Real, Barca ni vita ya historia Send to a friend Saturday, 16 April 2011 09:08
MADRID, Hispania
UHASAMA baina ya Barcelona na Real Madrid ulianza mwaka 1902, na sasa watakutana mara nne katika siku18 za msimu wa kipekee.
Mashabiki wa soka duniani watakuwa wakisubili vita hiyo ya pekee ya 'El Clasico', kila moja akisema lake juu ya klabu hizo mbili tajiri na zenye mafanikio zaidi katika soka ya Hispania zitakapombana kwenye Ligi, Kombe la Mfalme na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Kila klabu na jiji zinamalengo tofauti kabisa, huku Madrid wanalengo la kutunza heshima ya Hispania, huku Barcelona wanataka kutambulika wenye kama nchi ya Catalan, si Spanish, ambayo ndiyo lugha yao.
Kihistoria, Real inamafanikio zaidi kati ya timu hizo mbili, ikiwa imetwaa mataji tisa ya Kombe la Ulaya, huku Barcelona ikiwa imetwaa mataji matatu, ubingwa wa ligi Madrid imetwaa mataji 31, huku Barcelona mataji 20.
Vijana hao wa Catalans kwa misimu ya sasa ndio wanatawala, huku soka yao ya kuvutia imewawezesha kutwaa ubingwa ligi mara mbili na mwaka 2009 walitwaa taji la Ligi ya Mabingwa.
Mchezo wa kwanza wa Clasico atafanyika leo ikiwa ni mechi ya ligi itayochezwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu. Barcelona inaongoza ligi kwa pointi nane mbele ya Real, pia wanapewa nafadi kubwa ya kushinda mechi zote tatu na kutwaa ubingwa.
Baada ya kupokea kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Barcelona kwenye mchezo wa kwanza wa ligi wa Clasico kwenye Uwanja wa Camp Nou pale Novemba, hiyo inamaanisha Real watalazimika kulipiza kisasi katika mchezo huo.Ni kipigo cha kwanza kikubwa kwa Jose Mourinho kwenye maisha yake ya ukocha, pia ulikuwa mchezo wake wa kwa kwanza wa Clasico na endapo atafungwa tena leo basi ndoto yake ya ubingwa itakuwa imekwisha ikiwa imebaki michezo saba.
Mourinho, ambaye alikuwa mkarimani ndani ya Barcelona, haamini kwamba matokeo yao ya mechi ya kwanza yanaweza kuwaathiri kwenye mechi hizi tatu. "Tunauchukua kila mchezo kwa namna ya pekee," alisema Mourinho.
"Sifikiri kwamba matokeo yaliyotokea kwenye mchezo wa kwanza yanaweza kujirudia kwenye mchezo wa pili, watatu au wanne."
Kocha wa Barcelona, Pep Guardiola ameipokea ratiba hiyo kwa mikono miwili huku akiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 5-0."Hatojarisha tupo kwenye mazingira gani.Jambo la msingi ni kuwa tayari kiakili na hamu ya kufanya vizuri," alisema Guardiola. "Hii ni zawadi ambayo mtu yeyote wa mpira angependa kuipokea."
Real haijaifunga Barcelona tangu Mei 2008 waliposhinda 4-1 katika ligi kwenye Uwanja wa Bernabeu wakati kikosi bora cha Barcelona kilivyopoteza ubingwa kwa uchungu kwa mahasimu wao Real.
Mchezo huo wa ligi utafutiwa na ule wa kombe la Mfalme siku nne baadaye hapo Aprili 20 mjini Valencia kwenye Uwanja wa Mestalla, huku Mourinho akiwaza kupata taji lake la kwanza kama kocha wa Madrid.
Jambo la kufurahisha ni kuwa, Barcelona na Real hazijakuna kwenye fainali ya kombe hilo tangu mwaka 1990 wakati Barcelona iliposhinda 2-0.
Mechi ya mwisho baina yao ni ile ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ambayo mchezo wa kwanza utaanzia Bernabeu hapo Aprili 27 na marudiano Camp Nou hapo Mei 3.