno hayo juu! JF kuna watu wazima na vijana. Mizaha isiyo na staha haifai. Waheshimu wadau wote; vinginevyo hoja yako inaweza kuondolewa na ukawajibishwa.

Kuanzisha mada ambayo unataja chanzo ni jambo jema (tena ikibidi na link ya chanzo). Kutumia screenshots za social media platforms, kutumia vyanzo ambavyo havieleweki; inapelekea hoja kuondolewa hadi ithibitishwe.

Kuna wadau walikuwa na kawaida ya kuwasiliana na wenzao kwa mapenzi yao wenyewe au hata bila wao kuhitaji, namna pekee ya kuwasilisha PM au email ambayo unaona inaleta tatizo kwako si kuibwaga katika hadhara bali kuituma kwetu na sisi tukaifanyia uchunguzi na kubaini ubovu wa PM wenyewe au Email husika ili mhusika achukuliwe hatua za kinidhamu. Tunalichukulia suala la PM na Emails kuwa private, kulileta hadharani ni kutafuta magomvi na kudhalilishana.

Hapo juu panajieleza. Lakini, ukionekana upo humu ajili ya kukera watu, hoja zako zitawekwa kando na akaunti inaweza kufungiwa.

Wengi wamekuwa wakiivunja hii makusudi kabisa; wanaanzisha salaam ndani ya topic na mods huchukua hatua za kuondoa kila post yenye kuwa nje ya hoja au wanapoona topic imejaa majibizano yasiyo na tija kwa jamii basi topic nzima hufungwa au kuondolewa kabisa. Aidha, kuanzisha mjadala wa kidini sehemu ya siasa wakati kuna jukwaa la dini ni kukosea, mods huhamisha mjadala husika kwenda jukwaa husika wakiwa wameacha redirection na ukibonyeza title ya topic husika utajikuta unaendelea kuisoma katika location mpya.

Ieleweke kuwa kila post ambayo inaondolewa kwenye public domain ipo; zinabaki kwa ushahidi siku za usoni maana wengine hukana kuwa walifanya makosa wanayoambiwa walifanya; hatufuti MOJA KWA MOJA, zinawekwa sehemu kwa ajili ya reference za makosa ya wanachama wetu.

Nudity / Porn
Please, remember that this board is a PUBLIC forum. There are 12 year olds here just as there are 60+ year olds. Nudity and porn are prohibited for obvious reasons.
Inajieleza, ukikosea post/hoja yako itafutwa!

Signatures & Avatars
We do not have any specific set of rules regarding signatures. However, we do ask you that it will not be offensive to others. No adult, drug related or racist content please.
Signatures za watu wengine huwa ndefu SANA, au zina maneno yasiyo na heshima kabisa. Huwa tunaziondoa na kumfahamisha mhusika, akionekana kuwa mbishi basi ananyimwa access ya kuwa na signature. Hii pia hujitokeza kwa avatars.

Na hii ndo huwapa mods kazi ngumu, wanajaribu kuzipitia threads kuangalia kama zinastahili kubakia katika public domain au zinavunja yale niliyoonyesha kwa rangi nyekundu hapo juu.... Inakuwa ni mtihani lakini kwa ushirikiano wa members wanaojali basi huzifanyia kazi accordingly.


IELEWEKE KUWA:

JF kamwe haitamsimamia au kumpendelea mtu kwa sababu ya DINI yake au ITIKADI YA KISIASA aliyokuwa nayo.

Tutaendelea kutoa uhuru, hatuwezi kumfungia mtu kwakuwa hupendi anavyopingana na mtizamo wako wa kisiasa au kidini; kama huwezi kujizibizana naye kaa mbali naye.

Hatutamwonea huruma yeyote anayeonekana kutaka kuvunja sheria kwa kisingizio chochote kile; endapo unaona kuna mtu kaenda kombo na sheria hizi usisite kuwasiliana nasi, unaweza kubonyeza CONTACT US au hata kutumia barua pepe kwenda support@jamiiforums.com ili hatua za haraka zichukuliwe.

Malalamiko ya baadhi ya comments au topics kuachwa bila kutoa ushirikiano kwa kuziripoti hoja zenyewe via REPORT Button (inaonekana kwa wanachama).


