Migogoro ya Ardhi Tanzania

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Wanajamvi mtakubaliana nami kwamba migogoro ya ardhi inaongezeka.

Sababu ziko nyingi ambazo ama zinatokana na mgongano wa Sera ya Ardhi (1996) au Sheria ya Ardhi (1999 - 4&5). Ila ukweli ni kwamba tunahitaji kufanya maendeleo kwenye kipande hicho hicho cha ardhi.

Mathalani kwa Serikali ya 5 ya viwanda (km kuongeza thamani ya mali ghafi), kiwanda kitahitaji huduma mhimu kama vile barabara, maji, umeme, nyumba za watumishi, huduma za afya na elimu kwa watumishi nk. Nawaza katika vijiji vingi hapa nchini kuna ardhi tupu kwa ajili ya haya mahitaji. La, itabidi wanakijiji waondolewe. Ni balaa na shidaaaaH.

Lakini inawezekana kwa teknolojia ya kisasa (geomatics & geoinformatics) kuweka mipango ya matumizi ya ardhi bila kulazimika kufanya ukaguzi/utafiti wa ardhi. Baada ya hapo Sheria ya Ardhi (1999 - 4&5) kutumika.

Natoa hoja
 
Kama kuna ardhi tupo huko vijijini si waende wakawekeze huko! Kwa nini wanakijiji waondolewe?
 
Vijijini wapi kuna ardhi ya kuwekeza. Suala je tumejiandaa kutenga ardhi vijijini kwa ajili ya miradi ya maendeleo au ndiyo mfululizo wa bomoa bomoa!
 
Wanajamvi mtakubaliana nami kwamba migogoro ya ardhi inaongezeka.

Sababu ziko nyingi ambazo ama zinatokana na mgongano wa Sera ya Ardhi (1996) au Sheria ya Ardhi (1999 - 4&5). Ila ukweli ni kwamba tunahitaji kufanya maendeleo kwenye kipande hicho hicho cha ardhi.

Mathalani kwa Serikali ya 5 ya viwanda (km kuongeza thamani ya mali ghafi), kiwanda kitahitaji huduma mhimu kama vile barabara, maji, umeme, nyumba za watumishi, huduma za afya na elimu kwa watumishi nk. Nawaza katika vijiji vingi hapa nchini kuna ardhi tupu kwa ajili ya haya mahitaji. La, itabidi wanakijiji waondolewe. Ni balaa na shidaaaaH.

Lakini inawezekana kwa teknolojia ya kisasa (geomatics & geoinformatics) kuweka mipango ya matumizi ya ardhi bila kulazimika kufanya ukaguzi/utafiti wa ardhi. Baada ya hapo Sheria ya Ardhi (1999 - 4&5) kutumika.

Natoa hoja
Sheria za ardhi c mbaya kivile.
Migogoro mingi ya ardhi imesababishwa na watumishi wa ardhi wenye tamaa ya pesa kwa kuuza maeneo mara mbili.
Aidha baadhi ya kamati za ardhi za vijiji nazo ni chanzo kwa kushindwa kuanisha matumizi ya ardhi.
Kwa mfano maeneo ya ufugaji, kilimo, makazi, maeneo ya wazi.
. Migogoro hii tunaoiona leo ni matokeo ya ukiukaji wa taratibu siku au miaka iliyopita.
 
1465572607770.jpg
 
Back
Top Bottom