Mifumo Nje ya Mifumo (MNM): Ya Nini, Nani, Kwanini na ya Nani...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,483
40,002

Marehemu Jamal Khashoggi​
Na. M. M. Mwanakijiji

Tarehe 2 Oktoba 2018 mwandishi wa habari na mwanablogu kutoka Saudia Bw. Jamal Khashoggi alienda kwenye ubalozi wa Saudia huko Istanbul, Uturuki akiwa na lengo la kufuatilia nyaraka ambazo zingemwezesha kufunga ndoa na mchumba wake. Mchumba wake hakuingia kule Ubalozi bali alibaki kwenye mgahawa Fulani karibu akimsubiria na walikubaliana kuwa endapo hatotoka nje basi dada yule awataarifu watu kadhaa wa kuaminika. Na kweli, muda wa kazi ulikuwa unaishia saa 9:30 jioni lakini ilipofika saa 10 Ubalozi ukafungwa na Khashoggi hakuonekana kutoka. Mchumba akawasiliana na watu wao wa karibu na mara moja Rais wa Uturuki Erdogan akaagiza uchunguzi wa haraka kuanza mara moja.

Haikuchukua muda ushahidi wa awali ulionesha kuwa Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi ule. Uturuki ulidai kuwa kikosi cha wauaji (death squad) kilikuwa kimeingia masaa machache kabla na ndege binafsi. Kikosi hicho kilikuwa cha maafisa wa usalama ambao walikuwa na kazi moja tu kummaliza Bw. Khashoggi ambaye alijulikana kama mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudia ambayo inaongozwa (kwa maana zote) na mwana wa mfalme Bw. Mohammed Bin Salman. Serikali ya Saudia ilikanusha vikali mwanzoni, na ilidai kuwa Khashoggi alitoka ubalozini na kuwa kuihusisha na uuaji ilikuwa ni uchokozi tu wa Uturuki.

Hata hivyo, uzito wa ushahidi kutoka vyanzo mbalimbali ulilazimisha hatimaye Saudia kukiri kuwa kweli Khashoggi aliuawa pale ubalozini na kuwa maafisa wake wa usalama waliohusika na tukio hilo walifanya hivyo bila kutumwa na mtu yeyote, na kuwa 11 kati ya wale 15 ambao walipanga na kutekeleza tukio hilo watakabiliwa na adhabu ya kifo. Mkuu wa kikosi cha Usalama kilichotekeleza hilo alifukuzwa pamoja na msaidizi wake. Mwisho wa siku, licha ya kauli kali kutoka nchi mbalimbali na licha ya ushahidi mzito wa mauaji ya mwanahabari huyo serikali ya Saudia imeng’aka na kuwa Mwana wa Mfalme hausiki, na wale waliohusika wanaweza kunyongwa peke yao.

Mfumo Nje ya Mfumo ni Nini?

Katika utendaji wa serikali karibu zote duniani – ziwe za kidemokrasia au kidikteta, zilizoendelea au zinazotaka kuendelea kuna mifumo miwili mikubwa ya kiusalama. Upo mfumo rasmi wa vyombo vya usalama ambavyo huundwa na majeshi, polisi, taasisi za inteligensia na hata za binafsi ambazo zinaongozwa na kanuni, taratibu na sheria zinazojulikana. Vyombo hivi vya “mfumo rasmi” vina uongozi unaojulikana na unaoweza kuwajibishwa. Kama ni jeshi una mtu wa cheo cha chini kabisa (Private) hadi mwenye cheo cha juu kabisa (General). Mnyororo wake wa amri (chain of command) unaeleweka katika ngazi zote.

Lakini pia kuna mfumo mwingine wa usalama na ulinzi; mfumo ambao unafanya kazi nje ya sheria, taratibu na amri zinazoelweka. Ni mfumo ambao hauna uongozi unaojulikana (wenyewe wanajuana) na unafanya kazi kwa maelekezo na maagizo ambayo hayaachi alama za maandishi (no paper trail) na kwa kadiri inavyowezekana unafanya yale yote ambayo mifumo na watendaji rasmi hawawezi kufanya. Ni mfumo wa usalama na ulinzi ambao unafanya mambo yote ambayo yakijulikana ni rahisi kuyaruka na kuwaruka wahusika wote.

