Real ikimaliza kwa Spurs safari kwa Barca Send to a friend Tuesday, 12 April 2011 19:56
LONDON, England
REAL Madrid inakibarua cha kumaliza kazi yake ya kuitoa Tottenham Hotspur leo kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kucheza dhidi ya mahasimu wao Barcelona.
Real itakuwa White Hart Lane wakiwa kifua mbele baada ya ushindi wake wa mabao 4-0 dhidi Spurs 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wiki iliyopita.
Real na Barca zitakutana kwa mara ya kwanza kwenye hatua hiyo tangu walipofanya hivyo mwaka 2002.
Kocha wa Real, Jose Mourinho, aliisifia Spurs na soka ya England kuwa ni bora na inayopaswa kuheshimiwa kwa kusema ni timu za England pekee zinaweza kusawazisha mabao manne.
Kama alichosema ni kweli, basi klabu kama Spurs, ambayo hajashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa muda wataweza kupigana na kupata ushindi.
Baada ya Manchester United, Spurs ni timu nyingine ya England iliyokuwa na historia ya pekee barani Ulaya kwa mwanzoni mwa miaka ya 1960 ilikuwa timu yakwa kutwaa taji la Ulaya kwa kuifunga Atletico Madrid 5-1 katika fainali ya Kombe Washindi Ulaya mwaka 1963.
Spurs pia mwaka 1962 ilifanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Ulaya wakati huo wakiwa na kocha Bill Nicholson, aliyejijengea heshima kubwa kwa kuibwaga Real ikiwa na nyota wake Alfredo Di Stefano na Ferenc Puskas.
Real, nayo iliweka historia kwa kuwa timu ya kwanza baada ya miaka 24 kushinda kwenye Uwanja wa White Hart Lane walipowafunga mabingwa watetezi wa Kombe la UEFA, Spurs kwa bao 1-0 mwaka 1985, sasa wamejiweka kwenye nafasi nyingine nzuri ya kurudia historia hiyo leo.
Kocha wa Spurs, Harry Redknapp alisema: ìHadi sasa tumepata uzoefu wa kutosha naamini leo pia tutaongeza uzoefu mwingine. Tutacheza kwa kiwango chetu cha kawaida.î
Watashuka dimbani bila ya mshambuliaji wake Peter Crouch, aliyepewa kadi nyekundu wiki iliyopita, nayo Real Madrid itamkosa beki wake Pepe.
Mourinho, pia atamtumia mshambuliaji Karim Benzema aliyepoma majeruhi yake kuchukua nafasi ya Emmanuel Adebayor, aliyefunga mabao mawili kwa kichwa wiki iliyopita.