Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Yanga kuwafaraji waathirika wa mabomu Send to a friend Monday, 21 February 2011 21:26

sendeuyanga1.jpg
ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu

Jessca Nangawe

UONGOZI wa klabu ya Yanga pamoja na wachezaji wake leo wanatarajia kutembelea waathirika wa mabomu katika eneo la Gongolamboto jijini Dar es Salaam na kuwafariji kwa misaada ya vitu mbalimbali.

Klabu hiyo imeelezwa kuguswa mno na tukio hilo na kulazimika kutoa msaada kwa wakazi wa Gongolamboto kulikotokea milipuko hiyo ya mabomu iliyosababisha watu zaidi ya 20 kupoteza maisha na mamia wengine kuumia na mali zao kuharibiwa.

Akizungumza na Mwananchi jana, ofisa habari wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema Yanga ikiwa sehemu ya jamii leo itazuru Gongolamboto ambako wachezaji na viongozi wa klabu hiyo watatoa pole na kuwafariji waathirika.

Alisema uongozi huo utakwenda kutoa msaada huo kuanzia saa 4:00 asubuhi huku wakitoa changamoto kwa watu wengine walioguswa kwa namna moja ama nyingine kujitokeza na kutoa msaada.

"Tukiwa kama sehemu ya jamii ambayo imepatwa na tatizo hili tutahakikisha na sisi tunakua mstari wa mbele katika kutoa msaada wetu kwa ndugu zetu, hivyo sisi pamoja na wachezaji wetu tutakwenda huko (Gongolamboto) na kuwafariji wote waliokumbwa na tatizo hilo pamoja na kuwapa kile kidogo ambacho tumekipata,"alisema Sendeu.

Katika hatua nyingine, Sendeu alisema kiungo wao Shamte Ally aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu sasa ameanza mazoezi na kujiunga na wenzake baada ya hali yake kuonekana kuleta matumaini makubwa.

Alisema kwa mujibu wa daktari wake Shamte ameanza kurejea katika hali yake na endapo hali yake itaridhisha anaweza kucheza katika mchezo wao ujao kati yao na Ruvu Shooting.

 
Chelsea, Man United zaingia majaribuni Send to a friend Monday, 21 February 2011 21:21

LONDON, Uingereza
MATOKEO mazuri ya Arsenal na Tottenham Hotspur katika mechi za kwanza za hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki moja iliyopita ndiyo yanayozifanya Chelsea na Manchester United kuwa katika mtihani mkubwa wa michuano hiyo wiki hii.

Spurs ilianza vyema kwa kuilaza AC Milan kwenye Uwanja wa San Siro kwa bao 1-0, kisha Arsenal ikailaza Barcelona kwa mabao 2-1 dhidi ya Barcelona, kiasi cha kuwakuna mashabiki wa soka wa England, ambao macho wameyaelekeza kwa Chelsea na Man United.

Chelsea , imesafiri kwenda Denmark kuikabili FC Copenhagen huku ikikabiliwa na changamoto kadhaa zikiwamo za kuporomoka kwa kiwango , kutolewa kwenye Kombe la FA mwisho wa wiki.

Mtihani huo wa kutakiwa kuwafurahisha mashabiki wa soka wa England, unaanzia kwa Chelsea leo mjini Copenhagen, Denmark , huku Man United ikijitupa dimbani ugenini kesho dhidi ya Olympic Marseille ya Ufaransa.
Lakini, wasiwasi wa mashabiki wa soka wa hapa ni kufanyika kwa fainali ya ligi hiyo kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, wakikumbuka tukio la mwisho la mechi kama hiyo kufanyika Old Trafford, Manchester na kuzikutanisha timu za Italia.

Tukio la msimu wa 2003 lilizikutanisha AC Milan ambayo iliilaza Juventus kwa penalti baada ya suluhu ya bila mabao.

Ushindi wa Spurs dhidi ya AC Milan unachkuliwa kama changamoto kwamba uwezekano wa kukutanisha timu za Italia,Wembley Stadium utakuwa mdogo, huku mashabiki wa England wakieleza matumaini ya kushuhudia timu mojawapo ya Ligi Kuu ikicheza fainali hiyo, Mei 28.

Lakini, matokeo ya msimu uliopita ambako hakuna klabu hata moja ya England iliyofikia nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu 2003 yanachukuliwa kama changamoto nyingine kubwa inayozikabili timu za England, huku zote nne zikijiamini.

