Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Ruvu Shooting kuwahi kuingia kambini

Na Addolph Bruno

KLABU ya soka ya Ruvu Shooting imesema wachezaji wake wakimaliza likizo fupi waliyopewa wataanza mazoezi mara moja, kujiwinda na Ligi Kuu Bara msimu ujao
ili kujenga mazingira ya kufanya vyema.

Ruvu Shooting ni miongoni mwa timu zilizoponea chupuchupu kushuka daraja msimu huu, ikiwa imemaliza ligi nafasi ya tatu kutoka mwisho.

Akizungumza kwa simu jana akiwa Kibaha, Msemaji wa klabu hiyo, masau Bwire alisema watalazimika kufanya hivyo kuandaa ili mazingira mapema kufanya vizuri zaidi msimu ujao kutokana na nafasi hiyo.

"Timu nzima kwa maana ya makocha, wachezaji kwa sasa wapo wapo likizo fupi na wakirejea, mpango utakaofuata ni kufanya majumuisho na mambo mengine ya usajili na baada ya hapo ni kambi na mazoezi moja kwa moja.

"Ligi ya msimu huu ilikuwa ngumu mno, ushindani uliongezeka zaidi bila shaka kila timu sasa inajiandaa kutokana na changamoto iliyopata, sisi tunaanza kupanga timu yenye nguvu kwanza," alisema Bwire.

Alisema wanaamini kambi na mazoezi ya mapema yatawawezesha wachezaji wao wasibweteke na kuongeza kuwa wanaamini itawezekana kutokana wachezaji wao wengi kuwa wanajeshi.
 
Yanga wazikataa sh40 za Azam Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 21:13

Calvin Kiwia
UONGOZI wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam umezikataa sh40milioni zilizotengwa na Azam kwa ajili ya kumnasa kiungo wake, Nurdin Bakari.

Jumatatu iliyopita, Nurdin alitangaza kuwa yuko huru baada ya kumalizika mkataba wake wa kuitumikia Yanga na kwa alikuwa tayari kujiunga na klabu yoyote itakayokuwa tayari kumpatia fedha atakazokuwa akizihitaji.

Nurdin alisema kuwa ana mambo mengi anahitaji kuyafanyia kazi, hivyo fedha atakazopatiwa, yuko tayari kuitumikia klabu itakayokidhi haja zake. "Mimi nafanya mpira kama kazi, sichezi mpira wa sifa, kama kuna timu inataka kunipa mkataba tukakubaliana niko tayari," alikaririwa Nurdin.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga, Seif Ahmed alisema kuwa tayari wamemsainisha kiungo huyo mahiri aliyeifungia Yanga mabao mawili kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya Toto African.

"Nurdin alikuwa tayari amemaliza mkataba wake na klabu yetu na alitufuata kutaka kujua hatma yake kwamba tutamwongezea ama aondoke kwenda klabu nyingine zilizokuwa tayari zimeonyesha nia ya kumsainisha kwa lengo la kuzichezea kwa msimu ujao wa ligi," alisema Seif.

"Hivyo ikatulazimu kumfuata mwalimu wetu Sam Timbe kujua kwamba bado anamwitaji kiungo huyo kwenye kikosi chake cha msimu ujao na kutujibu anamwitaji sana na kuchukua uamuzi huo wa kumuongezea mkataba wa miaka miwili kuichezea tena klabu yetu," aliongeza.

Alisema walimwongezea mkataba huo mapema kuhofia kiungo huyo kujiunga na klabu ya Azam iliyokuwa ikimtolea macho kutaka saini yake kwa kiasi cha Sh. 40 mil, hivyo kuzima ndoto hizo za kumwania kiungo huyo aliyejiunga na timu hiyo akitokea kwa mahasimu wao wakubwa wa jadi Simba.

"Hatuwezi kutaja hadharani kuwa tumemsainisha kwa kiasi cha shilingi ngapi bali ni siri yetu ya klabu na yeye mchezaji mwenyewe," alisisitiza.

Hata hivyo, taarifa za kina kutoka kwa rafiki wa karibu wa Nurdin Bakari aliyekataa kutajwa jina lake kwenye gazeti hili alikiri kuwa kiungo huyo amesaini mkataba huo kwa kiasi ambacho Azam waliokuwa wamemuahidi kumpatia, cha sh40milioni.

Juhudi zilizofanywa za kumpata Nurdin Bakari kuzungumzia ukweli wa suala hili uligonga mwamba pale simu yake ilipokuwa ikiita bila ya kupokelewa na muhusika na hata baadae kuzimwa kabisa.

Wakati huo huo, kuna tetesi kuwa baada ya kumkosa Nurdin, uongozi wa timu hiyo umeanza mikakati ya kumleta kundini, beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kwa nia ya kupata saini yake kujiunga na klabu hiyo kwa msimu ujao kutokana na kocha Stewart Hall kumhusudu beki huyo na lengo lake ni kumuunganisha na Aggrey Morris kama ilivyo kwa timu ya Taifa Stars na Zanzibar Heroes.

Wakati huo huo kamati hiyo ya usajili imesema kuwa haitafanya usajili wa mchezaji yeyote yule bila kupata mapendekezo kutoka kwa mwalimu wao mkuu Sam Timbe. Yanga itaiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
 
Timu 6 zatinga fainali Shinyanga

Imeandikwa na Na Shangwe Thani, Shinyanga; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 31; Jumla ya maoni: 0

TIMU sita kati ya 12 zilizoshiriki duru la pili la michuano ya ligi ya taifa ngazi ya mkoa wa
Shinyanga, zimefuzu hatua ya fainali ya ligi hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi ijayo katika uwanja wa Kambarage mjini hapa.

Timu zilizosonga mbele hatua hiyo kutoka kituo cha Segese ni Timbaland ya Kahama na
Leopard ya Segese, kutoka kituo cha Mwadui ni Mwadui FC na Majengo FC na kutoka kituo cha
Usanda ni California ya Bariadi na Original ya Usanda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama cha soka mkoani hapa Jumatano, fainali itaanza
Jumamosi kwenye dimba la Kambarage kwa mchezo utakaozikutanisha California ya Bariadi na Timbaland ya Kahama.

Jumapili ni Original ya Usanda na Leopard ya Kahama na mzunguko wa kwanza utaanza
Jumatatu kwa mchezo kati ya timu za Msajengo FC na Mwadui FC na timu zote zimetakiwa kufika kwenye kituo cha mchezo siku moja kabla ya mchezo.

