balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 14,416
- 12,511
Kwa siku mbili hizi za Jana na Leo nimepata nafasi ya kufuatilia bunge mubashara toka Dodoma. Nimetazama na kusikiliza lakini ile radha ya bunge haipo kabisa.
Kuna wenye hoja lakini kwa jinsi wanavyoziwasilisha ni kwa kiwango kisichokidhi viwango vya bunge.
Kuna aliyekuwa na hoja ya kuhalalisha pombe za kienyeji lakini uwasilishaji wake uliifanya hoja kuonekana haina mashiko.Eti akalazimika kwenda na vyombo bungeni!.
Ilikuwa ni hoja kuntu lakini ikawasilishwa kwa kiwango cha chini. Kuna mbunge mmoja alishindwa kujua kwamba mbunge akiongea jambo ndani ya bunge ana Kinga kwa mujibu wa ibara ya 100 ya katibu yetu,yeye alienda kumkosoa mwenzake nje ya bunge.
Leo Kuna mbunge wa viti maalumu toka Arusha alipokuwa akichangia, kila baada ya maneno mawili au matatu lazima ataje Mheshimiwa spika.
Kuna yule aliyesema eti tunafundisha kwamba sisi tulitokana na sokwe, akaomba profesa awasaidie mbona hakuna continuation wa manyani na masokwe kuwa binadamu.Hapa nikagundua nadharia ya Evolution haikueleweka.
Nimpongeze Mheshimiwa Kishimba mbunge wa Kahama aliyeomba elimu mbadala, hiyo nadhani ndiyo iliyo hoja ya msingi.