Chelsea, ina kibarua zaidi cha kufuzu kucheza robo fainali ikiwa na mategemeo ya kuwa ya kwanza kutoka London kutwaa taji hilo baada ya jaribio la mwaka 2008 kuzimwa na Manchester United kwa penalti mjini Moscow, Russia.

Kikosi cha Chelsea, ambacho kimeongeza nguvu ya Fernando Torres kwa pauni 50 milioni kutoka Liverpool, hata hivyo kimegeuka kivuli, kiasi cha kumweka katika mtihani kocha Carlo Ancelotti huku beki aliyesajiliwa kutoka Porto, Daivd Luiz akiwa hawezi kuichezea timu yake mpya.

Chelsea, kwa upande mwingine inaingia uwanjani ikisaka taji la kwanza kubwa Ulaya, huku Man United wakisubiri kuendeleza mafanikio yao Ulaya, ambako wameshinda taji hilo mara tatu wakiwa chini ya Sir Alex Ferguson.

United, ambao waliruhusu bao moja kaitka hatua ya makundi watasafiri kwenda Ufaransa wakiota mafaniko hayo huku Wayne Rooney akirejea katika makali yake .


 
Orient yaiduwaza Arsenal Kombe la FA Send to a friend Monday, 21 February 2011 21:18

TIMU ya Daraja la Tatu, Leyton Orient imeiduwaza Arsenal iliyochezesha kikosi tofauti na kile kilichoilaza Barcelona kwa kulazimisha sare ya bao 1-1 katika mchezo wa raundi ya tano ya Kombe la FA.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Brisbane Road, wageni Arsenal walikuwa na matumaini ya kufuzu kucheza robo fainali kirahisi, lakini Orient wakatibua mipango hiyo.

Kocha Arsenel Wenger alikiri baada ya mchezo huo kuwa hajawahi hata kumsikia Jonathan Tehoue ambaye alisawazisha bao hilo,

Kwa matokeo hayo, Orient watasafiri hadi London Madhariki kwa mchezo wa matumaini ya kukutana na Manchester United robo fainali

"Sijawahi kumsikia huyo mchezaji wao,í Wenger alikiri alipoulizwa kuhusu Tehoue, ambaye alifuta bao la mapema la Tomas Rosicky.

ëNdiyo ni Mfaransa, lakini simjui, sikuwahi kumsikia, nimeshangazwa naye, amefunga bao zuri . Leyton Orient walicheza mchezo safi . Hatuwezi kusema tumewaondoa, bado."

Kocha wa Orient, Russell Slade alikuwa mwenye furaha kwa matokeo hayo na bao la kusawazisha dakika za mwisho.

"Kupata bao dhidi yao (Arsenal) chini ya Arsene Wenger na watu wake kama Cesc Fabregas au yeyote ni jambo la ajabu," alisema.

ëNilipomchezesha tangu dakika za mwanzo, mara kadhaa Jonathan hakuwa na matokeo kama hayo, leo ameanzia benchi ameonyesha ujuzi. Amefunga mabao mengi kwetu, lakini hili la dakika ya 85 limetufurahisha."

Mwenyekiti wa Orient , Barry Hearn alikuwa ameahidi kuwazawadia safari ya Las Vegas, Marekani kama watalazimisha mchezo wa marudiano dhidi ya Arsenal.

Kocha huyo alieleza kuwa amehakikishiwa na mwenyekiti wake kwamba ziara ya Las Vegas itakuwa kati ya Mei na Juni mwaka huu kwa siku tatu.

"Tunawaza kucheza na Man United, lakini kwanza twende Emirates."

Kuhusu kuikabili Man United endapo watafuzu, Wenger aliongeza : "Ni kitu cha kuvutia, ni mchezo ambao kila mmoja anausubiri."

"Lakini, leo nimepata onyo kwamba mchezo wa marudiano kwetu dhidi ya Leyton Orient utakuwa mgumu."

Wakati huo huo, Inter Milan inajiandaa kuivamia kambi ya Arsenal msimu ujao kwa kumsajili Robin van Persie.

Van Persie amekuwa akielezwa kuwa mchezaji pekee ambaye nter Milan imepanga kumnasa msimu ujao na imekuwa ikimfuatilia kwa karibu yeye na mwenzake, Andrey Arshavin.

Inter imeshindwa kurejea kiwango chake cha msimu wa mafanikio mwaka jana na mataji matatu chini yaJose Mourinho, ndiyo maana wanapanga kufumua na kuunda upya kikosi chao.