Ligi hiyo hatua ya kwanza ilishirikisha timu 24 kutoka wilaya nane za mkoa wa Shinyanga na mzunguko wa pili ulishirikisha timu 12 zilizocheza kwenye vituo vitatu vya Segese, Mwadui na Usanda.

Timu zilizotupwa nje ya michuano hiyo katika mzunguko wa pili kutoka kituo cha Segese
ni Vijana Segese na Cobra ya Masumbwe, kituo cha Mwadui ni vijana ya Maswa na Lamadi
FC na kituo cha Usanda ni Nguzonane FC na Shinyanga United.

Hatua hiyo ya mwisho ni ya kutafuta bingwa wa mkoa na mwakilishi wa mkoa katika
michuano ya ligi ya kanda.
 
Serengeti yatoa milioni 80/- Tuzo za Taswa

Imeandikwa na Na Evance Ng'ingo; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 37; Jumla ya maoni: 0

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imetangaza kutoa Sh milioni 80 kwa ajili ya kudhamini Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2010 zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa).

Pia hoteli ya Movenpick ya Dar es Salaam nayo itakuwa mdhamini mshiriki wa tuzo hizo zitakazofanyika Mei 6, 2011 kwenye ukumbi wa hoteli, ambapo zaidi ya vyama 15 vya michezo wanamichezo wake watazawadiwa.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari, Jumatano kuwa wana matumaini makubwa tuzo za mwaka huu zitakuwa za aina yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto akizungumza kwenye mkutano huo aliishukuru Serengeti na kusema kuwa udhamini huo ni wa kupigiwa mfano.

Alisema bajeti yao kwa tuzo ya mwaka 2011 ni Sh milioni 160, ambapo Serengeti imeshachukua nusu ya gharama hizo, wakati kampuni nyingine zitasaidia kwa nusu iliyobaki.

"Naamini udhamini huu ambao ni wa kwanza mkubwa na wa aina yake katika historia ya tuzo za TASWA, utaleta yale mabadiliko ya kweli ambayo TASWA iliahidi kuhusiana na tuzo hizi.

"Ushahidi wa jitihada za kuboresha tuzo ulianza mwezi mmoja uliopita, wakati Kamati ya Utendaji ya TASWA ilipoamua kuunda Kamati Maalum kushughulikia tuzo, ambayo hivi sasa inaendelea na mchakato wa kutupatia wanamichezo ambao tutawazawadia Mei 6, mwaka huu.

"Lakini ushahidi mwingine ni leo hii, siku ya kihistoria ya kutangaza udhamini wetu, nawashukuru sana SBL na wameonesha kweli wao ni marafiki wa waandishi wa habari na pia ni marafiki wa wanamichezo wa Tanzania," alisema Pinto.

Alisema tuzo za mwaka huu Serengeti ndiyo mdhamini mkuu, ambapo Movenpick Hotel na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) watakuwa wadhamini washiriki na kwamba wadhamini wengine wanaendelea kutafutwa.

Naye Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando alisema tuzo za mwaka 2011 watazawadia
wanamichezo bora kwa kila mchezo na kwamba tayari mchakato wa jambo hilo unaendelea.

Wanamichezo Bora kwa miaka ya hivi karibuni na miaka yao kwenye mabano ni wanariadha Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle (2007) na Mary Naali (2008), wakati mwaka 2009 alikuwa mcheza netiboli Mwanaidi Hassan.
 
TASWA yapigwa 'tafu' sh80milioni Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 21:12

Sosthenes Nyoni
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imekabidhi hundi ya Sh 80 milioni kwa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) ikiwa ni udhamini wake kwaajili ya kufanikisha sherehe za tuzo za wanamichezo bora ambazo zimepangwa kufanyika Mei 6 kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.

Hafla ya makabidhiano ya hundi hiyo ilifanyika jana kwenye hoteli ya Movempick na kuhudhuriwa na wawakili kutoka Taswa na SBL.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda alisema kuwa kampuni yake imekudhamini sherehe hizo kutokana na kutambua mchango wa waandishi katika maendeleo ya michezo na sekta nyingine.

"SBL kwa moyo mkunjufu leo inakabidhi hundi hii kama mdhamini mkuu katika kufanikisha sherehe za tuzo za wanamichezo bora, mchango wa waandishi ni mkubwa na sisi tunautambua, ahadi yetu ni kwamba tutaendelea kushirikiana ili kufanikisha tukio hilo,"alisema Maounda.

Akipokea hundi hiyo, Mwenyekiti wa Taswa, Juma Pinto alisema kuwa udhamini wa SBL umerejesha heshima ya tuzo hizo tofauti na awali .Alisema kuwa licha ya fedha hizo kuwa ni nusu ya bajeti yao zitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha tukio hilo.

"Licha ya kwamba hizi milioni 80 ni nusu ya bajeti yetu ambayo ni Sh 160 milioni ukweli ni kwamba zitasaidia sana kufanikisha tukio hilo kwakushirikiana na wadhamini wengine,"alisema Pinto.

Kwa mujibu wa Pinto tuzo za safari hii zitakuwa tofauti kidogo na nyingine zilizotangulia ambapo watachaguliwa wanamichezo bora wa miezi kutoka michezo tofauti kabla ya kumpata mwanamichezo bora wa mwaka atakayewakilisha michezo yote.
 
Five Stars mbioni kuibuka upya

Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 82; Jumla ya maoni: 0

KUNDI la Jahazi Modern Taarab la jijini, Dar es Salaam ambalo hivi karibuni lilipoteza wanamuziki 13 kwa ajali ya gari limesema halijafa ingawa kwa sasa limesimamisha shughuli zote za burudani hadi baada ya hitma ya kuwaombea wenzao waliofariki.

Hitma hiyo imepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa PTA Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu
Nyerere, Dar es Salaam Jumapili wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Jumatano, Mwenyekiti wa Five Stars, Hamis Slim, alisema uongozi wake umesimamisha shughuli zote za burudani za bendi kwa kipindi hiki hadi watakapomaliza hitma ya wapendwa wao.

Alisema katika kuhakikisha hilo linafanikiwa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu aliteuliwa
kuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ambayo wajumbe wake wapo baadhi ya wabunge na viongozi wa bendi za muziki.

Wanamuziki hao walifariki kutokana na ajali iliyotokea Mikumi Machi 22 wakitokea kwenye ziara ya Kyela, Mbeya.

