kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Takwimu zinaonyesha kuwa Umri wa kuishi wa mtanzania umeshuka hadi kufikia miaka 54 tu, lakini mifukuko ya yakijamii (NSSF, GEPF, PPF, LAPF, etc) imeamua kumlipa mstaafu kwa mkupuo hela kidogo sana (25% tu ya hela yake aliyojikusanyia kwa miaka yote 30-40 ya kufanyakazi) huku wao wakibaki na 75% ya hela zake kwenye mikwiji yao kwa kisingizio eti cha kutaka kumlipa mstaafu malipo makubwa ya kila mwezi hadi kufa kwake huku wakifahamu wazi kuwa wastaafu wengi (80%) huwa wanakufa ndani ya miaka 5 tu baada ya kustaafu. Mstaafu akishakufa wao wanabaki na mihela yoote iliyobaki. Hii ni dhuluma mpya ya waziwazi. Yaani kama mafao yako ni mil. 100,000,000 wao watakulipa kwa mkupuo sh. 25,000,000 tu, halafu wao wanabaki na sh.75,000,000 zako ili wao wakulipe kidogokidogo (let say sh.500,000 ) kila mwezi, lakini kama bahati mbaya utakufa hata baada ya miaka 2 baadaye hela zako zooote hizo zitapotea.
Hii sio sawa.
Hii sio sawa.