Habarini wana MMU,
Jana ilikua ni siku tulivu sana kwangu toka asubuhi hadi mida ya saa tisa hivi alasiri , lakini Mambo yaligeuka mambo ghafla kama bahari bs ilichafuka sana aisee .
Hili sijui ni pepo jaman mweee! An mtu una wachumba watatu halafu wote unawapenda sana tena sana wala hutaki apungue ata mmoja , na kila mmoja nlikua nampromis kumuoa japo hakna aliekua anapenda nioe huo wakati nliopanga mimi( nlikua nampromise kila mmoja kua baada ya miaka miwili ijayo namuoa) walionesha kukubaliana na hilo pia nliendelea kuwasiliana vizur kabisa nao japo wapo mikoani.
Jaman siku ya jana ilikua ngumu sana kwangu adi nimeamka nayo ( badala ya kuamka na hangover basi kijana nimeamka na pombe .
IKO HIVI.....
1. siyo kawaida yangu , jana nkiwa humu Jf mara ghafla hisia zinkantuma niingie Fb nimsearch bebee kweli nkamsearch mara tip post ya kwanza kabisa nakuta pic ya baby yupo kansan kavaa yale magauni yao na kajamaa kamevaa eti suti afu pembeni wapambe,daaaa nliumia sana sikuamini ikabidi nisone comments maan zlikua zinamiminika sana hapo ndio nkaamini, lakini nlijikuta kama namcheka hivi halafu machozi kwa mbali km nko kukata kitunguu maji (kicheko + machozi) nlijikuta na mimi nacomment then nafuta×3 hivi then fasta nka log out nkaona nkimuuliza huyo ntaoneka dhaifu," weee mwache atantafuta tu huyu" ( nkawa naleta mazoea kumbe ndo imetoka hivyo )
Sasa apo Nkapata akili ya kuwasearch mabebe angu wote .
2. Huyu nae daaa shenz kabisa, kama waliambiana sijui, let call it a day! dadeQ
nae post ya kwanza mekuta kampost jamaa caption ikiwa " Nakupenda sana mume wangu , baba watoto watoto angu. Jaman inaumaa atarii, Moyo ulilia paaaaa nkapitisha fasta chini ake ili nione post nyingine nkakuta kuna maneno tu yale ya taarabu taarabu hivi nkayasoma kwa makini kwa mbali nkahis kama yananiusu mimi lakini nkapotezea kwa lazima, baada ya hapo nkaamua kwenda kuoga kwanza maana sura ilikua kama nimepigwa na mawe na macho yalikua mekundu sanaa
Nliporudi tu ndani nkaamua kuangalia comedy tu ndani ili nifute kabisa sura ya huzuni , hapo nkawa safi kwa kweli, nkarudi zangu home Jf nkaperuzi weeee kuna akili, hisia sijui ilitoka wapi labda kwa vile nlikua metoka kusoma thread za kiroho za ndgu Mshana jr, Hisia hizo zilinituma nirudi fb nkamalizie kumsearch huyu baby mwingne, kweli nkafanya hivo nkijipa moyo na furaha kua huyu aaaah hawezi kufanya ujinga wa hao kabisa
3.ndgu zangu siku ya kufa nyani miti yote huteleza nimeamini! Jana siisahau kwa kweli , huyu nae kwikwi tena nilimpa cheo cha juu kabisa cha mapenzi , tena yeye alikua anataka kuja kabisa niliko nlikua nampga chenga maana mifuko ilikua imetoboka istoshe nauri ya kumtoa aliko ni mbali kidgo na skutaka apate shida maan ni chombo kweli nkahofia atakuja kupauka tu kwangu, kumbe Mungu alikua anatoboa mifuko ili nisimtumie nauri aje , unazani kwa nini?
Yeye nlipoingia tu nkakuta ameji selfie mwenyew akiwa amevaa dilaa na kitumbo kinaonekana kabisaa(mimba) ! hapo nlizima tu simu yangu nkapagawa kabisa nkahisi kuna mtu ananirogaa tena bado hajatoka kwa Mgaga ndio mana mapigo makali, nkapata wazo la kuogea CHUMVI YA MAWE kama ushaurivyo mshana Jr, nkasahau kua dozi yake si ya siku moja kama nlivozan kwa mda ule, yeye huyu ilibidi nimtafute , kweli nlimtafuta ilikua vurugu na akakili me sieleweki eti Nkamuuliza Kwahiyo ulivokua unataka kuja huku ingekuaje na huo ujauzito? Akasema kwani huwezi kulea mimba ya mwenzio mbona kawaida tu!
"Jaman kile usichopenda kufanyiwa na basi nawe usikifanye"
Malipo ni apa apa Chini ya jua.