Soma mwongozo kwa watumiaji hapa: JamiiForums' Community Engagement Guidelines
 
Asante sana Invisible kwa kutukumbusha kuendelea kuzitunza sheria zetu tulizojiwekea, maana JF inazidi kuwa kubwa sasa ina wanachama wa rika mbalimbali wenye uwezo tofauti, kuna wenye elimu ya kati, kuna maprofesa, kuna viongozi wa kitaifa, kuna wanafunzi/walimu, vile vile kuna wazuri na wabaya etc.

Kwa hiyo JF inahitaji organization ya hali ya juu ili ku maintain huo mchanyato, bila kufanya hivyo tunaweza kujikuta tunafanya mambo ya ajabu ajabu. Nilishawahi kushuhudia members wa Forum fulani (ya nje) wakipelekana mahakamani kwa sababu ndogo tu ya tofauti iliyoachiwa iwe sugu kwenye posts zao.
 
lugha zisizopendeza ni vyema zikakoma....huwa nakumbusha kuna watoto nao wanapita humu tuwe wazazi na walezi wema wa taifa letu kwa ujumla......!
 
umesema. lkn mbona topic yenye opposite na slaa hufutwa mara moja?
Mkuu, how many times unaanzisha topic zilizo opposite na Slaa? Huwezi ku-sense kitu unapoanzisha nyingine na zikaondolewa?

Kumbuka, tunaweza kutofautiana kwa hoja, vikiingia vioja basi huichakachua hoja ya mhusika na kuipelekea aidha 'natural death' au kutupwa kapuni. Vinginevyo, wewe endelea kurusha mawe; nilimwona Slaa mwenyewe akikujibu kuwa anafurahishwa na changamoto anazozipata kwako na anaelewa unakuwa unalenga nini, sasa unapopata mtu akakubali kukusoma basi jaribu kumpa heshima na umwulize kiungwana swali lako ili apoteze dakika kadhaa kufikiria majibu muafaka.

Mkuu invisible, hivi thread ikifungwa au kufutwa inakuwa bado inaonekana?Na hizi tunazokuta zimepigwa msitari juu yake ziko kundi hilo?Nisamehe kama imeelezwa na nimeruka. Asante.
Mkuu, ukiona topic imepitishwa mstari katikati, maanake mjadala umefungwa kwa mjadala zaidi lakini unaruhusiwa kusoma kilichomo kwenye mjadala husika; kama unadhani mjadala huo unahitajika bado basi unaweza kuwafahamisha mods na wakachukua hatua za haraka kuufungua ili uendelee. Hoja iliyofutwa kabisa haipo wazi kwako hivyo kuweza kuirejelea ni vigumu.

Shukrani wakuu
 
Mkuu Invisible!

Kwa kweli na mimi kuna wakati nilihisi labda una wasaidizi wa kukujibia baadhi ya mambo, kiubinadamu hii shughuli inabidi uwe na Turbo equipment ,ndio uweze kuifanya na la kusikitisha ni bahati mbaya /nzuri kuwa unafanya kazi na binadamu-mawe, matope vyote vinakuja kwako ni nadra kuwapata watu wanao angalau tambua kuwa hii kazi ni ngumu.

Anyway wakati mwingine mengi tunafanya kwa ajili ya binadamu-hujui wangapi wanafaidi hata kama hawasemi. Mungu azidi kukujalia hizo nguvu au kama ni vidonge uzidi kupata ambavyo vina nguvu zaidi. Maana watu hawataki hata uugue masaa kadhaa-JF ipo kazi!:confused2:
 
Invisible,

Makala yako ndefu sana ila umeeleweka, labda utekelezaji ndio utakuwa mgumu.

Kuna watu naona kila siku wanakiuka lakini hawachukuliwi hatua.
 
mmh!! Umesomeka, ingawa nilikuwa nasinzia nashituka naendelea kwa huo urefu.
 
Mkuu Invisible, nashukuru kwa kutukumbusha. Sijui kwannini sijawahi soma, nilikuwa na-presume something else. Having gone through it, really good material kwa ajili yetu. Thanks Mkuu kwa kazi nzito hapa jamvini.

Ukweli ni kuwa watu kama MS huwa wanakera, naona tumepumzika sasa!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…