Mwanamama wa kimarekani Lizzie Velasquez alizaliwa mwaka 1989 akiwa na tatizo kubwa sana la mwili wake kukosa uwezo wa kuweka akiba ya mafuta. Hiyo ina maana kwamba hawezi kamwe kunenepa. Hali hii inamfanya aonekane kiumbe cha ajabu sana na wasiokuwa na huruma humcheka sana na kumdhihaki kwa kumpachika majina ya ajabu.
Baadhi wamempachika 'cheo' cha mwanamke mwenye sura mbaya kuliko zote duniani n.k.
Mbona mzuri jamani kila mtu amshukuru Mungu kwa jinsi alivyomuumba kwani ni neema tu..yy amejikubali na maisha yanaendelea. Tusithubutu kudhihaki kwa namna yoyote
Huyu mwanamke ni mzuri sana kuliko hata wenye sura nzuri au maumbo mazuri, msikilize hapa akiongea kwenye TED uone alivyobarikiwa kuliko wanawake kibao tu. binafsi ananiinspire sana.