Wahusika ni Watu Ndani na Nje ya Serikali

Mfumo Nje ya Mfumo hufanya kazi kwa kuhusisha watu ndani na nje ya serikali. Unahusisha wafanyabiashara, wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za umma na hata binafsi. Lengo lake kubwa nikilirudia tena ni kufanya mambo yale yote ambayo yakifanywa na mtu mwingine ni ya uhalifu na kwamba endapo yatakuja kujulikana basi wahusika wa mfumo rasmi wanaweza kuyaruka maili nyingi za mbali.

Mifano Mikubwa ya MNM

Kama nilivyosema hapo juu MNM ipo katika nchi zote bila kujali kama ni nchi zilizoendelea au la, zilizo na demokrasia au hapana. Kuna mifano michache ya matukio makubwa ambayo yamewahi kutokea kama nilivyotolea mfano wa Khashoggi. Nitaje mifano michache tu hapa mikubwa:

Kashfa ya Watergate – Marekani

Kati ya mwaka 1972 na 1974 huko Marekani kulitokea kashfa kubwa ambayo iliishia kwa kujiuzulu kwa Rais wa nchi hiyo Bw. Richard Nixon. Kwa ufupi kabisa kashfa hii ilimhusisha Rais Nixon na chama chake cha Republican ambapo iligundulika kuwa Rais alikuwa anatumia njia za MNM kuwapeleleza wapinzani wake. Juni 17 mwaka 1972 vibaka watano walikamatwa wakijaribu kupekua ofisi za chama cha Democrat kwenye jingo la Watergate (ndio jina la kashfa). Ilikuwa jambo dogo lakini baada ya kufuatilia na waandishi kuchunguza mwisho wa siku ikaonekana mpango mzima ulisukwa na kuihusisha Ikulu. Maafisa 69 wa Serikali ya Nixon walikamatwa na kushtakiwa; 48 kati yao walikutwa na hatia na kati yao wapo waliopata vifungo jela, kupigwa faini na wengi kupoteza kazi zao. Nixon mwenyewe alikuwa aondolewe kwa mashtaka ya kibunge (impeachment) lakini akaamua kujiuzulu. Hata hivyo, mrithi wake Gerald Ford alimsamehe. MNM ndio iliyomuangusha Rais Richard Nixon.

Kashfa ya Iran-Contra - Marekani

ni kashfa ya mwanzoni mwa miaka ya themanini huko huko Marekani. Maafisa wa Marekani walikula njama kuiuzia Iran silaha licha ya kuwepo kwa zuio la kuuza silaha kwa nchi hiyo. Japo mwanzoni Serikali ya Rais Reagan ilijaribu kuelezea jambo hilo kuwa ililazima ili kuwafungua wafungwa wa Kimareni huko Iran uchunguzi ulikuja kuonesha kuwa kulikuwa na zaidi ya hilo. Kanali Oliver North (kushoto) wa Baraza la Usalama alitumia baadhi ya fedha za mauzo kwenda kuwapatia waasi wa huko Nicaragua. Uchunguzi wa Bunge ulipofanyika maafisa kadhaa wa serikali ya Reagan walijikuta wanapoteza kazi zao akiwemo Waziri wa Ulinzi na maafisa kadhaa walishtakiwa na kukutwa na hatia mahakamani, akiwemo Kanali North. Hata hivyo, Rais George H. W. Bush aliwasamehe hao wote na kufuta hatia zao.

Operesheni “Ghadhabu ya Mungu” – Israel

Baada ya wanariadha wake 11 kuuawa na wapalestina huko Munich, Ujerumani mwaka 1972. Tukio hilo lilikuja kujulikana kama “Septemba Nyeusi”. Israeli iliapa kulipiza kisasi na kushughulikia wale wote waliohusika kufanikisha hilo kwa hali na mali. Na miezi michache baadaye vikosi maalum vya MNM vya Israeli vilianza kuwaaua (assassinations) watu mbalimbali waliohusika. Zilitumika kila aina ya mbinu na haikujali watu hao walikuwa nchi gani. Hata hivyo, mpango ulivurugika baada ya MNM kumuua mtu asiye na hatia (walimchanganya) huko Norway. Maafisa watano wa Israeli walikamatwa na ndio siri nyingi zilizidi kufichuka kuhusu “Ghadhabu ya Mungu”. Serikali ya Israeli ikasitisha operesheni zake hizo mwaka 1973. Hata hivyo, ikafufuliwa kwa muda mwaka 1979 kumshughulikia yule waliyemkosa kule Norway; walifanikiwa kumuua kwa bomu la gari. Israeli bado imeendelea kutumia mbinu za MNM kwa kushirikisha hata vikosi rasmi kuwashughulikia wale wanaoonekana ni tishio kwa Israeli mahali popote duniani.