"Bendi haijafa ni baadhi ya wasanii hivyo, tutaendelea kuwepo na tutatoa ufafanuzi baadaye
kuhusu wasanii tunaotaka kuongeza kwenye kundi. "Katika ajali hiyo tulipoteza wanamuziki 13, hivyo tulikumbwa na majonzi mazito ambayo mpaka sasa bado yanaendelea kutesa
mioyo yetu," alisema na kusisitiza kuwa katika kipindi chote wamesimamisha shughuli zote za burudani za bendi kwa sababu wapo kwenye maombolezo.

Aliishukuru serikali na vyombo vya habari kwa kuwa pamoja na uongozi wake kwa kipindi chote. Aliongeza kuwa tamko rasmi la bendi hiyo litatolewa baada ya hitma hiyo ikiwa ni pamoja na shukrani na mipango ya baadaye. Slim pia alipuuza taarifa tofauti zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na ajali hiyo.
 
Azam waanza mikakati Ligi Kuu 2011/12 Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 21:11

Calvin Kiwia
JUHUDI za klabu ya Azam FC kusajili wachezaji 10 wapya kwa ajili ya kukiongezea kikosi chao nguvu na makali na kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao wa 2011/12 baada ya kumaliza msimu wa 2010/11 nafasi ya tatu zimeanza kutimia baada ya kuwasajili wachezaji saba kati ya hao 10 inaowahitaji katika nafasi tofauti.

Nafasi ambazo klabu hiyo ilitangaza kuongezea wachezaji wapya na kuhakikisha msimu ujao wa ligi inatwaa taji hilo na kutorudia makosa ya msimu huu uliomalizika Aprili 10 mwaka huu ni nafasi mbili za makipa, beki wa kushoto mmoja na wakati wawili, viungo wawili, winga wa kushoto na washambuliaji wawili.

Hata hivyo habari kutoka kwenye mtandao wa klabu hiyo tayari imewasajili makipa wawili, Mserbia aliyewahi kukipiga na klabu ya Yanga misimu miwili iliyopita Obren Circkovic na Mwadini Ally Mwadini wa timu ya taifa ya visiwani Zanzibar 'Zanzibar Heroes'.

Wengine kutoka timu hiyo ni beki wa kushoto , Waziri Salum Omary, winga wa kushoto, Khassim Mcha Khassim na viungo Abdulghany Gulan na Abdulhalim Humoud kutoka Simba waliobadilishana na klabu hiyo kwa kumpeleka Patrick Mafisango na Zahoro Pazi kutoka African Lyon.

Katika hatua nyingine, katibu mkuu wa klabu hiyo, Nassor Idrissa aliliambia Mwananchi jana jijini Dar es Salaam kuwa watafanya usajili kwa wachezaji wengine kutoka nje nchi ili kukiimarisha zaidi kikosi cha timu hiyo kila idara na kuwa tishio msimu ujao wa Ligi Kuu.

"Mikakati yetu iliyopo mbeleni ni kuhakikisha tunakuwa na kikosi imara na bora kabisa kwenye michuano hiyo ya Ligi Kuu msimu unaokuja na kutwaa taji hilo na kwenda kushiriki mashindano ya kimataifa, si kuishia tena nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo," alisema Idrissa.
 
Tamasha la kuomba amani Afrika Ijumaa Dar es Salaam

Imeandikwa na Na Evance Ng'ingo; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 53; Jumla ya maoni: 0

WAIMBAJI wa nyimbo za Injili, viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa huduma za maombi na waumini mbalimbali Ijumaa hii wanatarajia kuungana kwa pamoja kwenye tamasha la kuomba amani kwa bara la Afrika.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Jumatano na Mratibu wa tamasha hilo, Safari Paul
ilieleza kuwa tamasha hilo la maombi litafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa maombi hayo yatahudhuriwa na kwaya ya Aflewo kutoka nchini
Kenya.

"Maombi hayo yanalenga kuombea amani na kuondoa maovu mbalimbali yanayolikabili
bara la Afrika kama vile maradhi vita na kukosekana kwa utawala bora," ilisema taarifa hiyo.

Kulingana na taarifa hiyo hakuna kiingilio chochote na kwamba wananchi wanatakiwa kuhudhuria kwa wingi.
 
Kado ataka wenzake kujituma Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 21:10

Jessca Nangawe
NAHODHA wa timu ya vijana ambae pia ni kipa namba moja wa timu hiyo, Shaaban Kado amewataka wachezaji wenzake kushirikiana kwa umoja na kuongeza juhudi katika mchezo uliopo mbele yao dhidi ya Uganda keshokutwa wa kufuzu Michezo ya Afrika.

Timu hiyo ya vijana inataraji kuondoka kesho kwenda Uganda kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na msafara wa watu 30 katika mchezo wao utakaofanyika keshokutwa kwenye uwanja wa Namboole uliopo Kampala.

Kado aliiambia Mwananchi jana kuwa kwa sasa wana jukumu kubwa la kuiwakilisha vyema Tanzania katika mshindano makubwa na ushirikiano ndio silaha kubwa kwao ili kuweza kufika mbali na kufanikiwa kufuzu katika hatua ya mwisho ya michezo hiyo ya Olympick.

"Kikubwa kwanza tunawashukuru Watanzania wote kwa kuwa pamoja nasi na kutupa nguvu kushinda mchezo wetu na Cameroon, kwa sasa tunapaswa kuelekeza nguvu zetu katika michezo iliyopo mbele yetu," alisema Kado.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo alisema wamejinadaa vyema kukabiliana na Uganda na wachezaji wake wote wako katika hali nzuri kiufundi na ana matarajio makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo.
 
Vijana Stars kuivaa Nigeria

Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 218; Jumla ya maoni: 0

DROO ya raundi ya pili ya michuano ya soka kuwania kucheza michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwaka 2012 jijini London, Uingereza ilifanyika wiki hii ambapo timu ya taifa ya Tanzania ya vijana ya umri wa chini ya miaka 23 ‘Vijana Stars' imepangwa kukutana na Nigeria katika raundi hiyo.

Kulingana na droo hiyo iliyofanyika Jumatano jijini Cairo, Misri na kusimamiwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Hicham El Amrani na kuhudhuriwa na wawakilishi wa mataifa yanayoshiriki michuano hiyo pamoja na mwakilishi wa Fifa Gordon Savic, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Michuano ya Kombe la Dunia na michuano ya kufuzu michezo ya Olimpiki, Tanzania ambayo iliitoa Cameroon raundi iliyopita, imejikuta ikiangukia mikononi mwa Nigeria ambayo ni moja ya miamba ya soka Afrika.

