HOMOSAPIEN
JF-Expert Member
- Mar 31, 2011
- 745
- 273
Naomba msaada kidogo wa kutaka kuelimishwa,kuna jambo limenitatiza jana wakati naangalia kipindi cha Prof. Shivji cha Katiba,kipindi kinachorushwa na ITV,kuna Mshirika mmoja aliimuuliza Prof.kuwa anapata tabu kidogo wakati ikiongelewa Tanganyika,ambayo haipo kwa sasa kutokana na muungano lakini Zanzibar nchi iliyoungana na Tanganyika bado ipo na wanajitambulisha kama wanachi wa Zanzibar na wana serikali yao.sisi wa bara tunajitambulisha kama wa Tanzania Bara kwa nini na sisi tusijitambulishe kama wa Tanganyika?
Majibu ya Prof. yalikuwa kuwa hiyo Tanganyika haikuwepo, na kama ilikuwepo ni kwa muda wa miaka mitatu tu kabla ya muungano hivyo haikuwepo,nashindwa kumuelewa huyu Prof. Kwani katika historia nimejifunza na kuelewa kuwa Tanganyika ilikuwepo zaidi ya mwaka 1885 wakati wazungu walipokaa Berlin na kugawana bara la Afrika kuwa makoloni yao je Zanzibar nayo haikugawiwa?au ilikuwepo kabla ya Berlin?au kabla ya muungano? Kwa nini iendelee kuwepo wakati sisi tumevunja Tanganyika yetu?
Je huyu Prof. tumueleweje? kwanini anapotosha watu kwa mihadhara yake hii,tena kwa macho maangavu! ashauriwe aongee ya ukweli siyo kuwapotosha watu eti kwa kuwa wamezaliwa baada ya muungano.
Historia itamsuta pomoja na kuwa na mazuri yake yote anayoongea,hii inaamsha ari ya vijana kutaka historia ijirudie yaani kuwepo na Tanganyika kama vile ilivyo Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia