Miembeni Z'bar & Ali Bushiri, "Jela" Miaka Mitano.

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Shirikisho la kabumbu la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeifungia kwa miaka mitano timu ya Miembeni ya Zanzibar na kocha wake Ali Bushiri, kwa kitendo cha kugomea kuendelea na mchezo kati yake na timu ya Heg Al Arab.
Sambamaba na adhabu hiyo ya kifungo, klabu hiyo imekumbana na fani nzito ya dola 20,000.
Miembeni ni wawakilishi wa zanzibar katika michuano hiyo ya vilabu bingwa vya Afrika Mashariki na Kati inayoendelea nchini Sudan.
 
Last edited:
Walitaka kuleta ubishi wa kipemba nini katika kabumbu la kimataifa?
 
kimenishangaza huyu Ali Bushiri kawa kifuu tundu kama hivi.
Kawa kama mun'gunye anaharibika ukubwani, anamtia aibu Maximo.
 
Karne hii bado watu wanagoma kucheza tena kwenye mashindano ya kimataifa? Hii kali ya mwaka!!
 
Back
Top Bottom