Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,174
Msema ukweli kipenzi cha Muumba hivyo sikani!
Ya kuwa mie nawe tulikuwa beneti sana tena sana!
Nakumbuka tulivyokutanishwa na aliyetutambulisha!
Unyenyekevu wako ulinikoga na Kiswahili kuniyeyuka!
Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!
Haba haba hujaza kibaba na penzi la kasi tulilifukizia
Hapa na pale tukajikuta tumo ndani ya lindi la mahaba
Bila ya kutarajia tukajikuta kitanda twalala sote bila mbinde
Huko tulinogewa na hata kusahau kuwekana sawa ya kesho

Kesho na kesho kutwa tuliiweka kapuni bila kukusudia
Bila ya kuipangilia mie nilijionea sawa na hata wewe vivyo
Hapa na pale mjuaji akaja na kutumbukia mawazoni mwangu
Kauli yake ilinitikisa na kesho yetu tukaipangilia bila zengwe!

Kosa langu nielimishe hadi sasa kuniita mdanganyifu.
Hakuna ahadi niliyokupa au hata wewe kunipatia pia
Yawaje sasa udai umetapeliwa khali hatuna makubaliano?
Manung'uniko yako yamenifikia lakini mwenzio kakuwahi!

Mengi unazoza lakini yote ni tisa tu hakuna jawabu.
Kama ungelikuwa makini ungelinitonya juu ya kesho yetu.
Mie nilidhani tunapita tu na hivyo sikukutilia maanani
Mbona mwenzio aling'aka na kutaka ajue yatakayomsibu?