Miiko ya kuishi Dar Es Salaam ili uepuke kuibiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miiko ya kuishi Dar Es Salaam ili uepuke kuibiwa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by nhassall, Oct 2, 2012.

 1. n

  nhassall Senior Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Miiko ya kuishi dar ili uepuke kuibiwa

  Huu ni ushauri wa bure kwa wale wanaokuja dar


  1. Usiwe ni mwenye tamaa. Ukiwa na tamaa kuibiwa ni rahisi sana kwa njia ya kutapeliwa. Binafsi nilishakoswakoswa mara mbili miaka ya 90 na matapeli. Nlikuwa natembea njiani, mmoja akanipita na kuangusha kifurushi, aliyuwa nyuma yangu akaja akakiokota na kuniuliza yule jamaa kaangusha nini. Muda mfupi yule aliyeangusha akarudi, alipofika usawa wetu akasema kwa sauti kuwa ameangusha shilingi laki mbili. yule niliyekuwa naye akanitaka tukagawane. Bahati nzuri mi mtoto wa mjini, sikuwa wakuja na pia sikuwa mwenye tamaa, nikamwambia akatoe sadaka kanisani/msikitini.

  2. Usigombanie kuingia ndani ya daladala, unaweza kuibiwa kilichomo mifukoni mwako au katika pochi/begi/mkoba. Subiri vurugu zipungue kisha utapanda.

  3. Kuwa makini na abiria wanaopanda wakiwa wameshika gazeti/vijarida mkononi, wengine huvaasuti za nguvu ili waonekane ni maofisa, wengi wao hua ni vibaka/wezi. Wanabeba magazeti na kuvaa suti ili usiwastukie kirahisi. Magazeti hutumika kuficha mikono yao wanapokuchomoa pesa mfukoni.

  4. Pia kuwa makini na abiria wanaopanda wakiwa wamebeba mabegi ya wanafunzi, baadhi yao ni vibaka, hubeba mabegi ili wasistukiwe kuwa ni wezi.

  5. Ukiona abiria mwenzio hataki kusogea mbele angalia mifuko yako. inawezekana anakusimamisha kusudi ili kibaka wa nyuma yako akuibie.

  6. Ukishuka kituoni angalia kama kuna abiria ulipanda nae kituo kimoja naye pia anashuka uliposhuka wee. Huenda anakutafutia muda muda muafaka akupore baada kushindwa kukuibia ulipokuwa ndani ya gari.

  7. Usicheze michezo ya kamali kama vile karata tatu hata kama ukikuta wanawake au wazee nao wanacheza, siku hizi hata wanawake na wazee pia ni wezi.

  8. Ukienda karume au kwengineko kununua bidhaa usipokee pesa toka kwa muuzaji baada ya kuwa mlishapatana atakuuzia kwa kiasi gani kisha baadaea anakwambia kuwa uongeze pesa au acha bidhaa na uchukue pesa zako. Ukikubali kupokea pesa ujue unapewa pesa bandia au pesa pungufu.

  9. Usinunue simu barabarani, utauziwa kipande cha sabuni

  10. Unapoingia sehemu kwa mtindo wa foleni mfano ubungo stendi ya mkoa, angalia walioko nyuma yako, inawezekana unaingia ndani au unaongozana na wezi wa kukuchomolea
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Hiii nzuri asante kututaarifu
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  mwenye masi,na na asikie.....
   
Loading...