Nigeria ndio walikuwa washindi wa medali ya dhahabu katika michezo ya mwaka 1996, wakati Sudan ambao nao waliwaondosha kwenye michuano hiyo Ghana wamepangiwa kuchuana na Misri katika raundi hiyo ya pili.

Ratiba hiyo iliyopatikana jana kwenye mtandao inaonesha kuwa Algeria itacheza na Zambia, wakati Morocco watakabiliana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo). Congo Brazzaville itaumana na mshindi wa mechi ya marudiano kati ya Ivory Coast na Liberia ambayo ilisogezwa mbele na sasa itafanyika Aprili 20 mjini Monrovia, huku Ivory ikiingia
katika mchezo huo ikiwa mbele kwa mabao 4-0 iliyopata katika mchezo wake wa awali.

Katika droo hiyo Gabon itakutana na Mali, huku Benin ikipangwa na Afrika Kusini, Tunisia na Senegal. Washindi wa mechi hizo watakutana raundi ya mwisho ya michuano hiyo ambayo mfumo wake bado haujatangazwa.

Mataifa matatu ya Afrika yatafuzu michezo hiyo ya Olimpiki ya London itakayofanyika mwakani na pia inaweza kupata nafasi ya nne endapo timu itakayoshika nafasi ya nne kwenye michuano hiyo ya kuwania kufuzu Olimpiki mwakani kwa upande wa Afrika itaibuka na ushindi itakapokutana na mshindi wa nne kwa upande wa mataifa ya Asia.

Mechi za kwanza za raundi hiyo ya pili zitafanyika kati ya Juni 3 na 5 wakati mechi za marudiano zitafanyika wiki mbili baadaye. Wakati huohuo, wachezaji wa Vijana Stars jana walizawadiwa Sh milioni 22 kutokana na kuitoa Cameroon katika mbio hizo Jumamosi kwa penalti 4-3.

Cameroon imepata kutwaa medali ya dhahabu mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2000 yaliyofanyika Sydney, Australia. Fedha hizo Sh milioni 12 zilitolewa na mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji na kiasi kingine kilitolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Fedha hizo zilikabidhiwa jana wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa maalumu kwa wachezaji hao hoteli ya New Africa, Dar es Salaam, ambapo Dewji aliwapongeza na kuwataka wasibweteke.

Hata hivyo katika kiasi cha fedha alichotoa Dewji, Sh milioni moja ni kwa kipa Shaaban Kado ambaye alifuta penalti na wachezaji wawili waliofunga mabao yaliyosababisha mshindi aamuliwe kwa penalti. Vijana ilishinda mabao 2-1 dakika za kawaida 90 za mchezo wa Jumamosi.
 
Azam yasaka washambuliaji

Imeandikwa na Na John Nditi, Morogoro; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 56; Jumla ya maoni: 0

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Azam, Stewart Hall, amesema tatizo la ushambuliaji ni miongoni mwa vikwazo vilivyochangia timu hiyo kushindwa kufanya vizuri msimu wa Ligi Kuu iliyomalizika Aprili 10, mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo anakusudia kuangalia zaidi safu ya ushambuliaji kwa kutoa mapendekezo ya kupatikana wachezaji watakaokuwa na uwezo mkubwa wa kufunga mabao.

Akizungumza mwishoni mwa wiki mjini hapa, kocha huyo alisema hakuridhishwa na safu yake ya ushambuliaji kwani ilikuwa inakosa mabao mengi ya wazi.

Hata hivyo pamoja na kasoro hizo, aliwasifu wachezaji kwa kuifikisha timu kwenye nafasi ya tatu, ambapo alisema jukumu lake kubwa ni kuiandaa upya timu hiyo ili msimu ujao wa Ligi Kuu iweze kuwa tishio zaidi na kuleta mafanikio ya timu.

Naye Mwenyekiti wa timu hiyo, Said Mohamed alisema, kwa upande wa uongozi utasubiri taarifa ya kocha na watakapoipata wataipitia kuona mapendekezo yaliyomo kwenye taarifa hiyo na baadaye kuifanyika kazi kikamilifu.
 
Tanzania yapanda kiwango Fifa

Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 65; Jumla ya maoni: 0

TANZANIA imepanda katika orodha ya viwango vya ubora wa soka duniani vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Kwa mujibu wa orodha ya Fifa ya viwango iliyotolewa Jumatano, Tanzania iliyokuwa ikishikia nafasi ya 121 katika orodha ya iliyopita sasa inashikilia nafasi ya 112.

Katika orodha hiyo mataifa yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda ndio inaongoza
ikiwa nafasi ya 84 ikifuatiwa na Tanzania ambayo imepanda nafasi tisa, Rwanda ambayo iko katika nafasi ya 123 na Kenya ni ya nne ikiwa nafasi ya 124, wakati Burundi inashika mkia ikiwa nafasi ya 148 katika orodha hiyo.

Wapinzani wa Tanzania katika michuano ya kuwania kufuzu kwenye michuano ya fainali
za Mataifa ya Afrika (CAN), ambao wamepangwa Kundi D pamoja na Tanzania, Algeria ndio iko juu kwenye orodha hiyo ikiwa nafasi ya 40, Morocco inashika nafasi ya 72 na Jamhuri ya Afrika ya Kati iko katika nafasi ya 114 ikishuka kwa nafasi mbili.

Msumbiji ambayo itavaana na Tanzania katika ufunguzi wa uwanja mpya wa michezo wa
kisasa wa taifa hilo baadaye mwezi huu, ipo nafasi ya 96 ikiwa imeshuka kwa nafasi tatu.

Kwa bara la Afrika Ghana ndio wanashikilia usukani katika orodha hiyo wakiwa nafasi ya
15 duniani wakifuatiwa na Ivory Coast iliyoko nafasi ya 21, Misri mabingwa wa soka wa Afrika
wapo nafasi ya tatu wakiwa nafasi ya 36 duniani wakifuatiwa na Nigeria iliyopo nafasi ya 38, Afrika Kusini 39 na Algeria nafasi ya 40.

Miamba ya zamani ya Afrika ambayo ilikuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu robo fainali ya kombe la dunia Cameroon inashika nafasi ya 48 ikiwa imeporomoka chini kwa nafasi sita, Senegal iko kwenye nafasi ya 51 ikiwa imepanda nafasi 18 na Tunisia ni ya 61 ikiwa imeshuka kwa nafasi 16.