Kulingana na gazeti la News of the World, Vam Persie ambaye amekuwa katika kiwango kikubwa msimu hu anaelekea kuwa kutakiwa na klabu hiyo.

Hadi sasa, amefunga mabao 13 baada ya kurejea uwanjani mwezi Desemba baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Lakini, Arshavin amekuwa hatabiriki tangu ajiunge na Arsenal , ingawa kwa sasa Inter imetenga pauni 42 milioni kuwasajili wawili hao, kitu ambacho kocha Wenger anaweza kupingana nacho.
 
Barcelona yazima mzimu wa matokeo mabaya Hispania Send to a friend Monday, 21 February 2011 21:19

BARCELONA, Hispania
BARCELONA imezidi kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Hispania baada ya kuilaza Athletic Bilbao 2-1 juzi na kupanua tofauti ya pointi kuwa tano dhidi ya Real Madrid.

David Villa ambaye Jumatano alifunga bao dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya aliipa timu yake bao la kuongoza dakika ya nne ya mchezo huo baada ya beki Dani Alves kuinasa pasi ndegu ya Xavi Hernandez na kumsogezea mpira ambao aliujaza wavuni.

Mshambuliaji wa Bilbao,Andoni Iraola alisawazisha dakika ya 50 kwa penalti baada ya Sergio Busquets kumchezea rafu Fernando Llorente.

Xavi na Alves walishirikiana kwa mara nyingine huku beki Alves akimlisha Lionel Messi ambaye aliujaza mpira wavuni na kuandika bao la pili kwa Barcelona, dakika ya 78.

ìNinafikiri ni mafanikio makubwa kuwa kileleni kwa tofauti ya pointi tano zaidi ya Madrid,î alisema kocha Pep Guardiola. ìHakuna timu iliyo bora barani Ulaya.î

Kwa ushindi huo, Barca ambao ni mabingwa watetezi walizika suala la kiwango chao baada ya Jumatano iliyopita kulazwa na Arsenal siku chache baada ya sare dhidi ya Sporting Gijon kwenye mchezo wa ligi.

ìNinachekeshwa na wale wanaowaza kwamba wao (Barcelona)wapo katika mzozo,î als ema kocha wa Bilbao,Joaquin Caparros.

Bilbao ililazimisha suluhu ya 0-0 dhidi ya Barca zilipokutana kwenye Uwanja wa Camp Nou kwenye mchezo wa Kombe la Mfalme, Januari mwaka huu walipoamua kucheza kwa kujihami.

Caparros alirejea mkakati huo katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo, akimwacha mbele Fernando Llorente pekee.

Huku beki Carles Puyol akiendelea kupata nafuu, Busquets alicheza pamoja na Gerard Pique kama beki wa kati wa Barcelona huku Jose Pinto akiwa golini badala ya Victor Valdes ambaye alipumzishwa kutokana na uvimbe kwenye goti.

Awali, timu zote zilicheza vizuri na kuonyesha ujuzi wao wote, lakini Barcelona wakimiliki zaidi mpira na Bilbao kucheza karibu na lango lao kwa muda mrefu na kushambulia kwa kushtukiza.

Bao la Villa ambalo ni la 16 kwake msimu huu liliipa uongozi timu hiyo, lakini Bilbao walikuwa imara na kumwezesha Llorente kupiga krosi safi ambayo Markel Susaeta alipiga nje dakika ya 11.

Baada ya hapo, Barca waliendelea kutawala mchezo, Villa akigonga mwamba dakika ya 26. Licha ya tishio hilo, Bilbao waliendelea kuonyesha kuwa hatari na Llorente akimlazimisha Pinto kufanya kazi ya ziada dakika ya 37 kuokoa hatari.

Mapema, Villarreal ilishikwa na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Malaga inayoshia mkia, hukuJavad Nekounam akigunga mawili katika ushindi wa 4-0 wa Osasuna dhidi ya Espanyol iliyokuwa chini ya kocha Jose Luis Mendilibar kwa mara ya kwanza na Ivan Rakitic aliipa Sevilla ushindi wa 1-0 dhidi ya Hercules.

Marco Ruben alitangulia kuipa bao Villarreal, dakika ya 36, lakini Sebastian Fernandez aliisawazishia Malaga kwa shambulizi la kushtukiza akisaidiwa na Jose Rondon, dakika ya 82.

Kwa sare hiyo, Villarreal imeendelea kushikilia nafasi ya nne, pointio mbili nyuma ya Valencia.

