Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,508
- 911,249
- Thread starter
- #2,421
Fifa yabuni kamati ya kupambana na rushwa Monday, 03 January 2011 18:11
BERNE, Uswisi
RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa ( Fifa), Sepp Blatter amesema umefika wakati wa kuanzisha chombo cha kupambana na rushwa ndani ya shirikisho hilo ili kujenga heshima ya mchez huo duniani.
Blater alisema juzi kwamba Fifa itaunda kamati ya kupambana na rushwa ambayo itachunguza, kusikiliza madai yote kuhusu rushwa katika soka ambayo mwaka jana ililitikisa shirikisho hilo.
Pia, Blatter amekosoa mfumo wa mikwaju ya penalti, akipendekeza kwamba lilikuwa kosa kuutumia, kwa kuwa unamgeuza mchezaji mmoja kuwa kisingizio.
Blatter, pia alipendekeza kwamba mikwaju ya penalti si sahihi mwisho wa mchezo ambao umemalizika kwa sare hasa kwenye mashindano makubwa.
"Bado majadiliano yanaendelea, kwa mtazamo wa kimichezo hasa soka, tunatafuta suluhisho kama timu ili kupata matokeo mazuri ," alisema.
"Si kitu kizuri kuamua mchezo kwa penalti, ambako mchezaji mmoja anayekosa hufanywa sababu."
Blatter alisema kupata suluhisho kwa mechi ambayo imemalizika kwa sare ni kazi ya kamati maalum ambayo tayari imeundwa na imeanza kulifanyia kazi kabla ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Mwaka jana, wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji ya Fifa kutoka miongoni mwa wajumbe 24 , Reynald Temarii kutoka Tahiti na Amos Adamu, Nigeria walisimamishwa kwa madai ya kutaka kuuza kura zao wakati wa mchakato wa kuteua nchi ambazo zitaandaa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022.
Wawili hao walifichuliwa na ripoti ya gazeti la Sunday Times la Uingereza ambalo waandishi wake walijifanya maofisa kutoka nchi ambazo zilikuwa zikiomba uenyeji huo.
Kutokana na kashfa hiyo, Temarii na Adam waliondolewa katika orodha ya wajumbe waliopiga kura Desemba 2 ambao walitoa uenyeji kwa Russia mwaka 2018 na Qatar mwaka 2022.
"Binafsi nitasimamia kamati hiyo ili kuhakikisha hakuna rushwa Fifa ," Blatter alisema katika mahojiano na gazeti la Uswisi la SonntagsZeitung. "Kamati hiyo itaimarisha kiwango cha kuaminika kwetu na kutupa sura mpya."
Alisema kamati yake hiyo itaundwa na wajumbe saba hadi tisa, ambao si kutoka ndani ya masuala ya michezo, bali siasa, fedha, biashara na utamaduni.
Rais huyo wa Fifa alieleza kuwa binafsi hatakuwa mjumbe wa kamati hiyo.
"Kamati itakuwa huru ili kuweza kufanya kazi zake na kuaminiwa ," alisema . "Ninataka kuwasilisha tume hiyo kwenye mkutano wa Fifa mjini Zurich mwanzo waJuni."
Tayari Fifa ina kamati ya maadili ambayo ndiyo iliyoshughulikia suala la rushwa ambalo liliwakumba maofisa wengine wanne waliosimamishwa.
Blatter, ambaye tayari ameeleza kuwa atagombea tena urais wa Fifa mwezi Juni, alisema kwamba hakuwahi kuwa na mpango wa kujiuzulu licha ya shirikisho lake kukumbwa na kashfa.
"Hakuna muda ambao niliwahi kujiwa na mawazo ya kujiuzulu ," alisema . "Nitaendelea kuwa hapa kwa muda mrefu zaidi . Lakini, ninahitaji kusaidiwa na kuwa na nguvu za kukabiliana na wakosoaji wangu."