MNM Haiwezi Kuzuiliwa; Inaweza Kufichuliwa Tu

Kimsingi ni vigumu sana kuzuia utendaji wa MNM. Hata hivyo, mifumo hii nje ya mifumo inaweza kufichuliwa tu kwa sababu kama nilivyosema hapo mwanzo mara nyingi inajihusisha na vitendo ambavyo kama vingefanywa na mtu mwingine au taasisi nyingine vingeitwa ni vya kihalifu na endapo wahusika wakikamatwa wanaweza kushtakiwa kwa uhalifu na serikali ikawaruka. Ikumbukwe tena kuwa hakuna nchi ambayo haina mifumo hii.

Katika Afrika mifumo hii ilitumiwa sana wakati wa utawala wa Makaburu kule Afrika ya Kusini lakini pia ilitumiwa na nchi zilizokuwa katika Mstari wa Mbele zikiongozwa na Tanzania. Tanzania ilikuwa imetengeneza mtandao mpana sana wa majasusi ambao waliwezesha kupitisha silaha kwenda Afrika ya Kusini na kuwapitisha wapigania uhuru hadi Tanzania ambako walipatiwa hifadhi. Mifumo hii iliendelea kufanya kazi kwa namna nyingi hata baada ya kuanguka kwa utawala wa makaburu.

Kwanini Mifumo Hii Inakuwepo?

Unaweza kuona kuwa mifumo hii ya nje ya mifumo ipo mara nyingi kwa sababu kubwa mbili na zinahusiana. Moja ni kulinda maslahi mapana ya nchi kutoka kwa matishio ambayo hayawezi kushughulikiwa kwa njia halali. Lakini la pili, mifumo hii ipo pia kulinda tawala, viongozi dhidi ya wapinzani wa kisiasa. Mfano wa Nixon hapo juu ni mmoja tu wa kuonesha jinsi gani Nixon alijaribu kutumia ofisi yake na watendaji wengine wa serikali kutimiza malengo ya kisiasa. Kurekodi wapinzani wake wa kisiasa na kuagiza vitendo ambavyo ni vya kihalifu Nixon alitumia vibaya zaidi MNM; lengo ikiwa ni kutaka kushinda uchaguzi. Hata mfano wa Khashoggi hapo juu unahusiana na hili zaidi.

Mifumo hii Haikomi Yenyewe

Mara nyingi mifumo hii inakuwa na matatizo makubwa zaidi pale ambapo inakutana na wapinzani wengi zaidi. Kwa kadiri inavyokutana na wapinzani ndivyo inavyozidi kufanya kazi yake – ya uhalifu kimsingi. Ni muhimu sana kutofautisha hapa utendaji wa vyombo halali na rasmi na hivi vya MNM. Utendaji wa MNM hauwezi kuacha - viongozi wanaoingia na wale wanaotoka hawana umiliki hasa; kila mmoja huwa na timu yake na wengine wanapewa timu na wanaona jinsi wanavyotumia. Njia pekee ya uhakika ni uwepo wa serikali ambayo haiogopi kuficha vitu, haiogopi kuhojiwa au watu kuiangalia kwa karibu.

Wakati wowote serikali inajaribu kuficha vitu, hasa kama hairuhusi vyombo vya habari kuangalia ndani kama kwa kurunzi basi ujue MNM inaanza kuwa na nguvu zaidi. Alama kubwa ya uwepo na nguvu ya MNM iko katika kutokuwepo uhuru mkubwa wa maoni, mawazo, na habari. Mara zote na sehemu zote duniani mifumo ya MNM imejulikana na kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari.

Swali kubwa ni je, kwa nchi yetu MNM imefikia kiwango gani, inaongozwa na nani na inawajibikwa hadi wapi? Je, wale wanaoitwa “wasiojulikana” ni kweli hawajulikani? Naomba kupendekeza kuwa majibu ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara hayajaukaribia ukweli hata kwa sentimita moja. Ukweli bado uko pembeni.

