Migambo wa vita vya Kagera

Mbona hata leo.zikitokea fujo.wanaotangulizwa ni mgambo.ni kawaida.labda ilo neno kuwa chambo ndo sio zuri kulitumia.ila wao utangulizwa mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilikuwa kidato cha kwanza maji nilikuwa siiiti Mmaaah ila uzi huu nimeona nichangie umenigusa sana.Kwanza kabla ya yote tujivunie sana uzalendo wa wakati ule na umoja wa kitaifa ndio ulichangia sana tukashinda vita ile.Ile vita tumepigana bila kusaidiwa msaada wa kifedha kutoka taifa lolote lile.Nchi za magharibi labda zilikuwa zinatukomoa shauri ya msimamo wa raisi wetu Mwl Nyerere.Wakati ule uzalendo ulikuwa mpaka chini mwanafunzi mdogo wa shule ya msingi.Shuleni kwetu tulichimba handaki na tulifundishwa jinsi ya kujihami tukisikia mlipuko au sauti ya ndege kila mwanafunzi alikuwa anajua kufungua silaha na kuifunga.Si kweli kuwa tulikuwa na jeshi la mgambo pekee mstari wa mbele kulikuwa mpaka na raia waliojitolea.Askari wetu kuhus chakula mpaka raia shinyanga walikuwa wanajitolea ngombe kama chakula kwa askari wetu.Marehemu Brigedia Yusuph Himid ndio alikuwa na kikosi hichi cha mgambo chini ya ungalizi maalum wa askari waliobobea wengi au wote walirudi salama kabisa kuwa walikufa sana sio kweli.Kuna majina makubwa maarufu wakati huo makamanda Mayunga,Herman Lupogo(amphibian) huyu battaliani yake ilipewa jina hili maana walilala kwenye maji kwa zaidi masaa nane,John Walden,Tumainieli Kiwelu,Imrani Kombe,Kanali Makunda(Torpedo),Kanali Tumbi(radi) huyu alikuwa mkuu wa kikosi cha mizinga ndio alimtesa Iddi Amini akapewa jina la Radi,Kanali Kitete(Supersonic), Kanali Bayeke,Major Robert Mboma wakati huo alikuwa mkuu wa kikosi cha anga,Brig David Musuguri(kamanda Mutukula),Nsimanyi,Mwita Ernest Kiaro,Abdala Twalipo,Mike Marwa
Hawa na wengine ndio waliomtoa Nduli wengine nimewasahau na wengine wametangulia mbele za haki mungu awarehemu walipo na ambao wako bado hai mungu azidi kuwaimarisha kiafya.Nimeamua kuchangia uzi huu kwa ajili ya kuwaenzi mashujaa hawa walioliletea heshima kubwa taifa letu na mpaka leo kwenye ramani ya dunia jeshi letu lina sifa kubwa
 