Kwa kushinda kwake, Osasuna imejitoa katika kundi la kushuka daraja, huku Espanyol inayoshika nafasi ya sita ikizidi kuporomoka kwa kupoteza mchezo wa nne.

Sevilla imeshinda mchezo wake wa kwanza katika muda wa wiki nne na kuhitaji pointi nne kukata tiketi ya michuano ya Europa League.

Kipa wa Deportivo La Coruna, Daniel Aranzubia alifunga bao la dakika za majeruhi na kuipa sare timu yake ya bao 1-1 dhidi ya Almeria, Racing Santander ikailaza Getafe 1-0.

Jana usiku, Mallorca ilitarajiwa kucheza dhidi ya Real Sociedad kwenye mchezo mwingine wa ligi hiyo.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments




0 #1 Nyagu Ncndagi 2011-02-22 06:59 kwamba Sevila inahitaji pointi nne tu kukata tiketi ya kucheza Europa League ni uongo mkubwa sana. Mwandishi wa habari hii anatakiwa aombe msamaha kwa wasomaji wake!
"Sevilla imeshinda mchezo wake wa kwanza katika muda wa wiki nne na kuhitaji pointi nne kukata tiketi ya michuano ya Europa League".Hispania inapeleka Europa league timu 2 tu moja kwa moja achilia zile za kupitia milango ya mashindano mengine tofauti na ligi kuu, kwenye ligi kuu bado mechi 14 ligi kuishi iweje useme akipata pointi 4 amekata tiketi ya Europa? Basi Barcelona ameshachukua kombe! Na wewe mwandishi sikutofautishi na washabiki wanaosema Chelsea imeshashinda magoli 3-0 wakati mchezo unaendelea na ni dakika ya 60 tu! How far are u sure that the game will end with the same results so far!

Quote
 
Polisi Dodoma yamponza kocha Majimaji Send to a friend Monday, 21 February 2011 21:16

Sosthenes Nyoni
UONGOZI wa Majimaji ya Songea, umemtimua kocha wake Sebba Nkoma baada ya timu hiyo kutandikwa mabao 3-2 na Polisi Dodoma katika mchezo wa Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.

Majimaji ambao walicheza vizuri mechi na Yanga na kuonyesha uhai mkubwa, ilishindwa kuhimili vishindo vya Polisi na kufungwa mabao hayo.

Mwenyekiti wa Majimaji Hemed Dizumba aliiambia Mwananchi jana kuwa Nkoma ameondolewa kwenye timu hiyo kwa kushindwa kutimiza malengo ya timu ikiwemo kufanya vema katika mechi za Ligi Kuu.

Dizumba alisema kuwa mkataba wa Nkoma ulikuwa umalizike Februari 27 lakini wameamua kusitisha baada ya kuona timu inazidi kufanya vibaya.

"Tuliingia naye mkataba wa miezi miwili ili atusaidie lakini sasa tunaona kila kukicha timu inaboronga tu hivyo hatuoni sababu ya kuendelea kuwa naye.

"Ukiangalia hadi sasa tumeshacheza nusu ya mechi za mzunguko wa pili lakini hakuna mabadilio, hivyo wakati tunaendelea kuangalia utaratibu mwingine timu itakuwa chini ya mwalimu msaidizi, Peter Mhina," alisema Dizumba.

Hata hivyo, kocha msaidizi wa Majimaji, Peter Mhina aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa kutokufanya vizuri kwa timu hiyo kwa sasa kunatokana na klabu kuendeshwa kisiasa za CCM.

Alisema kuwa siasa hizo zimepelekea hata wakazi wa mkoa huo kupunguza mapenzi yao kwa timu hiyo kiasi cha kuwafanya wachezaji wapende kucheza ugenini zaidi kuliko nyumbani.

Katika msimamo wa ligi, Majimaji iko katika nafasi ya 11 kati ya timu 12 zinazoshiriki Ligi Kuu ikiwa na pointi 11.

Makocha wengine ambao tayari walikuwa wametimuliwa ama mikataba yao kusitishwa na klabu zao kwa msimu huu pekee ni Kostadin Papic(Yanga), George Ssemogerere (Kagera), Wilfred Kidau (AFC) na Fredy Minziro aliyekuwa Ruvu Shooting.
 
Kipa Azam aanza tambo za ubingwa Send to a friend Monday, 21 February 2011 21:15

Sosthenes Nyoni
KIPA namba moja wa timu ya Azam, Vladimir Niyomkuru amesema kuwa wamejipangia lengo lao ni kuhakikisha wanashinda mechi zote pasipo kuangalia Yanga na Simba zinafanya nini.