Wakati nafasi ya za juu za orodha hiyo viwango vya ubora wa soka vaya Fifa, bado hakuna mabadiliko kwani mabingwa wa soka wa dunia Hispania wanaendelea kushikilia nambari moja ikifuatiwa na washindi wa pili wa michuano ya kombe la dunia Uholanzi na Brazil inashika nafasi ya tatu.

Ujerumani iko nafasi ya nne ikifuatiwa na Argentina na England iko kwenye nafasi ya sita, Uruguay iko nafasi ya saba ikiwa haijapanda wala kushuka, wakati Ureno imepanda kwa nafasi moja na inashikilia nafasi ya nane huku Italia ikiwa nafasi ya tisa na Croatia ya 10.
 
Fainali Kili Taifa Cup kufanyika Arusha

Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 15; Jumla ya maoni: 0

MAMBO yameiva kuhusiana na mashindano ya Kombe la Taifa ambayo yamepangwa kuanza Mei 7, 2011.

Lakini wakazi wa Dar es Salaam, ambako karibu miaka mitatu iliyopita hatua kuanzia ya robo fainali ilikuwa ikifanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, sasa hawataona mashindano ya mwaka 2011.

Akizungumza Jumatano, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro inayodhamini michuano hiyo, George Kavishe alisema maandalizi yamekamilika na kwamba Ijumaa watapanga droo ya mashindano hayo.

Hata hivyo alisema kutokana na Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kufungwa wameamua sasa kuanzia hatua ya robo fainali, nusu fainali na fainali zifanyike Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Michuano hiyo itaanza kwa timu kushindana kwenye vituo, ambapo vituo sita vimeteuliwa na timu ya kwanza kila kituo itafuzu robo fainali, wakati timu mbili nyingine zitakuwa zile zenye uwiano mzuri wa pointi lakini hazikushika nafasi ya kwanza kwenye makundi yao.

Kituo cha Kilimanjaro kitakuwa na mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na timu ya Taifa ya vijana, wakati Mwanza itakuwa na Kagera, Shinyanga, Mara na Mwanza.

Kituo cha Tabora kitakuwa na mikoa ya Kigoma, Singida, Dodoma na Tabora, huku Mbeya ikiwa na Rukwa, Iringa, Temeke na Mbeya. Mikoa itakayokuwa Lindi ni Mtwara, Ruvuma, Kinondoni na Lindi, huku Morogoro ikiwa na Pwani, Manyara, Ilala na Morogoro.

Kampuni ya Bia Tanzania ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo.
 
FIFA yaunda kamati kuisuluhisha Bosnia Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 21:08

ZURICH, Uswisi
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa, FIFA limeteua watu sita kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro ulioikumba soka ya Bosnia pamoja na kujaribu kuumaliza mgogoro huo uliosababisha taifa hilo kusimamishwa soka ya kimataifa.

Kamati hiyo iliyoitwa ya usuluhishi na maridhiano, itakuwa ikiujaribu kuleta maridhiano katika shirikisho la Bosnian chini ya kanuni za FIFA na UEFA na kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kabla ya Novemba mwaka huu.

"Baada ya majadiliano na wadau mbalimbali wa soka na kutokana na mashauriano na UEFA, kamati ya watu sita imeteuliwa kwenda Bosnia-Herzegovina kwa ajili ya kuweka mambo sawa," ilisema taarifa ya FIFA.

"Kamati ya maridhiano itakuwa ikifanya kazi badala ya Chama cha Soka Bosnia katika kipindi cha mpito kuelekea kwenye uchaguzi mkuu."Bosnia ilisimamishwa Aprili 1 baada ya shirikisho (NFSBiH) kushindwa kufumua mfumo wa utawaka wa shirikisho hilo ambao una marais watatu.

NFSBiH, iliundwa baada ya vita ya mwaka 1992-95 ya Bosnian kumalizika na kutokea mgawanyiko, imekuwa ikiongozwa na marais watatu ambao huchaguliwa kutokana na koo na kutumia utaratibu wa kawaida.

Vikundi vya waumini vya Serb, Croat na waislamu wamekuwa wakiongoza NFSBiH kwa miezi 18 kwa awamu.

Kufungiwa kwa Bosnia kunamaanisha kuwa haitoweza kushiriki michano ya kimataifa ikiwemo Euro 2012 na klabu za taifa hilo haziwezi kushiriki michuano yoyote ile ya Ulaya.

FIFA ilisema kuwa kazi ya kwanza ya kamati hiyo ni kuandaa taratibu za mkutano wa uchaguzi na katiba mpya ifikapo Mei 26, hatua ambayo NFSBiH haitahusisha viongozi wake wa sasa.
 
Barcelona, Man United nusu fainali Ulaya Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 21:09

LONDON,
BARCELONA na Manchester United zimeingia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kama ilivyokuwa mwaka 2009 baada ya kupata ushindi mwingine katika mechi zao za marudiano juzi usiku.

Lionel Messi aliifungia timu yake bao la 48 katika dakika ya 43 na kuifanya Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk na kuifanya timu hiyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-1.

Shughuli nyingine ilikuwa Old Trafford, ambako Park Ji-sung aliiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea iliyokuwa na wachezaji 10, alifunga dakika ya 46 kabla ya Didier Drogba kukwamisha mpira wavuni dakika ya 77. Javier Hernandez alikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 43 na kuifanya United kufuzu kwa jumla ya mabao 3-1.

"Nafikiri tumecheza vizuri mno dhii ya timu kali," kocha wa United, Alex Ferguson alisema. "Chelsea wamecheza soka ya aina yake leo (juzi). Nadhani sisi tulikuwa wazuri zaidi yao. Tulikuwa na watu wazuri kama, Park, Chicharito (Hernandez), kila mmoja amecheza soka ya aina yake."

Barcelona ni wazi sasa itakutana na Real Madrid, ambayo jana ilikuwa uwanjani na hazina ya mabao 4-0 dhidi ya Tottenham katika mechi yao ya marudiano.

United itacheza na mshindi kati ya Schalke na mabingwa watetezi, Inter Milan, na ni wazi watakwenda Ujerumani baada ya mchezo wa kwanza kushinda mabao 5-2 nchini Italia..

