Miguu kuuma maumivu makali sana

Miguu kuuma maumivu makali sana

Mr pianoman

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2019
Posts
2,649
Reaction score
6,485
Wakuu natumaini wazima wa afya. Acha niende kwenye mada moja kwa moja

Iko hivi ninasumbuliwa na maumivu makali sana ya miguu (nitaweka na picha ya mfano ili muone sehemu inayo nisumbua hasa) tatizo hili limeanza baada ya kuanza mazoea ya kukimbia.

Mara ya kwanza nilijua labda ni kwa vile nimekaa muda mrefu sana bila kufanya mazoezi. Lakini kadiri siku zilivyo kuwa zinaenda ndivyo maumivu yalivyo kuwa yanaongezeka ikabidi niache nione kama itapoa ila haikupoa kabisa.

Nilimuelezea rafiki yangu akanipa matawi ya miti furani hivi nikawa naikanda hapo kidogo maumivu yalikwisha. Sasa leo nikaona niendelee na mazoezi yangu ya kukimbia.

Duh! Nimekuwa kama vile nimechokoza kidonda wakuu maana ilinibidi niishi njiani tu nirudi home huku natembea maana ni kama vile umepigwa rungu, yani ni maumivu makali sana na mbaya zaidi iliendelea kuuma hata kipindi nimekaa napumzika.

Nikaenda nikaikanda tena na yale majani hapa saivi naona imepoa. Sasa najiuliza ni tatizo gani hili maana naona kama linataka kunikwamisha michongo yangu maana swala la kukimbia mimi Kwangu ni la muhimu sana ila miguu naona inaleta nongwa.

Hivyo wakuu naombeni msaada wenu maana ni miguu yote miwili inauma sehemu hiyo hiyo picha nimeweka hapo chini [emoji116] [emoji116]

N.B huo sio mguu wangu ni mfano tu nimewawekea muone sehemu zinazo nisumbua


20200304_211440.jpeg
 
Kuna wakati mashost walinishauri green tea ni nzuri kwa digestion and weight loss. Nilianza kunywa green tea for breakfast, after lunch and before bed time.

Miguu ilianza kuuma, sikujua sababu. Kushuka kwenye gari ilikua kimbembe au uamke ghafla kuchukua simu inayoita.

Siku moja nilikua ninatafuta unga wa ugali, kwenye lile duka nilikuta dagaa, nilikumbuka sijala dagaa muda mrefu. Nilinunua nusu kilo ya dagaa.

Nilifika nyumbani na kupika ugali na dagaa. Kesho yake asubuhi sikusikia maumivu kabisa. Nilikumbuka nilikosa calcium kwenye mwili.
 
Back
Top Bottom