Niyonkuru ambaye kwasasa anauguza kidole chache cha mkono baada ya kuumia akiwa mazoezini na timu yake, alisema kuwa hawaoni timu ya kuwazuia kutimiza azma yao hiyo kwani wachezaji wote wanajituma.

"Hatuchezi kwakuangalia Yanga na Simba zinafanya nini, sisi tunejipanga kuhakikisha hatupotezi mechi na tukitimiza hapo ndiyo tutajua tupo katika nafasi gani.

Alisema kuwa kwa ujumla kikosi chao kimebadilika sana baada ya ujio wa kocha Stewart Hall hivyo uhakika wa kushinda nafasi mbili muhimu za juu wanao.

Katika hatua nyingine Niyonkuru ambaye ni raia wa Burundi aliwataka waamuzi kuchezesha kwa haki badala ya kuzibeba Yanga na Simba.

"Nakwambia kama waamuzi watachezesha kwa haki utaona kitakachotokea, tatizo yale mambo yao ya Yanga na Simba, mimi nimetembea Kenya na hata Uganda hapa waamuzi wanaharibu sana ligi," alisema Niyonkuru

 
Oljoro JKT kutambulishwa leo Send to a friend Monday, 21 February 2011 21:14

Moses Mashalla,Arusha
KLABU ya soka ya JKT Oljoro ya mkoani Arusha leo itapambana na Rangers Sports Club ya Kenya katika mchezo wa kirafiki unaotaraji kupigwa ndani ya dimba la Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Chama cha Soka mkoani Arusha (ARFA), Adam Brown alisema kuwa lengo la mchezo huo ni kuipongeza timu hiyo kwa kukata tiketi ya Ligi Kuu pamoja na kuwapa fursa wakazi wa Arusha kuishuhudia timu yao .

Pia taarifa hiyo ilisema ya kuwa mchezo huo utakuwa ni wa maandalizi kwa klabu ya Rangers ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Kenya inayotaraji kuanza hivi karibuni.

Brown, aliwataka wakazi wa Arusha na viunga vyake kujitokeza kwa wingi mnamo siku hiyo kushuhudia mchezo huo ambao unataraji kuwa mkali na wa kuvutia.

Naye Calvin Kiwia anaripoti kuwa Meneja wa timu ya AFC Arusha, Dennis Shemdoe amewapongeza maafande wa Oljoro JKT Arusha baada ya kukata tiketi ya kushiriki Ligi kuu ya Vodacom msimu ujao na kuufanya mkoa huo kuwa na timu mbili sasa Ligi kuu.

Shemdoe aliliambia Mwananchi jana kwa simu kuwa ni jambo la kujivunia kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na dhahiri umepiga hatua moja ya kimaendeleo ya soka.

"Nawapongeza viongozi na wachezaji wa timu ya Oljoro kwa kazi nzuri waliofanya ya kuhakikisha wanashiriki Ligi kuu pamoja na ushindani uliokuwepo kwenye ligi hiyo na kufanikiwa kwa hilo," alisema Shemdoe.

 
Milan kuipa dawa Simba kuiua Mazembe


Na Elizabeth Mayemba

KOCHA Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri ameanza kutafuta mikanda (DVD) ya fainali ya michuano Klabu Bingwa ya Dunia kati ya TP Mazembe na
Inter Milan, ili aweze kuitumia katika maandalizi ya timu yake.

Simba inatarajia kucheza mchezo wa mzunguko wa pili wa Klabu Bingwa Afrika, dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Machi 18 na 20 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja wa Simba Innocent Njovu, alisema kocha huyo kuna mkanda ambao anatarajia kuupa hivi karibuni kwa ajili ya kuutumia wakati timu yake ikijiandaa kupambana na TP Mazembe.

"Kocha kasema kuna mkanda ambao anatarajia kuupata muda wowote kuanzia sasa, sijui ni mkanda gani lakini alisema akiupata wa fainali ya Klabu Bingwa Dunia kati ya TP Mazemba na Inter Millan, utamsaidia sana," alisema Njovu.

Alisema kocha anataka kuhakikisha anaandika historia kwa kuifunga timu hiyo na ndiyo maana, amekuwa akihangaika kupata mkanda wake ili kusoma mbinu za wapinzani wao.

Njovu alisema timu yao imeanza kufanya mazoezi ya ufukweni jana asuhuhi na leo wataanza kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu ya Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Jumapili.