Vijana wa Barcelona, ambao waliifunga United 2-0 katika fainali miaka mwili iliyopita, walikuwa wanataka kuhakikisha hawafanyi vibaya Ukraine licha ya kuwa juu kwa mabao 5-1 waliyopata katika mchezo wa kwanza.

Lakini kocha, Pep Guardiola anasema Messi, Xavi Hernandez na David Villa sasa watapumzishwa mechi za ligi na michuano ya Copa del Rey wakiisubiri Madrid nusu fainali.

Nayo Shakthar iliyoivaa, Barcelona ilikuwa ikicheza kwa kasi lakini Messi ndiye aliyeanza kufunga bao dakika ya 43 baada ya kupata pasi ya Dani Alves aliyemzidi maarifa beki Pyatov likawa bao la tisa katika mechi 10.

Hiyo ni mechi ya kwanza kwa Shakhtar kupoteza ikiwa uwanja wa nyumbani kwa miaka miwili sasa.

"Nimekuwa shabiki wa kuifuatilia Shakhtar kwa miaka mitatu," Guardiola alisema. "Timu ni kali na naamini hatutakutana nao."Ryan Giggs alikuwa akitengeneza mipira kwa United na kuisaidia timu hiyo kuifikisha nusu fainali mara ya nne kati ya tano.

"Ilikuwa mechi ngumu," alisema Giggs. "Tumefunga mabao mawili. Kazi yangu ilikuwa rahisi, aliirahisisha Michael Carrick, ambaye alicheza vizuri sana. Mambo yanakuwa mepesi kadiri siku zinavyosonga."

Giggs waligongeana haraka haraka na John O'Shea upande wa kulia kabla ya kuingia nao ndani na kutoa krosi iliyomkuta Hernandez na kupiga shuti la karibu na kujaa wavuni.

Hernandez mwanzoni alifunga bao, lakini lilikataliwa, hiyo ilikuwa dakika ya 25 kwamba alikuwa ameotea kabla ya kufunga pasi ya Wayne Rooney.

Chelsea ambayo ilitumia nusu nzima ya kipindi cha kwanza kushambulia, ilikuwa siku mbaya tena kwa Fernando Torres, ambaye ameitwa na Carlo Ancelotti kwa kuunganisha nguvu akitumia mfumo wa 4-3-3 pamoja na Nicolas Anelka na Florent Malouda katika wingi.

Hata hivyo, mambo bado kwa Torres ambaye alinunuliwa kwa dau la pauni50-million kutoka Liverpool mapema Januari, alitoka na akaingia Didier Drogba.

"Tulitawala mchezo dakika 25 za kwanza, lakini tulishindwa kufunga," Ancelotti alisema. "Mwishoni mwa kipindi cha kwanza, tulitawala, walipofunga, ndipo mambo yakawa magumu zaidi, tumekwenda lakini tumerudi 10 na mambo yakawa mabaya."

Kazi ya Chelsea ilikuwa ngumu hata wakati Ramires alipoonyeshwa kadi ya pili ya njano katika dakika ya 70 kwa kumkwatua Nani, lakini Drogba alifunga kwa mpira wa pasi ya Michael Essien baada ya kutuliza gambani na kufumua shuti lililomzidi nguvu, Edwin van der Sar.

Lakini Park aliisaidia United. Giggs alitoa majalo kwa Park ambaye naye alituliza kabla ya kuujaza kimiani.
 
Carlo Ancelotti set to leave Chelsea at the season's end

• Chelsea hunt hindered by Arnesen's departure
• Third season of Abramovich era without a trophy

  • Dominic Fifield
  • guardian.co.uk, Wednesday 13 April 2011 22.30 BST <li class="history">Article history
    Carlo-Ancelottis-time-as--007.jpg
    Carlo Ancelotti's time as Chelsea manager looks set to end this summer Photograph: Jason Cairnduff/Action Images

    Carlo Ancelotti will see out the remainder of the season as Chelsea's manager but is expected to leave in the summer as the club come to terms with what will be only the third season of the Roman Abramovich era to fail to yield a trophy.
    Elimination from the Champions League on Tuesday by Manchester United, whom Chelsea trail by 11 points in the Premier League, prompted Ancelotti to admit that it was "not my decision" as to whether he would see out the remaining year on his contract. The Italian knows he will be compensated for that period if he is sacked and has yet to speak directly with Abramovich about his future. The club's chief executive, Ron Gourlay, has indicated that an assessment will only be made next month.
    Abramovich visited the dressing room following the 2-1 second-leg defeat, urging the crestfallen players to "keep going" through the run-in, an indication that no announcement on the manager's position is imminent. Yet there is an expectation within the squad that Ancelotti will depart.
    He and his staff, who were back at Cobham overseeing a light training session on Wednesday, accept such a relatively disappointing season will thrust the focus on their performances. They, like the players, remain committed to finishing the season with a flourish, which could see them overhaul Arsenal and go second. "We win together, we lose together," the goalkeeper Petr Cech said. "We need to finish the season strongly for ourselves, for the club, for everybody. We are not only playing for the manager or the owner. We are playing for the entire club."
    Chelsea's planning is not helped by the fact that the sporting director, Frank Arnesen, is due to leave for Hamburg at the end of the season. The Dane would have played a key role in the recruitment of a new manager, but his own replacement has yet to be determined.
    The list of candidates would include some familiar names though José Mourinho &#8211; who still commands fierce loyalty from a faction within the Chelsea squad &#8211; has stated his intention to remain in Spain and Guus Hiddink, a previous interim manager at the Bridge, would likely only be available once Turkey's Euro 2012 qualification campaign is complete. That could be as late as November.
    The former Italy manager Marcello Lippi expressed an interest on Wednesday. "I'd like to coach Chelsea and the Premier League fascinates me," he said. "I've had a satisfying year [off], but I miss coaching." Yet the lack of an obvious and available replacement for Ancelotti will effectively see him through to the summer. The reserve-team manager, Steve Holland, had been mentioned as a possible stopgap until the end of the campaign because he has the relevant coaching badges, though that notion has been abandoned.
    Whoever is in charge over the close season will have to oversee the continued regeneration of the team, with the exodus of older squad members expected to be quickened by the side's failure to reach the latter stages of the Champions League. Didier Drogba, José Bosingwa, Paulo Ferreira and Nicolas Anelka will be entering the final years of their contracts and will effectively be available.
    Younger players &#8211; such as Ajax's Gregory van der Wiel and Anderlecht's Romelu Lukaku &#8211; are on the list of targets.

