Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF ichunguzwe

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
18,349
14,556
Wadau,

Naleta hii mada kwenu ili muweze kuchangia maoni yenu hasa tulio wanachama wa mifuko hii kwa wizi, udhalimu na manyanyaso ya mifuko hii hasa matumizi maovu ya pesa zetu wanachama.

Kwa miaka mingi tumeona namna mifuko hii inavyotumia mabilioni ya fedha za wanachama kuwekeza katika miradi mingi ya majengo, barabara na madaraja, miradi ambayo haina faida hata chembe kwa mwanachama wa mifuko hii na wala haimwongezei chochote katika stahiki zake.

Ukweli wa hili hawa wakuu wa Taasisi hiki wanachofaidika nacho wao binafsi ni mgao (10%) wanazopata toka kwa wakandarasi wa tender hizo ndio maana wanakimbilia hata miradi ya hasara!

Kibaya zaidi wafanyakazi wa mifuko hii wanaishi kama wako Ahera kwa namna wanavyogeuka Mchwa kutafuna fedha za wanachama huku wakijitengenezea package nzuri mno kwa maslahi yao huku wanachama wakilipwa fedha kigogo mno anapostaafu tofauti na wao ambao huruka na fedha za kufa mtu wanapostaafu!

Tulitarajia Regulator wa mifuko hii angekuwa kwa mkombozi kwa maelfu ya wanachama lakini kwa wenye akili tulipoona mkurugenzi alikuwa ni mfanyakazi wa PPF tukajua hapa ni 'Funika kombe mwanaharamu apite.

Tunamuomba Rais wetu Magufuli aigeukie mifuko ili atumbue majipu kwani kuna unyonyaji, dhulumati, ujambazi, uonevu, uovu na ukandamizaji wa mifuko hii.
 
kwa kweli hawa ni majipu kuliko kumchukuwa Dau kumpeleka ubalozi ni bora ubadilishe mifumo ya mahesabu katika vyombo hivi hasa lile fungu la mwisho unalopewa. yaani mshahara wako wa mwisho kwa miaka mitano kwanini isiwe kwa idadi ya miaka uliyofanya kazi kama serikali kuu.Tuelewesheni jamani nini kigumu
 
Usemalo lina chembe chembe zenye uhai wa ukweli mwingi,Mfumo uliokuwapo kabla kabla ya mageuzi yanayofanywa na Serikari mpya ya JPM ulikuwa mfumo unaobariki uozo,uvundo na uchafu mwingi.

Kandarasi nyingi zimetolewa kwa undugu,ujamaa,urafiki na kufanya miradi kuwa ghari mnooo hivyo ku affect their economic viability...

Mfano:Bei ya nyumba zinazoitwa za bei nafuu na kwa ajili ya wastaafu kuuzwa Tsh 150;250;350 milioni huku wengi wa wastaafu walengwa wakilipwa viinua mgongo vya milioni 30;40;50;60 n.k..Haiingii akilini kwa kweli
 
Back
Top Bottom