Suluhu yakera wachezaji Man. United
Send to a friend Thursday, 24 February 2011 20:36 0diggsdigg
LYON, Ufaransa
KIUNGO wa Manchester United, Michael Carrick amesema yeye na wachezaji wenzake, wamekerwa na suluhu dhidi ya Marseille ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 lakini akasema anaamini Red Devils itashinda mchezo wa marudiano.
Katika mchezo huo, kila upande ulishindwa kutumia nafasi ilizopata, na Darren Fletcher ndiye pekee aliyepata nafasi nzuri ya kumtungua kipa wa Marseille, Steve Mandanda lakini akashindwa kufunga.
Kikosi cha Sir Alex Ferguson kilichokuwa Stade Velodrome kina nafasi ya kutumia uwanja wa nyumbani licha ya kuelezwa kuwa si kigezo sahihi cha timu kushinda, na Carrick alisisitiza kusema, walicheza ovyo.
Aliiambia ITV Sport: "Tumesikitika kushindwa kufunga, lakini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri nyumbani, lakini hiyo si kitu sana, kinachotakiwa ni kucheza vizuri zaidi ya mchezo wa kwanza.
"Mechi za ugenini ni ngumu hasa Ulaya, lakini tulichofanya hakifanani na sisi, tulistahiki kushinda.
"Tunaamini marudiano tutafanya kweli kwenye Uwanja wetu wa Old Trafford.
"Haikuwa kama vile tunataka, hatukucheza vizuri, hatukuwa makini kwa k ila tulichokifanya.
Naye kocha wa Manchester United, Ferguson alisema: ìMechi ilikuwa mbaya.
Wenzetu walihakikisha hatufungi. 0-0 ni matokeo mabaya, lakini sasa tunajiamini kwa kuwa tutakuwa nyumbaniî aliongeza Ferguson ambaye naye anaamini mambo yote yatakuwa Old Trafford wiki tatu zijazo.
ìSi matokeo mabaya sana, uzuri ni kwamba hatukuruhusu bao,î alisema kocha wa Marseille, Didier Deschamps. ìIlikuwa mechi ngumu dhidi ya timu ngumu yenye wachezaji wazuri.î
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amekiri kuwa vijana wake wa Bavarian walikuwa na bahati hata kushinda bao 1-0 tena ugenini dhidi ya Inter katika mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 ya Ligi ya Ulaya.
Rummenigge alisema kila upande ulipata nafasi ya kufunga, lakini vijana wake wa Bavarians walikuwa washindi mwisho wa siku.
"Kila timu zilipata nafasi nyingi na nzuri za kufunga, lakini wachezaji walishindwa kuzitumia," aliiambia Sky Sport baada ya mechi. "Ilikuwa mechi ya kufurahisha kuangalia.
"Tulikuwa na bahati na tunashukuru tumeshinda. Lakini hatuwezi kufikiria kuwa tayari tumeshafuzu. Lazima kujipanga vizuri zaidi tuweze kufika mbali," alisema.
Naye Rais wa Inter, Massimo Moratti amesema pamoja na vijana wake wa Nerazzurri kupoteza mchezo kwa kufungwa 1-0 na Bayern Munich kwenye Uwanja wa Giuseppe Meazza, bado wana imani kubwa kufuzu.
Mlezi huyo aliwapongeza wachezaji wake, kwa kucheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kitu kinachompa matumaini kwa mchezo wa marudiano.
"Hatukuwa na bahati kwa jinsi mchezo ulivyokuwa," Moratti aliiambia Sky Sport baada ya mchezo. "[Kocha] Leonardo alifanya kazi nzuri, katika timu ilivyocheza, kwa kutengeneza mipira mingi, pasi na mashambulizi.
"Tunatakiwa kujipanga na kuicheza mechi vizuri, tunaweza hata kushinda 1-0 huko kwao Munich kwa jinsi tulivyocheza mchezo wa kwanza."
Moratti alisikitishwa kuumia kwa Andrea Ranocchia. Mchezaji huyo aliumia kifundo cha mguu na kushindwa kuendelea na mchezo. Kuumia kwa Ranocchia kweli kumetumaliza," alimaliza. Mechi za marudiano zitachezwa Machi 15.