Migomo Ya wanafunzi Elimu ya juu

MndemeF

Member
Jan 15, 2011
35
5
Habari wapendwa wangu wote wa jamii forum.Leo ningependa kidogo tushirikishane kuhusu hii migomo ya wanafunzi wa elimu ya juu au vyuo vikuu. Kwa sasa kwa ukweli limekuwa ni donda ndugu ambalo linakuwa ni gumu kupona. Leo wanafunzi wanazua lile na kesho jingine, la kujiuliza ni kweli migomo hii na maandamano yote yana maana?

Jibu ni kuwa mengine yana maana lakini mengine yanachochewa na wanafunzi walioenda pale kwa ajili ya kukua tu na wala si masomo. Kwa mfano maandamano yaliyowafanywa na wanafunzi wa UDSM hapo juzi kwa ajli ya kuishinikiza serikali kuongeza kiwango cha malipo wanayopata kwa siku kutoka sh 5000 mpaka sh 10,000 kwa kweli yanasikitisha sana. Iweje leo mwanafunzi uleenda kusoma kwa kodi ya watanzania wote uhitaji malipo makubwa kwa siku wakati wazazi wenu huko vijijini wanaishi kwa pesa isiyofika hata sh 5000 kwa siku? Tuseme ule ukweli kabisa ya kuwa wengi wenu mnapopata hiyo pesa badala ya kuitumia kwa matumizi ya maana nyie mnakimbilia kununua TV na Radio. Kumbukeni ya kuwa Serikali yenu inatumia pesa nyingi kwa ajili yakuwasomesheni ile mje kulitumikia taifa baadaye. Naogopa kuwa ipo siku moja serikali itaona kuwa ni bora kufuta kabisa hata hicho kidogo inachotoa ili kila mwanafunzi akitaka kusoma chuo kikuu ajilipie mwenyewe. hapo wadogo zenu mtakuwa mmewavictimize. Mnasema ni mkopo mbona mkimaliza mnakuwa wagumu kulipa? Acheni hizo someni bwana!
 
you don't know what you are saying...tena kama wewe umemaliza chuo na umesahau ulipotoka t's ok! but know there is real pain kwa wale wanaoishi kwa siku bila hata maji ya kunywa! i dont want to harass you bt just to keep you off if you dont have any feeling over what majority are experiencing!
 
Back
Top Bottom