Hali ya ndoa nyingi siyo kama inavyoongekea, nafikiri kuna chumvi nyingi juu ya tuhuma hizi. Marafiki zangu, ndugu zangu, wafanyakazi wenzangu wengi tu wako happy kwenye ndoa zao. Ni wachache tu wenye figisu figisu.
Halafu pia Ndo nyingi hazivunjiki kama inavyosemwa. Nimejaribu kuangalia katika ma classmate, workmates na ndugu ninaowafahamu ambao wamefunga ndoa kuanzia 2005, ni wa 4 tu kati ya 46 ndo wametengana, mmoja sababu ya michepuko ya mwanamke, wawili tabia za wanaume lakini siyo michepuko, na mmoja tuhuma za ushirikina kwa mwanamke.
Nafikiri tunapenda ku generalize sana mambo bila kuwa na data. Naamini ndoa nyingi ziko imara na zina upendo ukiacha mikwaruzano ya hapa na pale ambayo ni kawaida sana.