Michezo ya Jackpot ni ujinga

ankai

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
3,280
4,236
Yaaani vituo vya radio vinawahamasisha wajinga 100k wanachanga ml 100 kwa kupitia kile wanachokiita eti cheza ushinde ama mchongo pesa kwa kuwambia wacheze huo mchezo kwa gharama ya sh 1000.

Halafu baada ya kituo cha radio kukusanya ml100 kutoka kwa wajinga au mabwege 100k wanamchagua mjinga mmoja labda aliyecheza mara nyingi zaidi na kumpa ml 1.

Halafu wao kituo cha radio kinabaki na ml99 hii ni kwa mchezo mmoja let say hii ni ndani ya kipindi kimoja tu chenye lisaa limoja tu hewani.

Halafu baada ya hapo wanampigia simu na kumpongeza kwa ujinga na uzuzu wake alafu wanamuuliza je unawashauri nini wale wanaotaka kukata tamaa ya kucheza?

Lile zuzu utaskia linasema nawashauri wasikate tamaa waendelee kucheza mara nyingi maana mimi mwenye nimecheza zaidi ya mara 300 daaah unajiuliza hivi ni akili au matope kiukweli kwa akili hizi daah raia wa Tanzania wataendelea kupigwa na kuibiwa mpaka mwisho wa dunia hii kama utakuwepo lakini.

Usalama wa taifa wapo, polisi wapo. Ustawi wa jamii wapo, Rais wa nchi yupo watunga sera wa nchi wapo na vyombo vyooote vya ulinzi na usalama dhidi ya raia vipo.
 
Ajabu na kweli asee tz ni taifa la mazuzu na mabwege
 
Nakubali kiongozi yaani watu hawajui kama kuna muswada wa BIMA ya afya Yao lakini wapo vizuri kujadili mayele na phiri ,Joni anakuja nisaidie shilingi 5000 nikanunue fungu la dagaa
 
We kweli hesabu zime kupita kushoto.
Buku,buku kwa watu elfu moja ni sawa ma Milion 1 tu...!
Usije ma muhemko kwa hesabu za lasaba afu zimekushinda.

Alafu kucheza sio lazima na wala hulazimishwi kama wale Ma boya wa Kylinda
 
Nakubali kiongozi yaani watu hawajui kama kuna muswada wa BIMA ya afya Yao lakini wapo vizuri kujadili mayele na phiri ,Joni anakuja nisaidie shilingi 5000 nikanunue fungu la dagaa
Mbona upo nje ya mada? Ulaya kwenyewe halaand yupo midomoni mwa watu..sisi ni nani mpaka tusiwafurahie akina mayele na phiri?
 
UWEPO WA WAJINGA, NI MTAJI TOSHA.
CCM MIAKA YOTE INASHINDA KWA SABABU YA MAZUZU
 
Yaaani vituo vya radio vinawahamasisha wajinga 1000 wanachanga ml 100 kwa kupitia kile wanachokiita eti cheza ushinde ama mchongo pesa kwa kuwambia wacheze huo mchezo kwa gharama ya sh 1000.

Halafu baada ya kituo cha radio kukusanya ml100 kutoka kwa wajinga au mabwege 1000 wanamchagua mjinga mmoja labda aliyecheza mara nyingi zaidi na kumpa ml 1.

Halafu wao kituo cha radio kinabaki na ml99 hii ni kwa mchezo mmoja let say hii ni ndani ya kipindi kimoja tu chenye lisaa limoja tu hewani.

Halafu baada ya hapo wanampigia simu na kumpongeza kwa ujinga na uzuzu wake alafu wanamuuliza je unawashauri nini wale wanaotaka kukata tamaa ya kucheza?

Lile zuzu utaskia linasema nawashauri wasikate tamaa waendelee kucheza mara nyingi maana mimi mwenye nimecheza zaidi ya mara 300 daaah unajiuliza hivi ni akili au matope kiukweli kwa akili hizi daah raia wa Tanzania wataendelea kupigwa na kuibiwa mpaka mwisho wa dunia hii kama utakuwepo lakini.

Usalama wa taifa wapo, polisi wapo. Ustawi wa jamii wapo, Rais wa nchi yupo watunga sera wa nchi wapo na vyombo vyooote vya ulinzi na usalama dhidi ya raia vipo.
1000x1000 ni 1,000,000 sio 100mil

Alafu iyo michezo ni utapeli kwa 100%.

Wanasajiliwa na kulipa kodi ndo mana mamlaka hazifanyi lolote... kikubwa ni watanzania kustuka na kuacha kucheza mbona watazikimbia tu biashara zao
 
Back
Top Bottom