Nini Kinawakuta watu wa MNM

Wiki ijayo inshallah, nitaendelea na sehemu muhimu zaidi. Nini huwa kinawakuta wahusika walioko ndani ya MNM? Je, wanaweza kweli kujificha au kufichwa miaka yao yote? Ipo mifano ya kusikitisha na kushtusha. Je watekaji wanaweza kuwa ndio MNM; nita -activate ka-nzi KIDOGO.
 

Attachments

  • 1563513298036.png
    1.4 MB · Views: 40
Asante sana Mwanakijiji. Tunakuombea afya, inshallah ufungue hili "black box" zaidi ya pale ulipokusudia.
 
Upo sahihi sana. Na taarifa za ndani hasa ni kuwa kwa sasa MNM imekuwa na nguvu sana kuzidi mfumo rasmi.

Kwa wasiojua MNM ipo chini ya Basht. Take my words. Na hiyo ndiyo sababu ya mtu huyu kuwa na nguvu sana. Na siyo sababu nyingine zozote ambazo baadhi ya watu huwa wanadhania.
 
I can smell something fishy sababu naona ni kama unataka kututoa kwenye reli! Naona ni kama unajaribu kuhalalisha udhalimu unaotokea kwa hoja kwamba sio jambo la ajabu kutokea! Naona bado upo kule kule kwenye threads zako za siku hizi ambazo mara kwa mara umekuwa ukihalalisha what's happening kwa kudai yamekuwa yakitokea tangia enzi za Mwalimu! Hata hivyo, leo umeamua kuhalalisha in a more genius way (though I don't buy it), kwa mfano unasema:-
Mfumo Nje ya Mfumo ni Nini?

Katika utendaji wa serikali karibu zote duniani – ziwe za kidemokrasia au kidikteta, zilizoendelea au zinazotaka kuendelea kuna mifumo miwili mikubwa ya kiusalama.
MM anaendelea kuhalalisha yanayotokea na kuonesha hilo ni jambo la kawaida duniani kwa kusisitiza kwamba:- Kisha MM anaendelea:-
Lakini pia kuna mfumo mwingine wa usalama na ulinzi; mfumo ambao unafanya kazi nje ya sheria, taratibu na amri zinazoelweka.
Hapa anajaribu kushawishi watu waamini kwamba this's not about JPM's Brutality Administration bali ni suala linalotokea hata kwa mataifa ya kidemokrasia! Na huo sio udhalimu bali ni sehemu tu ya "Mifumo ya Ulinzi na Usalama" duniani kote!!!

Yaani Ben Saanane kupotezwa kwa sababu za kijinga kabisa, ni sehemu ya ulinzi na usalama! Yaani Azory Gwanda ku-disappear and ku-die (according to Kabudi) akitekeleza majukumu yake, nalo ni sehemu ya ulinzi na usalama unaofanyika duniani kote! Yaani hata "vijitu vidogo" kama ROMA Mkatoliki kutekwa na kufanyiwa yale ambayo hadi kesho anashindwa kusema, nalo MM anataka kutushawishi ni sehemu ya ulinzi na usalama! Yaani Mo Kutekwa na siku tatu baadae maafisa polisi wanajumuika nyumbani kwake kunywa chai ya maziwa na bagia, nalo ni sehemu ya ulinzi na usalama unaofanyika duniani kote!

Lakini kama hiyo haitoshi, anaendelea kusisitiza jambo lile lile kwa kusema:- Yaani sio vitendo vya kihalifu bali VINGEITWA vya kihalifu, na kwamba kila mahali vitendo hivi ambavyo "vinaweza kuitwa vya kihalifu" vipo, kwahiyo tusimsakame JPM!!

Utamu zaidi, hapa:- Kutaka kuficha dhamira yake, anawataja madhalimu ya Kikaburu kufanya uhuni huu lakini hatimae anapulizia kwa kusema "sio madhalimu ya kikaburu tu, bali hata sisi wenyewe tuliokuwa mstari wa mbele kufanya udhalimu nasi tulitumia mfumo huu!!!

Kisha MM anataka mifano kadhaa kuhalalisha hoja yake kwamba udhalimu huu unafanyika kila pahala duniani, kwa mfano:-
Kashfa ya Watergate – Marekani

Kati ya mwaka 1972 na 1974 huko Marekani kulitokea kashfa kubwa ambayo iliishia kwa kujiuzulu kwa Rais wa nchi hiyo Bw. Richard Nixon.
Aidha,
Maafisa 69 wa Serikali ya Nixon walikamatwa na kushtakiwa; 48 kati yao walikutwa na hatia na kati yao wapo waliopata vifungo jela, kupigwa faini na wengi kupoteza kazi zao.
Mfano mwingine ni:- Hata kama MM anajaribu kuonesha haya ni ya kawaida tu manake duniani kote yanatokea, amesahau huko duniani issues kama hizi zinakuwa handled vipi!

