Michango Tumboni ni nini?

Tosha

Member
Aug 18, 2011
72
19
Kwa heshima kubwa naomba msaada wa kuelimishwa hii kitu nimekuwa nikiisikia huku mitaa lakini sijapata kujua hasa ni kitu gani?mara ooh inasumbua kwenye uzazi(wamasai wamekuwa wakiuza sana dawa za michango tumboni),mara wengine wanasema ni minyoo tu inakuwa mingi tumboni na kadhalika na kadhalika sasa naomba kwa wanaojua hili suala la kuwa na michango tumboni!hii hali ni ugonjwa gani?nini kinasababisha?madhara yake ni yapi?na tiba yake hasa ni nini?
natanguliza shukrani kwa wote nawasilisha
 
Daktari: Je, minyoo inasababisha kuwashwa sehemu ya haja kubwa?

KUSIKIA muwasho sehemu za haja kubwa si jambo geni kwa wengi na pengine wewe unayesoma makala hii ulishawahi kupatwa na tatizo hili.Hili ni miongoni mwa matatizo ambayo husumbua kwa mda mrefu na pengine bila kupatiwa matibabu, kwani watu huona aibu kusema kwa vile ni sehemu nyeti ya mwili wa binadamu.

Wakati mwingine ule muwasho husumbua ukiwa katika kadamnasi, hivyo inabidi mhusika kwenda sehemu ya faragha kujikuna, kwani kufanya hivyo kwenye kadamnasi humfanya ajisikie aibu.Hata wale wanaomuona mtu akijikuna maeneo nyeti kama hayo hushangaa kwa kuwa si jambo la kawaida. Ukweli ni kwamba katika maisha binadamu inatokea kuwashwa sehemu ya haja kubwa.

Minyoo na muwasho
Sababu za kuwasha sehemu ya haja kubwa ni nyingi; lakini leo nitajibu swali la msomaji linalohusiana na minyoo na hasa ile ya tumboni.

Sehemu ya haja kuwa ni sehemu ya mwisho kabisa ya utumbo mpana ambayo hupitisha kenyesi kutoka tumboni. Ni kweli kabisa kuwa kuna minyoo inayosababisha kuwasha sehemu hii. Minyoo hii pengine ulishaiona kwa macho kwani ina rangi nyeupe na wakati mwingine utaona imeshika kama utando kwenye makalio ya nyuma ya mtoto au miguu yake kwani inaweza kutoka tumboni yenyewe.

Kwa kiingereza minyoo hii ina majina kibao. Wengine huiita ‘pinworm', ‘seatworm' au ‘threadworms'. Kwa jina la kitaalamu minyoo hii hutwa ‘Enterobius Vermicularis'.

Tatizo la minyoo hii huwakumba watoto wa shule na wale wanaokaribia kuanza shule zaidi. Unaweza kukuta nusu ya wanafunzi wana minyoo hii kwa sababu inaambukiza na kwenye familia wanaweza kuwakumba watu zaidi ya mtu mmoja.
Si kawaida kwaingia watu wazima ila unawaza kuukuta kwa mama mzazi wa mtoto mwenye minyoo. Pengine kwa sababu ya mahusiano ya mama na watoto kuwa karibu (kama kumuogesha mtoto nk).

Minyoo inaambukiza kwa njia ya kinywa. Mayai ya minyoo kutoka haja kubwa yanaweza kuishi kwa muda wa wiki mbili kwenye ngozi, nguo, taulo, shuka, blanketi; hivyo ni rahisi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na hasa kama atakula bila kunawa mikono.

Tofauti na minyoo ya aina nyingine, ugonjwa huu zaidi ya kuwasha sehemu ya haja kubwa na ukeni kwa wanawake, mara chache sana kuumwa tumbo, kukosa hamu ya kula na kukosa usingizi.

Sababu zingine za kuwashwa sehemu ya haja kubwa ni fungusi, viotea au heamorrhoiss, choo ngumu, kula viungo vikali ikiwemo pilipili kwa wingi.

Tunashauriwa kuhakikisha kuwa tunanawa kwa sabuni kabla ya kula. Tuwe na tabia ya kuwafanyia watoto uchunguzi na kuwapa dawa za minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu, kufanya usafi wa nguo, taulo na mashuka mara kwa mara.
 
michango is myth. I hate the word as it lacks specificity to any disease
 
Kwanza michango ni nini na ina dalili gani
Their little white worms that come out your asshole at night and lay eggs.WHen you scratch your ass your fingers pick up the worms then you put it in your mouth.This is really common! if you want to catch these worms put tape over your asshole and they can lift out.They are half an inch and you'll have to catch them at night. They're little parasites and a sympton of them are a itchy asshole.
The left side is a more severe case of worms that live inside humans

The ride side is the common pin worm.
ngbbs475df96d9d495.jpg


Hiyo ndio michango au minyoo
 
Roundworm-Enterobius (Human Pinworm)

Roundworm—Enterobius vermicularis (Pinworms or Seatworms) causes Enterobiasis. The severity of disease depends upon the worm load, since most nematodes cannot multiply in their host. The picture on the right shows what you see on a positive pinworm scotch tape test under the microscope (after staining) and upon an endoscopic rectal exam (right picture):
Note that the adult (white) worms are greatly enlarged. These worms are actually one about a quarter of an inch long and are fairly clear so they are hard to see.
This particular worm is only passed to humans via humans by fecal-oral route. The eggs can also stick to bed sheets or become airborne. Adults mature and settle in the small intestine, colon and cecum. The females sneak out at night and lay eggs around the perianal areas then sneak back into the rectum .
Lifecycle of the Pinworm:
Enterobius (Human pinworm) lifecycle
 
Naomba kuuliza Dada yangu anamimba ya wiki 36 ilaanawashwa sana tumbo sababu itakuwa nini naombeni ushauli
 
Back
Top Bottom