Alisema maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri na makosa yaliyojitokeza katika mechi iliyopita, kocha atayafanyia kazi ili waibuke na pointi tatu.

 
Spanish La Liga Roundup, Feb. 20


storypage_APlogo_01.png




PRINT RSS

52 comments »

Updated Feb 20, 2011 5:17 PM ET
Barcelona beat Athletic Bilbao 2-1 Sunday to move five points clear of Real Madrid at the top of the table in Spain.
David Villa gave Barcelona the lead in the fourth minute after Dani Alves tapped back a long pass from Xavi Hernandez for the Spain striker to volley home.
Bilbao's Andoni Iraola equalized in the 50th from the penalty spot after Sergio Busquets had fouled Fernando Llorente in the area.
Xavi and Alves linked up again for the Brazil right back to assist Lionel Messi inside the six-yard box for Barcelona's 78th-minute winner.

Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats

With the victory, the defending champions laid to rest any doubts about their form after having drawn with Sporting Gijon and lost to Arsenal in the Champions League this past week.
Bilbao had earned a 0-0 draw in its last visit to Camp Nou in the Copa del Rey in January by playing without forwards and putting everyone behind the ball.
Bilbao manager Joaquin Caparros repeated the same strategy in the first half, with the exception of striker Fernando Llorente alone up front.
With Carles Puyol still recovering from a leg injury, Busquets played alongside Gerard Pique in the middle of Barcelona's defense, while Jose Pinto replaced Victor Valdes in goal as he rested a sore knee.
Both sides were true to their styles early with Barcelona controlling the ball and Bilbao playing deep and looking for the counterattack.
Villa put the hosts ahead early with his 16th goal of the season, but Bilbao held firm and Llorente sent a dangerous cross that Markel Susaeta shot into the side netting in the 11th.
Barcelona continued to dominate possession with Villa hitting the crossbar with a chip shot in the 26th. Even so, Bilbao remained dangerous and Llorente drew a save from Pinto with a header in the 37th.
Caparros sent on forward Gaizka Toquero after the break and ordered his team to press up the pitch.
The tactic soon paid off when a bad pass from Eric Abidal led to Llorente winning the spot kick that leveled the score.
Villa came close to regaining the lead in the 70th, but Bilbao goalkeeper Gorka Iraizoz touched his shot just enough to send it wide.
Messi, much more active after halftime, beat his mark in close to score his league-best 25th goal- one more than Real Madrid's Cristiano Ronaldo. The Argentina star has 41 goals in all competitions.
Earlier, Villarreal was held to a 1-1 draw by last-place Malaga, Javad Nekounam scored twice in Osasuna's 4-0 win over Espanyol on coach Jose Luis Mendilibar's debut, and Ivan Rakitic gave Sevilla a 1-0 win over Hercules.
Marco Ruben put Villarreal ahead in the 36th minute, but Malaga's Sebastian Fernandez finished off a counterattack led by Jose Rondon to split the points in the 82nd.
"We were playing well, looking for the second goal, but we didn't get it and they waited for their chance and took it," Villarreal coach Juan Carlos Garrido said.
With the draw, Villarreal remained in fourth place, two points behind provincial rival Valencia.
Nekounam gave Osasuna the lead in the 14th minute, heading in a corner delivered by fellow Iran international Masoud Soleimani, and added the second from the penalty spot in the 55th after Espanyol's Aldo Duscher had handled in the area.
Manuel "Lolo" Ortiz made it 3-0 in the 80th, and Fernando Soriano capped the victory in the 88th.
"You dream to win in your debut," Mendilibar said. "But the important thing is the motivation of the players who believe in what they are doing."
Osasuna moved out of the drop zone with the win, while sixth-place Espanyol has lost its last four games.
At Sanchez Pizjuan stadium, Rakitic scored his first goal since joining Sevilla in January when he converted a pass from Alvaro Negredo in the 21st.
Sevilla's first win in four weeks lifted it within three points of the Europa League positions.
Deportivo La Coruna goalkeeper Daniel Aranzubia scored in injury time to give his team a 1-1 draw at Almeria, and Racing Santander beat Getafe 1-0.
Almeria looked set to convert Pablo Piatti's 49th-minute opener into three points, but Aranzubia headed home a corner right on the final whistle in the 95th to record the first goal scored by a goalkeeper with a header in the history of the Spanish league.
"I did what I see my teammates do," Aranzubia said. "I had come forward other times, but never scored a goal. I am thrilled."
In Madrid, Pablo Pinillos scored the 88th-minute winner for Racing Santander from the penalty spot after Getafe defender Ivan Marcano was sent off for pulling down Giovani Dos Santos with only the keeper to beat.
Mallorca is at Real Sociedad on Monday.
 