Niliwahi kwenda pale Hazina Dar mwaka 2001,nilimpeleka marehemu mzee wengu kufatilia mafao yake,wakati tukiwa kwenye foleni kuna mzee mmoja akawa anamuangalia sana mzee wangu,kwa bahati mbaya mzee wangu alikua ameharibika masikio so akawa hasikii vzr,ikabidi nimuulize kulikoni?akasema anamfananisha kama walikua kwenye kambi moja ya jeshi(Buhemba).nikamwambie sijui,nikamuuliza kama anamkumbuka jina akalitaja jina moja ambalo mzee alikua akilitumia kabla hajabadirisha dini,nikamshitua mzee kwamba huyu mzee anakufananisha,kweli na mzee wangu akamkumbuka bwana,wakacheka sana mpaka mle ndani hazina kwenye babenchi ikawa kama ukumbi wa burudani..ikabidi nimpeleke nje ili wakapige story zaidi,dahhhh..yani nilishangaa wakakumbushana hiyo vita..wakawa wanauliza wenzao waliokua nao kwenye uwanja wa mapambano..ilikua burudani sana maana nilikua naona kama imetokea juzi tu.But wengi wao wamechoka sana kimaisha na wana hali mbaya si mchezo.Babangu kafariki 2010 akiacha kibanda tu cha vyumba viwili ingawa alikua mzalendo sana na jeshi.Nikiwa darasa la 4 aliwahi kuniuliza ningependa kufanya kazi gani nikiwa mkubwa?nikamwambia nataka kuwa mwl,dah,nilichezea vitasa vya haja na akasema siku nikiwa mwl nisikanyaje kwake maana hizo ni kazi za kike.Alipenda wototo wake wote tuingie jeshini,but bi mkubwa hakua hakitaka habari za jeshi maana zilimfanya kuishi peke yake kwa miaka miwili wakati mzee akiwa Uganda na pia hakuna faida kwenye familia kutokana na mzee kufanya kazi hiyo.
But now naona mambo yamebadirika sana jeshini maisha poa tu.
Binafsi nimewaona wapiganaji wa vita hii kama 11 akiwemo mzee wangu but ni wawili pekee walio hai na mmoja wapo ni mlemavu wa macho..yani wengi waliathirika sana kiafya.Marehemu mzee wangu alikua akitoka usaha masikioni.
 
Pole sana mkuu kwa kumpoteza mzee wako!
Simulizi yako imenifurahisha sana hasa ulipochezea vitasa kwa kusema ungependa kuwa mwalimu! [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati huo nilikuwa darasa la na mgambo wote niliwafahamu walirudi salama. Kusema kwamba waliwekwa mbele yaweza kuwa si kweli maana wengi wakipelekwa Uganda wakati nduli keshazidiwa nguvu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umenikumbusha mbali!
 
Wonderful pole sana kwa kumpoteza mzee wetu japo na mimi si wongo ni mhenga kidogo lakini mzee wako atakuwa ni kaka yangu mkubwa sana.Ila story yako ya ushuhuda imenifurahisha sana
 
Tulirudi mkuu,mimi nilirudi na cheo cha colonel,
nakumbuka siku tunaichukua jinja,nilikula risasi ya sikio, kutoka kwa mlibya mmoja sniper
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Inawezekana wapo mashujaa migambo walionusurika.

Ndio wapo na wengi wao walikua walinzi kwenye minara ya simu kunammoja alikua analinda tabora bsc na mwingine mnara wa ukumbisiganga (maarufu kama km 60) kwa wenyeji wa kaliuwa
 
Wonderful pole sana kwa kumpoteza mzee wetu japo na mimi si wongo ni mhenga kidogo lakini mzee wako atakuwa ni kaka yangu mkubwa sana.Ila story yako ya ushuhuda imenifurahisha sana
Shukrani mkuu.
 
Aisee dah walivyorudi kutoka uganda waliandaliwa sherehe yao uwanja wa uhuru dsm hasa chakuudhunisha ni pale askari wanapoonesha siraha walizotumia kumpiga nduli amini..walioyesha ndege za vita walizotumia wakiwa wanapta juu ya uwanja kuna ndenga ilianguka daah so sad wananchi acha wapagawe wakajua sijui amini..walimwonyesha JK Nyerere dah alipoa sana....source ITV.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio migambo,waliojitolea walikuwa wengi,wafanyakazi wa taasisi na wananchi wa kawaida.wengine walibaki uganda na kuanza maisha wengine walirudi kujenga nchi kwa namna mbali mbali
 
Mkuu ndoto yako ya kuwa mwalimu ilitimia?
 
Wakati huo nilikuwa darasa la na mgambo wote niliwafahamu walirudi salama. Kusema kwamba waliwekwa mbele yaweza kuwa si kweli maana wengi wakipelekwa Uganda wakati nduli keshazidiwa nguvu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mhenga kwa hiyo wagambo walipelekwa Uganda kufanya finishingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…