Migodi ya dhahabu kuanza kulipa ushuru

Migodi ya dhahabu kuanza kulipa ushuru

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2007
Posts
852
Reaction score
204
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TANGAZO.

MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI.

Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika. Halmashauri zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014.

Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement - MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali.

Mha. Ngosi C.X. Mwihava
KAIMU KATIBU MKUU
25 Februari, 2015

ni habari njema hii hongera sana Waziri Simbachawene na timu yako
 
Kwahiyo mda wote walikuwa hawalipi,mmeona mdamuafaka wao kulipa ni sasa tena 0.3.laita serikali ingekuwa inakomalia migodi kulipa kodi,Kama inavyokomalia wafanyabiashara wadogowadogo,basi nchi hii isingehitaji Misada toka nje
 
MAPATO YA SERIKALI KUTOKA MIGODI YA DHAHABU YAONGEZEKA: Timu ya Muhongo iliongeza mapato ya Serikali kama ifuatavyo: (1) Migodi inalipa30% CorporateTax. Majadiliano yanaendelea kwa migodi ambayo bado haijaanza kulipa kodi hii. (2) Mrabaha (Royalty) imepandishwa kutoka 3% hadi 4% - migodi yote inalipa (3) Service Levy (inalipwa) kwa HalmashaurI sasa ni 0.3% ya mapato yote ya mgodi Baadhi ya Halmashauri kupata zaidi ya USD 1M badala ya Dola Laki 2/mwaka.
 
nadhani kiasi cha fedha kinaweza kusaidia kuonyesha uhalisia maana nchi hii ina wasanii wengi, mnaweza kubadili asilimia ya viwango mnamtuma mmoja wenu kwenda kudai akienda kule wanajadiliana wanabadili figure kuonyesha biashara kidogo hivyo malipo yanabaki pale pale au kushuka ingawa viwango vingepandisha.

kama kuna takwimu kuwa mfano mwaka juzi tulipata kiasi fulani na mwaka jana tulipata kiasi fulani inaweza kusaidia.

lakini ni vema kama kuna takwimu za nchi nyingine ni bora zikiwekwa wazi maana yawezekana bado kwa viwango hivyo tunaibiwa pia.

MAPATO YA SERIKALI KUTOKA MIGODI YA DHAHABU YAONGEZEKA: Timu ya Muhongo iliongeza mapato ya Serikali kama ifuatavyo: (1) Migodi inalipa30% CorporateTax. Majadiliano yanaendelea kwa migodi ambayo bado haijaanza kulipa kodi hii. (2) Mrabaha (Royalty) imepandishwa kutoka 3% hadi 4% - migodi yote inalipa (3) Service Levy (inalipwa) kwa HalmashaurI sasa ni 0.3% ya mapato yote ya mgodi Baadhi ya Halmashauri kupata zaidi ya USD 1M badala ya Dola Laki 2/mwaka.
 
Hayo yako ktk makaratasi tu , unadanganya umma.
Mbona hamsemagi pesa za mgao kutokana na hisa?
Kwa nn ndege zinachukua madini juu kwa juu?
 
MAPATO YA SERIKALI KUTOKA MIGODI YA DHAHABU YAONGEZEKA: Timu ya Muhongo iliongeza mapato ya Serikali kama ifuatavyo: (1) Migodi inalipa30% CorporateTax. Majadiliano yanaendelea kwa migodi ambayo bado haijaanza kulipa kodi hii. (2) Mrabaha (Royalty) imepandishwa kutoka 3% hadi 4% - migodi yote inalipa (3) Service Levy (inalipwa) kwa HalmashaurI sasa ni 0.3% ya mapato yote ya mgodi Baadhi ya Halmashauri kupata zaidi ya USD 1M badala ya Dola Laki 2/mwaka.

Mzee Ruge alikuwa na hisa 30% tu za VIP but kavuna mabilion kibao !!!
Sasa wewe tuna migodi nchi nzima and then you are talking about that rabish money as nation???
That money is not Tanzanian level compared with mining we have!!!
Labda useme zimetoka GGM na BUZWAGI tu.
 
