Miezi 4 tangu kuanza kutumika Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi: Kamishna wa Mamlaka hiyo hajulikani wala Ofisi zake zilipo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
IMG_20230913_175731_313.jpg

Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika kupitia Programu shirikishi ya “AU-EU D4D Hub Project” umefungua mafunzo shirikishi ya watekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Mpango huu ambao unategemewa kuwa endelevu umeanza Leo Septemba 13, 2023 na utaendelea hadi Septemba 14, 2023 ukiwa una nia ya kuwakutanisha makamishna na watekelezaji wa Sheria hizi na kutoa mafunzo ikijumuisha kubadilishana ujuzi na mbinu mbalimbali za kusimamia na kutekeleza Sheria za Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Na Kwa mara ya kwanza, mafunzo hayo yanafanyika nchini Kenya ambapo Makamishna wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kutoka Kenya, Uganda na Tanzania wamekutana.

Zaidi ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika, programu hii inasimamiwa na kupata uungwaji mkono kutoka kwa Wadau mbalimbali Kama vile, the Smart Africa Secretariat, the East African Community ICT Secretariat and the East Africa Communications Organisation.

Hali ilivyo Tanzania
Wakati mafunzo haya yakiendelea, kumekuwa na sintofahamu juu ya nani na wapi alipo Kamishna wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Tanzania.

Ikiwa Sheria hii imeanza kufanya kazi Mwezi Mei mwaka huu, bado Umma haujafahamishwa zilipo Ofisi za Kamishna wala Kamishna mteule ni nani.

Hii inaleta ugumu kwa wananchi katika kuripoti uvunjaji au kufuatilia Utekelezaji wa Sheria hii kwakuwa haijulikani wapi na nani mwenye mamlaka ya kusimamia Sheria hii yenye kutarajiwa kulinda utu wa mtanzania.
 
Back
Top Bottom