Jose: Pressure on us not Barca


RivalsDM



PRINT RSS

19 comments »

Updated Feb 20, 2011 6:15 AM ET
Real Madrid coach Jose Mourinho believes the pressure is on his side and not leaders Barcelona in the race for the Primera Division title.
Madrid had trailed Barca by seven points earlier this month but have now trimmed that difference by five points after beating Levante 2-0 at the Bernabeu.

Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats

Barca, having been held at Sporting Gijon last weekend and then losing 2-1 at Arsenal in the Champions League in midweek, could be feeling the heat ahead of tonight's visit of Athletic Bilbao, although Mourinho believes it is still his side that is under pressure.
He said: "We have to win and keep winning. For many seasons I've been in front and everybody was asking me if I was feeling the pressure, and I said no, I wasn't feeling the pressure. The pressure is for the second-placed team, not for the first.
"The second place team needs to win every match, so the pressure is on us. But we've won two important matches the last two (Espanyol and Levante), the next one is important too, so you have to keep going and believe, and wait and see."
He added about the Levante win, which saw the Portuguese make a number of changes ahead of their Champions League trip to Lyon: "I liked that my team played a serious match. These games ahead of Champions League matches can be complicated because players may focus more on the European competition. The team played well and was very focused."
Madrid beat Levante 8-0 in their previous meeting at the Bernabeu in the Copa del Rey before Christmas and looked set for another big scoreline when Karim Benzema put them ahead after just six minutes.
However, despite spending almost the entire match camped in Levante's half, Madrid could only net one more goal, with Ricardo Carvalho slotting in just before the interval.
The victory was Madrid's 22nd successive home win in all competitions and marked nine years since Mourinho last suffered a home defeat in the league, which came on February 23, 2002, when his Porto team lost to Beira Mar.
It also gave them a morale boost ahead of Tuesday's Champions League last-16 first leg clash with Lyon in France. Madrid have been knocked out at this stage in each of the last six seasons - including at the hands of Lyon last season.
Looking ahead to that clash, Cristiano Ronaldo said on his club's website: "The Lyon match is very important and it will be difficult, but we are motivated. Lyon are a team that is always in the last 16. We are going there to play well and win."
 
Valencia's Aduriz out four weeks with ankle sprain


storypage_APlogo_01.png




PRINT RSS

2 comments »

Updated Feb 20, 2011 10:49 AM ET
Valencia's Aritz Aduriz will be sidelined for four weeks with an ankle sprain.




Team doctors say the Basque striker sprained his left ankle during Saturday's game against Sporting Gijon.
Aduriz is Valencia's top scorer with nine league goals this season.
He will likely miss the second leg of Valencia's round of 16 Champions League tie against Schalke on March 9.
Valencia is currently third in the Spanish league.
 
Timu ya Jiji la Mbeya yatesa Morogoro

Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Morogoro; Tarehe: 21st February 2011 @ 22:00 Imesomwa na watu: 46; Jumla ya maoni: 0








TIMU ya netiboli ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya, imefanya mauji, kwenye michuano ya ligi daraja la pili inayoendelea kwenye Uwanja wa Jamuhuri wa mjini Morogoro, baada ya kuiangushia kipondo cha mabao 47-16 timu ya Tigo ya jijini Dar es Salaam..

Wakati timu hiyo ikipata ushindi huo katika robo fainali za ligi daraja la kwanza, timu ya netiboli ya Tandahimba ya Mtwara imejikuta ikipata kipigo cha mabao 36-16 kutoka kwa mpinzani wake Ruvu JKT.

Timu nyingine ambayo nayo imeanza vizuri katika mashindano hayo ni Polisi Arusha iliyoitandika mabao 27 -24 Ruangwa ya mkoani Lindi.

Akizungumza na waandishi, Mkufunzi wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Mary Protas amesema, timu zote zimeonyesha ushindani mkubwa na hali hii inatokana na wachezaji kufanya mazoezi pamoja na umakini wao pindi wawapo uwanjani.

Alisema, chama kinategemea kupata timu bora zitakazofanikiwa kuingia daraja la kwanza na kwamba kupatikana kwa timu hizo kutaleta changamoto kubwa katika mchezo wa netiboli ambao umekuwa ukisahaulika sana kwa jamii.