Richard Nixon badala ya kuwasaka na kuwashughulikia kwa risasi za moto waliovujisha Watergate Scandal, yeye aliamuakujihudhuru, na wengine wote walishughulikiwa kwa mujibu wa sheria!

Hata ilipokuja suala la Iran-Contra, bado wahusika hawakushughilikiwa kimya kimya, bali legal channels zilifuata mkondo wake! Tena basi, hakuna hata moja kati ya hayo unayoweza kuyalinganisha na udhalimu unaotokea Tanzania, kwahiyo hoja ya MM kwamba haya yanatokea popote duniani, ni baseless argument! NI baseless argument kwa sababu kinacholalamikiwa Tanzania ni raia kutishwa, na wengine kupotezwa kama sio kuuawa! Ni taifa la kidhalimu ndilo linaweza kufanya ushenzi kama huo!

Sasa tofauti ya mataifa yanayofuata demokrasi na yale ya kidhalimu inakuja hapa (mfano mwingine wa MNM):- Kisha tena:- - Lakini MM amesahau (kwa makusudi) mifano mingine ya MNM, BBC wanatukumbusha:-
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amepigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma, katikati mwa Tanzania

Halafu huu hapa:-
The Minister revealed Gwanda’s fate during a BBC interview aired on 10 July, saying; "The state is dealing with all those who have unfortunately died and disappeared in Rufiji... it was very painful for someone who was doing his job to pass on".
Source Amnesty International. Mtandao wa All Africa nao unatujuza
Dar es Salaam — The mystery surrounding the seven bodies that were fished out of Ruvu River and disappearance of Chadema official Ben Saanane is yet to be resolved as the Police Force says it is still investigating both incidents.

Sasa ukisoma yaliyotokea Marekani na jinsi yalivyoshugulikiwa, utaona kuna tofauti kubwa na jinsi the so called MNM ilivyofanya kazi kwa Saudi Arabia, Israel na Tanzania, ambazo zote ni nchi za kidhalimu!

Unajua sana kuuma na kupulizia but I don't buy it! I don't buy it kwa sababu hoja iliyopo mezani ni kwamba Jiwe kwa kutumia watu anamtumia Cyprian Musiba kukashifu na kuwachafua watu wanaoukosoa utawala! Hiyo sio MNM bali ni kikosi tu cha wahuni kinachopata back up ya watawala ili waendeleze uhuni wao kwa maslahi binafsi! NI mataifa ya kifedhuli kama Saudi Arabia na Tanzania ndio yanafanya uhuni dhidi ya raia wake wanaoikosoa serikali!

Hata hiyo Israel pamoja na ufedhuli wake wote, ilifanya huo umafia dhidi ya magaidi ambao waliwaua raia wa Israel!
 
Kinachoangushaga mbinu hizi ni Murphy's Law inayosema 'Anything that can go wrong, will go wrong' au kwa tafsiri ya haraka 'Lolote linaloweza kwenda kombo litafanya hivyo'.

Mkuu Mzee Mwanakijiji na sisi Tanzania tuna mifano ya mbinu chafu ambazo zilienda kombo, naomba upate ujasiri wa kutumia mifano hiyo.

Na kama CCM wanafanya drama zao ili kupanga mpango mwingine mchafu, mipango yao itaenda kombo TENA.
 
Mbona hapa kwetu MNM wamejaa wajinga sana. Mission zao huwa ni za kijinga, hazilindi maslahi mapana ya taifa, zinaleta mifarakano zaidi katika jamii. Sana sana zinaleta hofu, ambayo sasa wababe wamshaanza kujitokeza kuikabili.
 
Juzi ulipoleta ile mada nyingine ya kina Kinana uliweka hiyo MNM, watu walipokuuliza ukaahidi kutuletea mada ya hiyo MNM. Sasa baada ya kuisoma mada hii yote najiuliza, kuna uhusiano gani kati ya MNM na ile mada yako ya akina Musiba na Kinana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…