Carlo Ancelotti set to leave Chelsea at the season's end

• Chelsea hunt hindered by Arnesen's departure
• Third season of Abramovich era without a trophy

  • Dominic Fifield
  • guardian.co.uk, Wednesday 13 April 2011 22.30 BST <li class="history">Article history
    Carlo-Ancelottis-time-as--007.jpg
    Carlo Ancelotti's time as Chelsea manager looks set to end this summer Photograph: Jason Cairnduff/Action Images

    Carlo Ancelotti will see out the remainder of the season as Chelsea's manager but is expected to leave in the summer as the club come to terms with what will be only the third season of the Roman Abramovich era to fail to yield a trophy.
    Elimination from the Champions League on Tuesday by Manchester United, whom Chelsea trail by 11 points in the Premier League, prompted Ancelotti to admit that it was "not my decision" as to whether he would see out the remaining year on his contract. The Italian knows he will be compensated for that period if he is sacked and has yet to speak directly with Abramovich about his future. The club's chief executive, Ron Gourlay, has indicated that an assessment will only be made next month.
    Abramovich visited the dressing room following the 2-1 second-leg defeat, urging the crestfallen players to "keep going" through the run-in, an indication that no announcement on the manager's position is imminent. Yet there is an expectation within the squad that Ancelotti will depart.
    He and his staff, who were back at Cobham overseeing a light training session on Wednesday, accept such a relatively disappointing season will thrust the focus on their performances. They, like the players, remain committed to finishing the season with a flourish, which could see them overhaul Arsenal and go second. "We win together, we lose together," the goalkeeper Petr Cech said. "We need to finish the season strongly for ourselves, for the club, for everybody. We are not only playing for the manager or the owner. We are playing for the entire club."
    Chelsea's planning is not helped by the fact that the sporting director, Frank Arnesen, is due to leave for Hamburg at the end of the season. The Dane would have played a key role in the recruitment of a new manager, but his own replacement has yet to be determined.
    The list of candidates would include some familiar names though José Mourinho – who still commands fierce loyalty from a faction within the Chelsea squad – has stated his intention to remain in Spain and Guus Hiddink, a previous interim manager at the Bridge, would likely only be available once Turkey's Euro 2012 qualification campaign is complete. That could be as late as November.
    The former Italy manager Marcello Lippi expressed an interest on Wednesday. "I'd like to coach Chelsea and the Premier League fascinates me," he said. "I've had a satisfying year [off], but I miss coaching." Yet the lack of an obvious and available replacement for Ancelotti will effectively see him through to the summer. The reserve-team manager, Steve Holland, had been mentioned as a possible stopgap until the end of the campaign because he has the relevant coaching badges, though that notion has been abandoned.
    Whoever is in charge over the close season will have to oversee the continued regeneration of the team, with the exodus of older squad members expected to be quickened by the side's failure to reach the latter stages of the Champions League. Didier Drogba, José Bosingwa, Paulo Ferreira and Nicolas Anelka will be entering the final years of their contracts and will effectively be available.
    Younger players – such as Ajax's Gregory van der Wiel and Anderlecht's Romelu Lukaku – are on the list of targets.
 
Mourinho dismisses City link

RivalsDM

PRINT RSS

2

Updated Apr 14, 2011 4:30 AM ET
Real Madrid coach Jose Mourinho has said it would be "impossible" for him to take over at Manchester City if they sacked Roberto Mancini.

Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats

Mourinho stated this week that he has no intention of leaving the Bernabeu any time soon, but he did admit that he saw his future back in the Premier League.
However, when asked about being linked with the City job, Mourinho replied: "Me to Manchester City? That's impossible."
Mourinho was also asked about the possibility of Cristiano Ronaldo joining AC Milan after their owner Silvio Berlusconi admitted his liking for the Portuguese superstar but, again, Mourinho was doubtful such a move would happen.
"I'm not saying it's impossible, because in football you never know, and (AC Milan's owner, Silvio) Berlusconi can make a crazy offer," he said.
"But it must be a true madness because Real Madrid don't want to sell Cristiano Ronaldo. "
 
Carlo Ancelotti at Chelsea: The case for him staying &#8211; or going

Should Chelsea's owner Roman Abramovich appoint a seventh manager in nine seasons or keep faith with the sixth?

  • Chelseas-manager-Carlo-An-007.jpg
    Chelsea's manager Carlo Ancelotti is on the brink but the club has already had six managers in the last eight years. Photograph: Alex Livesey/Getty Images

    WHY HE SHOULD STAY

    1 Better the devil you know

    This is no time for a knee-jerk reaction. Roman Abramovich had pursued Carlo Ancelotti over a period of time, hoping to prise him from Milan, and appeared to have been vindicated when the Italian secured the Premier League and FA Cup Double in his first season.
    That demonstrated his pedigree, so why should the faith be eroded now, even after a stodgier second campaign? Manchester United are seeking to secure a fourth league title in five years, and a third appearance in the Champions League final in four seasons, with their whole structure having benefited from the stability provided by Sir Alex Ferguson at the top.
    Chelsea, meanwhile, have been overseen by six managers in the eight years since Abramovich's takeover. If continuity is the key, then why instigate yet more upheaval?
    2 Lack of good replacement options

    Are Chelsea realistically likely to entice anyone better to the position than a two-time European Cup winning manager?
    Frank Rijkaard, Rafael Benítez and Marco van Basten are available, but may feel too much like damaged goods these days. Real Madrid's José Mourinho and Barcelona's Pep Guardiola would prefer another year at least in La Liga.
    Seeking out Porto's André Villas Boas, treading a familiar path to the Estádio do Dragão for an up-and-coming managerial talent, would constitute a risk. Would Marseille's Didier Deschamps take Chelsea to another level?
    And while Guus Hiddink, currently enduring an underwhelming stint with Turkey, has served as a stopgap at Stamford Bridge before, would either his or Marcello Lippi's appointment feel progressive? The list of potential candidates feels underwhelming.
    3 Time to finish the job

    The Italian deserves the chance to oversee the continued regeneration of this squad. He inherited a side that still bore the hallmarks of the Mourinho era at Stamford Bridge, with players who constantly reflect on the glory days of the recent past, and coaxed a fine domestic season from them last term. Yet the next stage, when the older players were to be moved on, was always likely to prove traumatic.
    The five senior players who left last summer were inevitably going to be missed at some point, just as some of those who depart over the next few months will be next season.
    But £73m was spent in January adding to this squad, including £50m on Fernando Torres, and more will be spent next summer. Ancelotti deserves the chance to mould this new side together and establish them as real contenders.
    WHY HE SHOULD GO

