Migiro leaves UN post; forced out or chose to leave?

Atafaa sana awe balozi wetu UN na itamsaidia mwanae amalize masomo, na pale utendaji wake tutausimamia wenyewe Watanzania tunayemuelewa. Nadhani Tanzania itamfikiria katika hili mara tu baada ya kurudi huku.

Yaani wewe unachoangalia kigezo cha yeye kuwa balozi UN ni mtoto wake amalize shule?.......Only in Tanzania.
 

.....a disappointment indeed. inaonekana ombi lake la kupata contract extension limekataliwa.

inaripotiwa kuwa sasa hivi anahaha namna ya kuhakikisha mwanae anayesoma huko amalize shule yake......je, hii haiwezekani ndiyo driving force ya yeye kuomba extension?? ubinafsi, huh?

anyways, kuna uwezekano kuwa tusipokuwa careful huyu failure aweza akawa ndiye our next prez... tujipe pole in advance!!
 
Hivi Asha Rose Migiro ni mkristo au muislam.Msaada tafadhari
 

na siasa za maji taka za bongo na nchi yenyewe magamba hayavuliki, duh! kazi ipo
 
Kama ndo anataka kugombea urais asahau hilo!! Kila mtu anatolea macho hiyo chance from lowassa to sitta etc...
 
Haya mama karibu bongo! Huku kuna Captain wa nchi anaitwa Edward Lowassa. Ila nasikia huyu mama ni godoro na ni mfuasi mtiifu wa EL. Anaandaliwa kuwa PM wa EL
 
May be ufanisi wake ulikuwa mdogo ndo maana U.N wamekataa kumpa Mkataba mpya.
 
Kurudi kwake c mbio za urais tu 2015 kama ambavyo JK anaweza taka kumbeba,bali ukweli mtiti wa UN umemshinda otherwise ilikuwapo nafasi ya kuongezewa/extension, nadhani aliendeleza mambo ya bongo kwa wenzetu


Si lazima kuongeza muda wa mkataba wako ukimalizika
 

Madondoo muhimu katika taarifa hii:
1- Bwana Ki Mwezi alimteua Migiro kama zawadi kwa Tanzania: Hii inaonesha zaidi kulipana fadhila kuliko sifa za utandaji. Abebwaye hujikaza, na dada yetu inaonesha alijilegeza ndio maana Ki Mwezi anataka kuutua mzigo.

2- PS anasema "Dr Migiro’s tour of duty at the New York based UN headquarters was over. “We have not received an official document from the UN, but I’m aware that her tenure is almost ending,”
Hapa inaonesha lugha ya kejeli ya PS kwa Dr. Migiro's tiur. Ama hata huku TZ walihisi kuwa alikuweko kule kiutalii talii, au chuki binafsi za PS kwa Migiro.

3- Hii habari imekalia kiudaku udaku kwani habari makini haiwezi kuwa We have heard bla bla bla... hakuna uhakika bado.

4- Mr Ban said he intended to build a new team that was strong on substance and diverse in composition—what he called “a team that works as one”.....“Leading by example, I have placed priority on mobility, combining fresh perspectives and institutional continuity and synergy.”
Hapa tukichanganya na 1, i.e. kuteuliwa kama zawadi, kubebwa ukabweteka, ndiko kunakompelekea Bwana Ki Mwezi kutaka timu nyengine ambayo inaonesha kuwa Dr. wetu hayawezi.

Hata hivyo, wakati ndio utakao tupa jawabu kwa suala hili. Hata hivyo, lisemwalo lipo, kama halipo ni umbeya [Source: Lizzy].
 
tuwaulize watu wa usangi kama ana mume ila najua ana mtoto
na ni mwl wa sheria pale UDSM labda atarudi kufundisha
anaweza kuwa raisi ndio tena mzuri tu na atatukomboa kwa vile
damu ya magamba haijamdhuru kama hawa wengine.
 
aje atuambie ameachia post kubwa kuja kulitumikia taifa lake na kutokana watz wengi ni wavivu kufikiri watamchagua kila la kheli bi asha..

shavu la ukweli ameliacha hilo plus watu wanataka hiyo chance lowassa, sumaye, sitta n.k.. Kazi ipo hapo.
 
Sijawahi sikia jk kaenda marekani na mkewe i.e. Salima unganisheni dot.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…