Kwa upande wake , kocha wa Hamambe Joyce Mwakifamba, ametamba timu yake kuchukua ushindi na kufanikiwa kuingia ligi daraja la kwanza kwani tangu mashindano yaanze timu hiyo haijawahi kufungwa.

Alisema, siri kubwa ya timu hiyo kujipanga, mazoezi, umakini wa wachezaji pamoja na wadhamini wa timu hiyo ambao ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuwajali wachezaji kwa kuzingatia posho na malazi.

Timu 11 zilishiriki ligi hiyo, ambapo nane ndizo zilizoingia hatua ya pili ambazo ni Rwangwa, Tigo, Ruvu JKT, Polisi Pwani, Polisi Arusha, Hamambe ya Mbeya, Alliance One na Tandahimb
 
Wanaowania Kili Music Awards watajwa


Na Addolph Bruno

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro imetangaza wasanii watakaoshiriki tuzo za Kilimanjaro 'Kilimanjaro Music Awards'
mwaka 2011 katika kategori 22.

Fainali za tuzo hizo, ambazo hufanyika kila mwaka kwa zinatarajiwa kutolewa Machi 26, mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa bia hiyo, George Kavishe alisema wasanii hao wameteuliwa kwa ustadi mkubwa na kampuni ya Innovex iliyobobea katika fani hiyo, baada ya kuyafanyia kazi kwa umakini maombi ya wadau wa muziki waliyokuwa wakituma.

Alisema wasanii walioteuliwa wamegawanywa katika makundi ambayo yanahusisha majina matano, mpaka sita ya wasanii wanaowania tuzo mbalimbali zikiwemo za Msanii Bora wa Kike wa Muziki na Msanii wa Bora Muziki wa Kiume.

Wengine ni Mwimbaji Bora wa Kiume, Mwimbaji Bora wa Kike, Wimbo Bora wa Taarabu, Wimbo Bora wa mwaka na Wimbo Bora wa Kiswahili wa Bendi na Msanii mpya anayechipukia.

Kavishe alisema tuzo hizo pia zitashirikisha wasanii watano kutoka nchi za Afrika Mashariki, ambao watashindania tuzo ya wimbo bora ya mwaka kupitia nyimbo zao.

Nyimbo zitakazoshindaniwa na wasanii hao ni Nitafanya wa Kidumu akishirikiana na Lady Jay Dee, Kare wa kundi la P-Unit, Songambele wa Alfa wa Rwanda akishirikiana na AY, Vuvuzela wa GoodLife na Kasepiki wa Bebe Cool wa Uganda.

Aliwataja baadhi ya wasanii walioteuliwa ni pamoja na Linah, Shaa, Mwasiti, Khadija Kopa na Lady Jay D wanaowania tuzo za msanii bora wa kike ambapo tuzo za msanii bora wa kiume zinawaniwa na Abass Kianzi '20%', Ali Kiba, Barnaba, Belle 9, Banana Zoro pamoja na Diamond.

Wengine ni Gelly wa Rymes anayewania tuzo ya wimbo bora wa mwaka kupitia kibao chake cha Mama Ntilie, Sam wa Ukweli na kibao cha Sina Raha, pamoja na Chegge na wimbo wa Mkono Mmoja, huku tuzo za mtayarishaji bora wa mwaka zikiwaniwa na Marco Chali, Lamar, Man Water, Bob Junior na Pancho Latino.

 
BFT kuwapa semina makocha wa ngumi


Na Mwali Ibrahim

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), linatarajia kutoa semina kwa makocha wote wa timu zitakazoshiriki mashindano ya taifa ya
Klabu Bingwa Februari 25, Dar es Salaam.

Mashindano hayo, yanatarajia kufanyika Februari 26 hadi Machi 5 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo timu 21 zimethibitisha kushiriki.

Akizungumza Dar es Salaam jana Msemaji wa BFT, Eckland Mwaffisi alisema watatoa semina hiyo elekezi kwa makocha hao, ili kuwaweka tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

Alisema maandalizi ya mashindano hayo, yanaendelea vizuri na katika kuhakikisha wanafanikisha mashindano hayo wameunda kamati tatu ziatakazokuwa na jukumu la kuyaiwezesha michuano hiyo.

Alizitaja kamati hizo kuwa ni Kamati ya Mipango, Kamati ya Fedha na Kamati ya Mapokezi ambazo zinaundwa na wajumbe kutoka BFT na wengine kutoka klabu zitakazoshiriki.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom