Mifugo iliyokamatwa ndani ya Ranchi ya Misenyi kupigwa mnada

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,536
Mkuu wa wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera, Festo Kiswaga, amewapa siku 14 wafugaji ambao mifugo yao ilikamatwa kwenye Ranchi ya Taifa ya Misenyi kuhakikisha wanalipia faini mifugo yao kabla ya kupigwa mnada.

Katika kikao cha pamoja cha Kamati ya Ulinzi na Usalama hiyo wilaya hiyo na wafugaji amesema kuwa muda mrefu umepita tangu mifugo hiyo ilipokamatwa.Mkuu wa wilaya huyo amewataka hata wafugaji kutoka nje ya nchi ambao ni wamiliki wa baadhi ya mifugo hiyo wafike kulipia mifugo yao kabla hawajaipiga mnada.

Wafugaji hao wamewalalamikia walinzi waliopewa jukumu hilo kwa kukithiri vitendo vya rushwa na kusema wengine wametajirika kutokana na kukamata mifugo na kuomba rushwa ili kuiruhusu. Wamesema wanashangazwa na hatua hiyo ya kutaka kuuzwa kwa mifugo yao ambapo wengine wamesema kuwa walishatoa faini kwa mara ya kwanza lakini faini wanayotakiwa kulipa kwa mara ya pili hawaitambui.
 
Back
Top Bottom