Serikali imeanza kupokea viwango vipya vya kodi kutoka kwa Kampuni za uchimbaji madini hapa nchini, hatua ambayo ni utekelezaji wa makubaliano ya uboreshaji wa viwango vya ulipaji wa mirahaba, kodi ya huduma na ile inayolipwa na makampuni makubwa. Taarifa za uhakika zilizolifikia Dira ya Mtanzania kutoka vyanzo vyake vilivyoko serikalini zimeeleza kuwa kampuni zinazojihusisha na uchimbaji madini hapa nchini zimeanza kulipa viwango vipya vya kodi ikiwa ni utekelezaji wa agizo lilitolewa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kampuni hizo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kampuni hizo sasa zimeanza kulipa viwango vipya vya kodi ya asilimia 30 ya mapato yanayokusanywa na wazalishaji inayolipwa na makampuni makubwa. Kwamba baadhi ya kampuni ambazo hazijaanza utekelezaji wa ulipaji wa viwango vipya vya kodi hiyo ziko kwenye hatua za mwisho za majadiliano na Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hilo
.>>>>>>>>>>> (CHANZO; GAZETI LA DIRA)
 
Sidhani kama kuna ukweli wowote kuhusiana na hii taarifa, pengine ungetuambia mwanzoni walikuwa wanalipa kiasi gani. Ninavyofahamu ukijulishalipa kodi zote ( kutoka kwenye mauzo ya dhahabu+PAYE ya wafanyakazi migodini) ilikuwa haizidi hata 3%. Ila taarifa zilizopo ni kuwa midogo ilikuwa inalipa kama $200,000 kwenye Halimashauri na kiwango hicho kwa sasa kimebadilishwa na kuwa 0.3%. Hii ya 30% lete taarifa kamili.
 
Kwahiyo mda wote walikuwa hawalipi,mmeona mdamuafaka wao kulipa ni sasa tena 0.3.laita serikali ingekuwa inakomalia migodi kulipa kodi,Kama inavyokomalia wafanyabiashara wadogowadogo,basi nchi hii isingehitaji Misada toka nje

Kweli kabisa mtanzania mfanyabiashara anabanwa hatakiwi kuinua kipato chake kwa ukubwa wa mzigo wa kodi anao ubeba.Mfano ukiwa una Nyumba ya kupangisha unatakiwa kulipa kodi ya mapato 10% ya kodi unayolipwa pamoja na ushuru wa stempu 1%,matokeo yake tunayajua nini kinatokea.
wageni wanalipa 0.3% tumelogwa au kunakitu kinachezwa :Nyoka Mwenye Makengeza anajua ukweli wa hizo hesabu.
 
Serikali imeanza kupokea viwango vipya vya kodi kutoka kwa Kampuni za uchimbaji madini hapa nchini, hatua ambayo ni utekelezaji wa makubaliano ya uboreshaji wa viwango vya ulipaji wa mirahaba, kodi ya huduma na ile inayolipwa na makampuni makubwa. Taarifa za uhakika zilizolifikia Dira ya Mtanzania kutoka vyanzo vyake vilivyoko serikalini zimeeleza kuwa kampuni zinazojihusisha na uchimbaji madini hapa nchini zimeanza kulipa viwango vipya vya kodi ikiwa ni utekelezaji wa agizo lilitolewa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kampuni hizo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kampuni hizo sasa zimeanza kulipa viwango vipya vya kodi ya asilimia 30 ya mapato yanayokusanywa na wazalishaji inayolipwa na makampuni makubwa. Kwamba baadhi ya kampuni ambazo hazijaanza utekelezaji wa ulipaji wa viwango vipya vya kodi hiyo ziko kwenye hatua za mwisho za majadiliano na Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hilo
.>>>>>>>>>>> (CHANZO; GAZETI LA DIRA)

Huwa hatusemi agizo la waziri badala yake tunasema agizo la serikali
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TANGAZO.

MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI.

Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika. Halmashauri zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014.

Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement - MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali.

Mha. Ngosi C.X. Mwihava
KAIMU KATIBU MKUU
25 Februari, 2015

Hii ni habari ya zamani. Uamuzi huu ulifanyika February 2013 baada ya shinikizo la Maswi na Muhongo. Hili siyo habari ya leo wala kazi iliyofanywa/fanikishwa na akina Simbachawene kama mleta hoja anavyotaka kutuaminisha.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TANGAZO.

MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI.

Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika. Halmashauri zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014.

Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement - MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali.

Mha. Ngosi C.X. Mwihava
KAIMU KATIBU MKUU
25 Februari, 2015

ni habari njema hii hongera sana Waziri Simbachawene na timu yako
hivi huwa mnasomaga habari kweli kabla ya kuchangia? au huwa mnakurupukaga tu?

30% ni sheria, wala sio agizo!
 
Back
Top Bottom