Migogoro yawagawa wabunge Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Migogoro yawagawa wabunge Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 20, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 19 December 2011 20:51

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  Mussa Juma, Arusha

  WABUNGE wa Mkoa wa Arusha, wamekwama kuunda umoja wao kutokana na makundi na migogoro iliyopo baina yao na hivyo kukwama kuwa na sauti ya pamoja bungeni.

  Mbunge wa Viti Maalumu wa CCM, Mary Chatanda akizungumza katika kikao cha 30 cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Arusha, alimuomba ,mkuu wa mkoa huo, Magesa Mulongo kusaidia kushawishi wabunge hao kuanzishwa umoja huo.

  Mkoa wa Arusha una jumla ya wabunge 11 ambapo kati yao wabunge wa Chadema ni wanne na CCM ina wabunge saba na kabla ya uchaguzi uliopita Mwenyekiti alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa.

  Akizungumza katika kikao hicho, Chatanda ambaye pia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, alisema kutokuwa na umoja wao kunasababisha kushindwa kuwa na sauti ya pamoja bungeni katika kutoa hoja zinazohusiana na maendeleo ya Arusha na kuzitetea.

  "Mwenyekiti(mkuu wa mkoa) tusaidie kuundwa kwa umoja huu ili tuweze kukaa kwa pamoja kwani wenzetu bungeni wamekuwa na vikao vyao na kukaa na kukubaliana kwa maslahi ya mikoa yao, kuna mengi yanayokwamisha lakini sipendi kuyataja," alisema Chatanda.

  Akijibu hoja hiyo, Mkuu wa Mkoa Arusha, Mulongo alisema kuwa na umoja wa wabunge ni jambo muhimu sana kwani utasaidia kusukuma mbele masuala ya maendeleo ya mkoa.

  Alisema kwa hali ilivyo sasa mgawanyiko wa wabunge hao, unaweza pia kuathiri utendaji kwani pia unaibua mgawanyiko miongoni mwa watendaji wa Serikali.

  Alisema atajitahidi kuwashawishi Wabunge wa Mkoa wa Arusha kuwa na umoja wao na ikishindikana atatoa taarifa katika kikao kijacho cha bodi ya barabara ya mkoa."Mimi nitajitahidi kukutana na wabunge lakini watakayosema nitakuja kuwaambia hapa, ni vyema wajue migogoro yao kama ipo haina manufaa kwa wananchi kwani wao wanataka maendeleo," alisema Mulongo.

  Mkuu huyo wa mkoa pia aliwataka wabunge hao, kujenga tabia ya kuhudhuria vikao vya maendeleo ya mkoa kama cha bodi ya barabara na kamati ya ushauri ili wajue kero za wananchi na kuzifikisha bungeni.

  "Mimi bado ni mgeni lakini naona hata mahudhurio ya vikao sio mazuri sana," alisema Mulongo.

  Mkoa wa Arusha ni mmoja wa mikoa ambayo imeathiriwa sana makundi ya ndani ya CCM ambayo pia yalichangia chama hicho kupoteza viti kadhaa vya udiwani na ubunge

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Magamba yamekamata baridi yanaomba sweta.
   
 3. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  sasa chatanda anasifaa za kukaa meza moja na watu makini kama lema? maana wazo moja la lema ni sawa na 500 ya chatanda. acha magamba wajishaue!
   
 4. m

  matawi JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Magamba wauaji wakae na nani hawa subirini kimbunga cha 2015
   
 5. K

  Kampemba Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Chatanda si Mbunge wa mkoa wa Tanga!ama
   
 6. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145

  Mjinga hapo si ema sasa kama anawaza njia moja tu kufanya jambo. Chatanda anawaza njia 500 kufanya jambo moja. Ama kwa hakika huyu ni mwenye nguvu sana na matokeo ya ku-exhaust possibilities ni ufanisi zaidi. Ema atakuwa mjinga sana kwa fikra zako. Is he thinking outside the box. Chatanda hapa atakuwa genius IQ 170 hivi na ema pengine IQ 60. Au ulimaanisha vinginevyo?
   
 7. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wewe ni mgumu wa kuelewa, kama mtu anatoa wazo moja tu na linapelekea solution kupatikana bila chenga anawezaje kuwa ni sawa na mtu anayetoa mawazo yanafeli mpaka mia tano ndo anapata solution? Hata ingekuwa mtihani chatanda angefeli maana asingemaliza mtihani.
   
Loading...