    1 Leadership has drifted

    There have been occasions this season when Ancelotti has appeared rather limp and ineffective, leaving him vulnerable to accusations that he has failed to eke the best from this squad.
    His inability to rouse the players from their prolonged mid-season "bad moment" was damning, suggesting he was genuinely perplexed as to how a side who had swept all before them either side of the summer break had suddenly drifted rudderless into mediocrity.
    At that time Chelsea needed to be shrugged forcibly out of their slumbers. Instead, they staggered from one frustration to another through the winter, securing only 10 points from 11 games, to render their title defence forlorn.
    2 Rumours of discontent

    There are murmurings of disappointment among the playing staff at a perceived lack of strength from the management. Some point to an apparent lack of resistance to the owner's decision to oust Ray Wilkins as assistant first-team coach, such a needlessly disruptive mid-season sacking, with the manager accepting Abramovich's abrupt decision.
    Others query whether previous incumbents, such as Mourinho or Hiddink, would merely have accepted the club medical staff's initial assessments of players' injuries and illnesses rather than questioning them more forcefully.
    The Italian is well liked in the dressing room and around the club at Chelsea &#8211; he is an amiable man &#8211; but whether there is as much respect for his managerial acumen now as there once was within the squad is open to question.
    3 Failure in Europe

    This will be only the third trophyless season of the Abramovich era at Stamford Bridge and, most tellingly, the days of this team progressing into the last four of the Champions League are apparently long gone.
    Ancelotti arrived in south-west London with a reputation as an expert at accumulating European Cups, yet his Chelsea team have lost all four knockout games against pedigree opposition &#8211; Internazionale last season and Manchester United this &#8211; with his inability to outwit Mourinho or Sir Alex Ferguson tactically shown up.
    Even by his own admission, the selection against United for the second leg did not have the desired effect, while his inability to get the best from Torres since the striker became a Chelsea player has damaged him.

Carlo Ancelotti at Chelsea: The case for him staying – or going

Should Chelsea's owner Roman Abramovich appoint a seventh manager in nine seasons or keep faith with the sixth?

  • Chelseas-manager-Carlo-An-007.jpg
    Chelsea's manager Carlo Ancelotti is on the brink but the club has already had six managers in the last eight years. Photograph: Alex Livesey/Getty Images

    WHY HE SHOULD STAY

    1 Better the devil you know

    This is no time for a knee-jerk reaction. Roman Abramovich had pursued Carlo Ancelotti over a period of time, hoping to prise him from Milan, and appeared to have been vindicated when the Italian secured the Premier League and FA Cup Double in his first season.
    That demonstrated his pedigree, so why should the faith be eroded now, even after a stodgier second campaign? Manchester United are seeking to secure a fourth league title in five years, and a third appearance in the Champions League final in four seasons, with their whole structure having benefited from the stability provided by Sir Alex Ferguson at the top.
    Chelsea, meanwhile, have been overseen by six managers in the eight years since Abramovich's takeover. If continuity is the key, then why instigate yet more upheaval?
    2 Lack of good replacement options

    Are Chelsea realistically likely to entice anyone better to the position than a two-time European Cup winning manager?
    Frank Rijkaard, Rafael Benítez and Marco van Basten are available, but may feel too much like damaged goods these days. Real Madrid's José Mourinho and Barcelona's Pep Guardiola would prefer another year at least in La Liga.
    Seeking out Porto's André Villas Boas, treading a familiar path to the Estádio do Dragão for an up-and-coming managerial talent, would constitute a risk. Would Marseille's Didier Deschamps take Chelsea to another level?
    And while Guus Hiddink, currently enduring an underwhelming stint with Turkey, has served as a stopgap at Stamford Bridge before, would either his or Marcello Lippi's appointment feel progressive? The list of potential candidates feels underwhelming.
    3 Time to finish the job

    The Italian deserves the chance to oversee the continued regeneration of this squad. He inherited a side that still bore the hallmarks of the Mourinho era at Stamford Bridge, with players who constantly reflect on the glory days of the recent past, and coaxed a fine domestic season from them last term. Yet the next stage, when the older players were to be moved on, was always likely to prove traumatic.
    The five senior players who left last summer were inevitably going to be missed at some point, just as some of those who depart over the next few months will be next season.
    But £73m was spent in January adding to this squad, including £50m on Fernando Torres, and more will be spent next summer. Ancelotti deserves the chance to mould this new side together and establish them as real contenders.
    WHY HE SHOULD GO

    1 Leadership has drifted

    There have been occasions this season when Ancelotti has appeared rather limp and ineffective, leaving him vulnerable to accusations that he has failed to eke the best from this squad.
    His inability to rouse the players from their prolonged mid-season "bad moment" was damning, suggesting he was genuinely perplexed as to how a side who had swept all before them either side of the summer break had suddenly drifted rudderless into mediocrity.
    At that time Chelsea needed to be shrugged forcibly out of their slumbers. Instead, they staggered from one frustration to another through the winter, securing only 10 points from 11 games, to render their title defence forlorn.
    2 Rumours of discontent

    There are murmurings of disappointment among the playing staff at a perceived lack of strength from the management. Some point to an apparent lack of resistance to the owner's decision to oust Ray Wilkins as assistant first-team coach, such a needlessly disruptive mid-season sacking, with the manager accepting Abramovich's abrupt decision.
    Others query whether previous incumbents, such as Mourinho or Hiddink, would merely have accepted the club medical staff's initial assessments of players' injuries and illnesses rather than questioning them more forcefully.
    The Italian is well liked in the dressing room and around the club at Chelsea – he is an amiable man – but whether there is as much respect for his managerial acumen now as there once was within the squad is open to question.
    3 Failure in Europe

    This will be only the third trophyless season of the Abramovich era at Stamford Bridge and, most tellingly, the days of this team progressing into the last four of the Champions League are apparently long gone.
    Ancelotti arrived in south-west London with a reputation as an expert at accumulating European Cups, yet his Chelsea team have lost all four knockout games against pedigree opposition – Internazionale last season and Manchester United this – with his inability to outwit Mourinho or Sir Alex Ferguson tactically shown up.
    Even by his own admission, the selection against United for the second leg did not have the desired effect, while his inability to get the best from Torres since the striker became a Chelsea player has damaged him.

Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom